Showing posts with label Bongo Flavor. Show all posts
Showing posts with label Bongo Flavor. Show all posts

Saturday, March 25, 2017

http://revenuebrust.com/?refcode=4345

http://revenuebrust.com/?refcode=4345

Thursday, August 1, 2013

Agness Masogange Amponza Madee South Africa



Kwenye Exclusive interview na millardayo , Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana (Akina Masogange )  waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.


Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.


Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.


Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.


Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye foleni wanaposimama watu ila kwa pembeni kidogo, ni sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee anakwambia jamaa walinong’onezana sana wakati wanamkagua.


Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection walimuomba radhi baada ya kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika kulivuruga sana begi lake.

Source: Milard Ayo 

Saturday, July 27, 2013

Rafiki Wa Sharo Milionea Adaiwa Kudhulumu Mali za Marehemu

-->


MALI zilizoachwa na aliyekuwa staa wa vichekesho Bongo, marehemu Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Milionea’ zinadaiwa kudhulumiwa na rafiki yake wa karibu aliyejulikana kwa jina moja la Suma, Risasi Jumamosi lina  mkanda wote.


MADAI
Chanzo chetu kilichoongea na gazeti hili Julai 25, mwaka huu kilisema Suma anadaiwa kudhulumu mali za Sharo kufuatia kupewa madaraka ya kufuatilia na kuuza baadhi ya vitu bila fedha kumfikia mama wa marehemu, Zainabu Mkieti.

MAMA WA SHARO AFUNGUKA
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Alhamisi iliyopita, mama huyo alikiri kuonekana kwa njama za Suma kudhulumu mali hizo likiwemo gari aina ya Opa lenye namba za usajili T 879 CAR na shilingi milioni 1. 2 za seti ya sofa alizonunua marehemu siku chache kabla ya kifo.

AZUNGUMZIA GARI
“Kweli nahitaji msaada ili nifanikishe kupata mali za mwanangu kwani kuna mambo hayaeleweki, kikubwa ni gari ambalo baada ya arobaini tulimpa Suma akaliuze kwa shilingi milioni kumi na moja na anipe fedha hizo lakini hadi sasa sijaona hata shilingi mia. Arobaini ya Sharo ilikuwa Januari 2013.

FEDHA ZA MASOFA
“Ukiachilia mbali gari, kuna fedha za masofa shilingi milioni moja na laki mbili sijazipata hadi leo, Suma aliahidi kunipa baada ya kuuza masofa hayo kwa dada yake na nimeshajaribu kuzungumza naye lakini hakuna majibu ya ukweli.
“Kabla ya Tuzo za Kili Music, Juni, mwaka huu, mimi nilikuja Dar na nikaongea na Suma na mama yake kuhusu fedha hizo, nilipomuuliza kuhusu gari, Suma akasema hataliuza na badala yake baada ya siku mbili angenitumia fedha lakini hadi leo hii simpati kwenye simu.

FEDHA ZILIKUWA ZITUMIKE KWA UJENZI
“Nakosa njia rahisi ya kuzipata fedha hizo maana huyu Suma naona kama mjanja, nilikuwa nataka kuanza ujenzi  wa nyumba kwenye kiwanja alichokiacha marehemu lakini naona kama muda unakwenda,” alisema mama mzazi wa Sharo.

MAJIBU YA SUMA
Suma baada ya kupatikana kwenye simu yake ya kiganjani na kusomewa mashitaka hayo, alidai ameshaongea na mama Sharo lakini alisafiri na ni kweli alikuwa hapatikani kwenye simu.
“Mbona nimeshaongea na mama na mambo tumeyaweka safi, ujue nilikuwa South Africa (Afrika Kusini) nina kama wiki tatu tangu nirudi na kusema kweli sijawasiliana na mama Sharo ila tutamalizana tu mambo yakiwa vizuri,” alisema Suma.

KUMBUKUMBU
Sharo Milionea alifariki dunia kwa ajali ya barabarani Novemba 19, 2012 iliyotokea kwenye Kijiji cha Songa Maguzoni, Muheza Tanga akiwa ndani ya gari aina ya Harrier lenye namba za usajili T 378 BVR likitokea Dar es Salaam kwenda Tanga.
Alizikwa Novemba 23 kijijini kwao, Lusanga, Muheza, Tanga.

Source: GPL

Wednesday, July 24, 2013

Aibuu "SHILOLE" Aiba Simu za "Daimond", Alipewa na Ndugu wa Daimond South Africa, Hajampa Mwenyewe Hadi Leo!!!!



Stori:Shakoor Jongo na Musa Mateja
STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.
Mfano wa aina ya simu anazo daiwa kuiba Shilole
Msanii huyo alikumbwa na kasheshe hilo Julai 19, 2013 nyumbani kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sinza Mori, Dar.
Siku hiyo Diamond alikuwa akifuturisha na aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo mastaa lakini nusura futuru iingie doa kufuatia zogo hilo.
ISHU ILIKUWAJE?
Ndugu wa Diamond aitwaye Majaliwa Majuto ‘Q Boy’ alidai ndiye mwenye simu hizo. Alisema miezi kadhaa iliyopita, Shilole alikwenda nchini humo kufanya shoo ya muziki. Wakati wa kuondoka alimpa simu tatu, Ipad, Samsung Galaxy na Blackberry ili akifika Bongo ampe Diamond lakini msanii huyo hakufanya hivyo.
“Alikuja Sauzi kufanya shoo, wakati wa kuondoka nilimpa simu tatu amletee Diamond lakini nashangaa hakufanya hivyo na mimi tangu nirudi Bongo simpati, kila nikimpigia simu hapokei, leo ndiyo tumekutana hapa kwa Diamond,” alilalama Q Boy.
DIAMOND ALIAMBIWA SIMU ANAZO SHILOLE
Alisema awali akiwa nchini humo baada ya kumkabidhi mali hizo, alimpigia simu Diamond na kumtaarifu kuwa ‘mzigo’ anao Shilole, akashangaa staa huyo kujibu kwamba hajazipata wala hajamwona Shilole.

SHILOLE AJITETEA
Katikati ya mzozo huo, Shilole alijitetea kwa kusema: Mi namdai rafiki yake fedha yangu ya shoo iliyobaki, kama shilingi laki nane hivi ndiyo maana nikaamua kuzizuia simu za huyu (Q Boy) hadi nimaliziwe pesa yangu.
Hata hivyo, katika sakata hilo ilielezwa kuwa Shilole na Q Boy hawakuwa na makubaliano yoyote kuhusu shoo hiyo na simu hizo hivyo madai ya mwigizaji huyo ni ‘usanii’ tu.

MAMA DIAMOND AINGILIA KATI KUOKOA
Zogo hilo lilipopamba moto na kuashiria kuvurugika kwa amani, mama mzazi wa Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ aliamua kuingilia kati na kuagiza suala la kudaiana simu lifanyike kesho yake (Jumamosi) kwa vile siku hiyo haikuwa muafaka.
“Jamani! Jamani! We nani, Shilole na we Majaliwa, naomba kwa leo muepusheni shetani kwani hapa si mahali pake, ila kesho tutaitana na kumaliza suala hili, mimi mwenyewe nitalisimamia,” alisema bi mkubwa huyo na kumaliza henyahenya iliyoibuka.

JUMAMOSI YAFIKA, KIKAO VIPI?
Jumamosi, mapaparazi wetu walifuatilia ishu hiyo nyumbani kwa akina Diamond na kuulizia ili kujua kama kikao cha usuluhishi kilifanyika kama mama Nasibu alivyoagiza.
“Mh! Sijaona kikao chochote, kwanza Shilole mwenyewe akipigiwa simu hapokei,” alisema ndugu mmoja wa Diamond huku akiomba hifadhi ya jina lake.

MSIKIE DIAMOND
Juzi, Diamond alipopigiwa simu na kuulizwa kama anaijua ishu ya simu, alikubali.
Staa huyo alisema anashindwa kuingilia kati sakata hilo kwa sababu wahusika wote ni watu wake wa karibu kikazi.
“Yeah! Ishu ni kweli ipo, lakini mimi nilijiweka kando mapema, nikamwambia dogo (Q Boy) afuatilie mwenyewe baada ya kuona Shilole haeleweki.
“Unajua Shilole ni mwanamuziki mwenzangu, dogo yupo ndani ya Kampuni ya Wasafi Entertainment (ya Diamond), sasa kukomaa na ishu za simu tu nahisi itanishushia hadhi, napiga shoo za hela nyingi halafu leo nakomaa kwa hela ndogo, inakuwa siyo,” alisema Diamond.

SHILOLE TENA
Baada ya kuzungumza na Diamond, Shilole alipigiwa simu na kuomba kufafanua kwa undani ishu hiyo ambapo katika hali isiyotarajiwa, alimlalamikia paparazi wetu akidai anapendelea katika sakata hilo.
“Nyiye mnamtetea tu yule dogo, mimi sina tatizo, kama rafiki yake (aliyemuitia shoo Afrika Kusini) akinilipa hela yangu nawapa simu zao,” alisema Shilole.
Msanii huyo alikwenda mbele zaidi kwa kumwambia paparazi kuwa atatia timu kwenye Ofisi za Global Publishers ili kuzungumzia suala hilo na viongozi.
Baadaye Shilole alifika ofisini kwetu na kufafanua juu ya sakata hilo ambapo alirudia kukiri kuzuia simu hizo akidai kwamba anamdai Q Boy hivyo mpaka atakapomlipa ndiyo atampa simu zake.

Q BOY NAYE TENA
Kwa upande wake, Q Boy alipozungumza na paparazi wetu siku hiyo alisema amekusudia kwenda kufungua kesi kituoni ili apewe msaada zaidi wa kisheria kwa vile simu hizo zinamuuma hasa ukizingatia kuwa yeye siye aliyempeleka Shilole Afrika Kusini kufanya shoo.
“Mimi leo (Jumatatu) nimebanwa sana, kuna sehemu nakwenda na Diamond, nadhani nitamaliza jioni. Lakini kesho (Jumanne) nitaamkia polisi kufungua kesi nione watanisaidiaje?” alisema Q Boy.

POLISI AGUSIA ISHU
Risasi Mchanganyiko lilizungumza na askari mmoja kutoka Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kummegea mtiririko wote, kisha kumuuliza kama kuna kesi ambapo alijibu:
“Japokuwa mimi si msemaji wa jeshi (la polisi), lakini ishu kama hiyo shitaka lake lipo, ni wizi wa kuaminiwa. Unajua wengi wanadhani kuibiwa lazima mtu uwe hujui, lakini mtu akifanya kama hivyo alivyofanya huyo msanii nani sijui (Shilole), kama ni kweli, kosa linakuwa wizi wa kuaminiwa endapo atafikishwa polisi.”

DIAMOND, Q BOY WALIFANYA MCHEZO?
Hata hivyo, baadhi ya watu walioshuhudia sakata hilo walikuwa na maswali kibao yaliyokosa majibu.
Swali la kwanza: Shilole alikwenda kufuturu kwa mwaliko wa Diamond na alijua staa huyo na Q Boy ni wamoja na simu alizopewa ilikuwa amletee msanii huyo, kwa nini alikwenda huku akijua ana msala?
Swali la pili: Kama Shilole alikwenda akijua Q Boy hayupo Bongo, je! Si kwamba ulikuwa mpango wa wawili hao kumwita ili wampe kibano ateme simu zao?
Swali la tatu: Je, ni kweli Shilole alizuia simu ili amaliziwe deni lake kwa mtu aliyemuitia shoo Afrika Kusini au shetani alimwingia baada ya kutua Bongo na kuamua kuzitumia hasa ikizingatiwa kuwa siku hizi mambo ya Instagram ndiyo habari ya mjini?

SOURCE: GPL

Dah!! Kumbe Nay wa Mitego Mtoto wa Mama!!!


Mkali wa Muziki gani, True Boy Ney wa Mitego, Mzee wa Mkong'oto Jazz Band, alikutwa na Kamera ya Paparazi akiwa kajiachia katika mapaja ya mama yake mzazi huko maeneo ya kwao, kwa picha hii tunapata ukweli wa ule usemi usemao" Mtoto kwa Mama ....." Hata uwe Mbabe na Njemba Kiasi gani, Kwa Mama Utapiga Kimya kama asemavyo Ney.


Picha Credit: GPL

Thursday, July 18, 2013

Mzee Magari wa Bongo Movie apiga Hodi Bongo Flavor, Atoa Single ya Kwanza!!!

-->

Maisha ni kutafuta na si kutafutana, Yule Mkali na mkongwe wa Bongo Movie, Mzee Charles Magari amefunguka zaidi na kuangalia upande wa pili wa shilingi baada ya kuamua kujiingiza pia katika Bongo Flavour, Ameshatoa Single yake ya kwanza, ipo mtandaoni kwa jina la "Dar Raha" Hope Mzee Mzima ataliweza Game maana Ukubwa Dawa.

Monday, July 8, 2013

Uwoya yamkuta, Aambulia Matusi ya Nguoni Baada ya Kumfananisha Diamond na Michael Jackson

-->


Wiki iliyopita Muigazaji wa Filamu Inchini, Mwanadada Irine Uwoya aliandika katika Ukurasa wa Istagram ya kwamba msanii wa Bongo Fleva, Diamond ndiye wa pekee ambaye anaweza kumrithi mkali wa Pop Mareheme Michael jackson kwa Jinsi msanii huyo alivyojuu kwa sasa. Maneno hayo ya mtazamo wake yaliwakera baadhi ya mashabiki na kuanza kumporomoshea matusi ya nguo kwa mtazamo wake huo, wengine walihoji huku wakimtukana, iweje amananishe aliyekufa na aliye hai au sababu Diamond aliku...!!! Ndo mambo ya Wabongo hayo.

Angalia Picha za Diamond na CMB Katika tamasha la matumaini Jana.


Fireworks wakati mkali kutoka 254, CMB Prezzo akiingia stejini.
Diamond akiwachizisha mashabiki kwa wimbo wake 'Ukimwona'.…
Fireworks wakati mkali kutoka 254, CMB Prezzo akiingia stejini.
Diamond akiwachizisha mashabiki kwa wimbo wake 'Ukimwona'.
Prezzo akiwa kwa steji na Nelly Kamwelu.
Diamond akiwa stejini.

source: GPL.

Friday, July 5, 2013

Angalia Picha na Video ya Diamond na Pasha Katika Uzinduzi wa Msasani Mall







Msasani shopping mall ilifunguliwa jana huku wasanii wakali kama Diamond, Dull, Shetta wakitoa show kali kwa wakazi walioweza kufika kwenye jengo hilo.
Baadhi ya maduka ambayo yapo kwenye hiyo shopping mall ni Slash,lifestyle,shoemart,babyshop,max na mengineo mengi. Jengo lipo karibu na ubalozi wa Marekani.

Tuesday, July 2, 2013

Cheki Picha za Show ya Diamond Pale Mwanza, the Rock City

-->

 

Hizo ni Shangwe za Mini Kabaaang!! ya Tigo ndani ya Mwanza.



Silaha hatari kama kawaida yao wakianza taratibu.....Mpera Mpera tu
hadi kieleweke''



Haya sasa ni mwendo wa nyoka nyoka tu.......
wataelewa sasa hivi au wataelewa baadae...?






Rama Mpauka akimseti roboti wake 
ikafika time ya the prezident kuingia........
Nikistaajabishwa na shangwe na umati wa watu waliokuwa
wamefurika uwanjani pale pale tu nilipotokea uwanjani





....hapo sasa yanii....afe kipa afe beki lakini ushindi lazima....





Kaskazini mwa uwanja wa ccm kirumba umati
 wa watu waliofurika wakishuhudia
 amsha amsha ya wasafi








nimpende nani sasaaa...........???


Aya sasa....Nilikuwaga na nani zamani.....???? Alafu akafanyaje.....??
Leo nataka mtoto wa mwanza kunitibu maradhi nayougua



hakika nilikumbuka kigoma............







siwasikii..etiii??

Thursday, May 9, 2013

Chid Benz Yamkuta- Achezea Ngumi jiwe toka kwa Kala Pina



Baada ya kumtandika makofii Mangwair, Msanii Chid Benz amepata malipo hapa hapa duniani baada ya kuvamia shoo ya Kikosi cha mizinga Maisha Club Juz juz huku akiwa kalewa na kutaka kutoa burudani baada ya kumpokonya Nick Mbish Mic ambaye alikuwa stejin. baada ya tukio hilo Mic ikazimwa na ndipo Kala Pina akapanda Jukwaani na kuamrisha yoyote asiyehusika na shoo ashuke chini, hapo Chid akakaidi amri, kutahamaki boonge la gumi hadi chini, na alipotaka kurudi stejini ali a fight back akazuiwa na kamati ya ulinzi.


Cheki Video hapa chini

-->


Thursday, December 13, 2012

Mama wa Miaka 50 aonekana ana Miaka 30




Sijui tuuite Mkorogo au Virutubisho, maana vimemfanya bi Mtumzma mmoja uso wake na ngozi yake kwa ujumla kuwa kama binti wa miaka 30 hivi ile hali alishagonga miaka 50 na kitu. kwa gharama ndogo tukio hlo limevutia hisia za watu wengi hasa pale lilipoonekana kuwachukiza Madkatari wengi ambao walikuwa wanaweza fanya ya kukaribia na hayo lakini kwa gharama kubwa! Leo ndo ilikuwa siku ya mwisho kwa wanaotaka kuujaribu mzigo huo kwa bure halafu baada ya hapo gharama ndogo zitatumika kununua kama kawa! picha ndo hizo na mzigo ndo huo!
Blogger Widgets