Showing posts with label Bongo Movie. Show all posts
Showing posts with label Bongo Movie. Show all posts

Saturday, August 3, 2013

Gumzo kuhusu Sakata la Mzee Majuto Kuoa kwa Siri Dar!!!!

-->


Chande Abdallah na Haruni Sanchawa
AMINI usiamini, kuna taarifa kwamba gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’ almaarufu mzee Majuto amefunga ndoa ya siri ndani ya Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Tukio hilo limetokea Julai 8, mwaka huu pande za Mbagala Zakhem jijini Dar ambapo mzee Majuto alifunga ndoa na msichana mbichi aitwaye Rehema Omary.
Mzee Majuto aliambatana na wasanii wenzake Suleiman Barafu aliyekuwa mpambe wake na mwingine aliyefahamika kwa jina la utani kama mama Sharon.
Baada ya waandishi wetu kupata taarifa kuhusu tukio hilo, waliwahi kutia timu Mbagala, nyumbani kwa binti huyo.
Baada ya kufika, waandishi wetu walibaini kuwa ni kweli kulikuwa na shamrashamra za ndoa ambayo ilikuwa ikifanyika kwa siri huku watu wakizuiliwa kupiga picha.
Muda mfupi baadaye, gari aina ya Toyota Noah (namba za usajili tunazo) lililowabeba mzee Majuto na wapambe wake liliwasili.
Muoaji akaongozana na wakwe na mashehe kwenda Msikiti wa Aqswa uliopo jirani ambapo ndoa hiyo ilifungwa kisha wakarudi nyumbani ambako cherekochereko ziliendelea.
Paparazi wetu alifanikiwa kujipenyeza na kuonekana kama mmoja wa ndugu na kushuhudia mzee Majuto akikabidhiwa mkewe.
Baada ya robo saa, mzee Majuto na mkewe walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuingia kwenye gari hilo aina ya Noah.
Paparazi wetu alipojaribu ‘kufotoa’ picha kadhaa, alisababisha kuzuka kwa  kizaazaa kwa wanandugu waliomlazimisha kuzifuta picha hizo ambapo alitii.
Baada ya tukio hilo, waandishi wetu walijaribu kuzungumza na mzee Majuto kwa simu lakini kazi haikuwa nyepesi kwani simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
Alilipopigiwa simu mpambe wa bwana harusi, Barafu, alisema hana la kusema na kusisitiza atafutwe mzee Majuto.
Mwandishi wetu alirudi Mbagala kwa mama wa biharusi ambaye alikuwa mkali na kusema kuwa atafutwe mzee Majuto.
Siku hiyohiyo mzee Majuto alipokea simu na kuulizwa kama ni kweli amefunga ndoa na msichana aitwaye Rehema.
Katika hali ya kushangaza, mzee Majuto alicheka sana na kudai kwamba utafiti wake umekakilika. Alipohojiwa ni utafiti gani alisema:
“Nilikuwa nafanya utafiti wa kutaka kuigiza filamu ya ndoa ya siri ndiyo maana nikaenda kule Mbagala lakini sasa nimeamini kwamba hakuna ndoa ya siri,” alisema mzee huyo huku akikwepa kukubali.
Habari zinasema kwamba mzee Majuto anakwepa kukubali kwamba amefunga ndoa kwa kumhofia mkewe wa kwanza ambaye amemuacha jijini Tanga.

Source: GPL

Thursday, August 1, 2013

Kajala Atimkia South Africa, Wadau Wamohofia na Madawa, Mwenyewe Asema ni kupunguza Stress Tu!!!


Imelda Mtema
MWIGIZAJI Bongo, Kajala Masanja ambaye miezi michache iliyopita alichomoka nyuma ya nondo za Segerea kwa dhamana, ametimkia nchini Afrika Kusini kupunguza mawazo.
Kajala Masanja.
Mapema wiki hii, Kajala alitupia picha zake mbalimbali katika mtandao wa Instagram zikimuonyesha akiwa nchini humo na kusindikiza na ujumbe wa maandishi uliosomeka kuwa amekwenda kwa ajili ya kubadilisha hali ya hewa kwani toka akumbwe na matatizo, hajapata mtoko wa kupumzisha akili.
“Nimekuja kubadilisha hali ya hewa  maana nimetoka kwenye matatizo, sijapata kabisa muda mzuri wa kuipumzisha akili yangu hivyo nimeona bora nije huku kupumzika kidogo kisha nitarejea nyumbani,” alisema Kajala.

Source: GPL

Rose Ndauka Ababwa Kona na Njemba, Kisha Wakaingia Hoteleni kufanya Yao.


 
Rose Ndauka  au  Aisha  anaweza  kuwa  ameitia  najisi  funga  yake  baada  ya  kunaswa akiingia  hotel  moja   iliyoko  kinondoni  jijini  Dar  kwa  kile  kilichoelezwa  ni  kwenda  kuivunja  amri  ya  sita  na  mwanamziki wa  bongo  fleva  Nassoro  Ayoub  "Nasry"   au  Tajiri Boy
 
Rose ambaye alisilimu mwaka jana  na  kupewa  jina  la  Aisha  baada  ya  kuchumbiwa  na mwanamziki  mwasisi  wa  kundi  wa  TNG Squad, Malik Bandawe, alifumwa na  kamera  za wakazi wa jirani na  hoteli  hiyo  mwishoni  mwa  wiki  iliyopita.....

Shuhuda  wa  tukio  hilo  amedai  kwamba  majira  ya  mchana  kweupe  gari  aina  ya  Toyota Mark  X lenye  rangi  nyeusi  liliwasili  kwenye  viunga  vya  hoteli  hiyo  na  kusimama  kwa  takribani  dakika  10  kisha  likaondoka  na  kwenda  kupaki  sehemu  nyingine  ambapo  ni  umbali  mfupi  toka  hotelini  hapo...
  Kitendo  hicho  kiliibua  mashaka  miongoni  mwa  watu  hasa  kutokana  na  vioo  vya  gari  hilo  kuwa  tinted  hivyo  kutowaonesha  waliokuwemo  ndani...

"Walipoondoka  na  kupaki  palipojificha  tuliamua  kuwasogelea  ili  tujue  ni  akina  nani

"Baada  ya  muda, kioo  cha  dereva  kilishushwa kidogo, tukamuona  dogo  anayefanana  na Diamond  akiwa  anampapasa  demu  aliyekuwa  pembeni  yake...

"Tulipoona  hivyo, tulidhana  mnyamwezi  ameamua  kumaliza  mambo  yake  ndani  ya  gari, hivyo  tukaziweka  simu  zetu  standby  kwa  ajili  ya  kushuhudia" alisema shuhuda  huyo

Baada  ya  muda, mlango  wa  kulia  ulifunguliwa  kisha  wakamuona  dogo  aliyetambuliwa  kwa  jina  la  Nasry

"Kumbe  hakuwa  Diamond,alikuwa  ni  dogo  Nasry.Tulipotupa  jicho  ndani, tulihamaki  kumuona  Rose  Ndauka  akibadili  nguo  na  kujitanda  baibui. 

"Nadhani  alifanya  hivyo  ili  watu  wasimjue  pindi  atakaposhuka  kwenye  gari  maana  aliposhuka  tu, waliongozana  na  dogo  Nasry  kwa  mwendo  wa  kasi  hadi  ndani...

"Toka  walipoingia  ndani  hadi  walipotoka  iliwachukua  kama  masaa  matatu  hivi.Wakati  wa  kutoka, Nasry  alilifuata  gari  hadi  mlangoni  na  kisha  Rose  akaingia  na  kutokomea"...Kilimalizia  kusimulia  chanzo  hicho

Source: GPL (KIU)

Saturday, July 27, 2013

Angalia Jinsi Bongo Movie Wanavyopondwa na Kutathminiwa hapa



UTAJUAJE NI BONGO MOVIE? 

1.Jini akifika barabarani
anaangalia
pande zote ndo avuke barabara. 

2. Matajiri majumba yao yana askari
badala ya electric
fence &
gates.
3.Trailer inachukua
dakika 40.
4.Part2 ya movie ukiiona
mwanzo unajua part1
ilikuwaje.
5.Madem wanaamka wanamake ups
usoni na hereni kabisa.
6.Wakifika hotelini imezoeleka ni juice
inaagizwa au wine
isiyofunguliwa.
7.Nusu saa mtu anatembea,anafanya
mazoezi,anakimbizwa au ananunua vitu.
8.Wimbo wa malavidavi
unaimba
mpaka unaisha.
9.Mtu yupo
village,life gumu ana wave kichwani.
10.Wote wanaouwawa kwa risasi
hupigwa kifuani au
tumboni sio kichwani.
11.Jambazi
lazima awe anavaa miwani nyeusi,koti
kubwa na mvuta sigara mwenye sauti
nene na sura ya kutisha
12Tajiri anakuja kumpenda maskini.
13. Jina La Movie La Kingereza, Ndani
Mazungumzo Ni Kwa Kiswahili.
14.Editor Roy Kijusi, Camera man
Inosenti Kijusi, graphic designer Roy
Kijusi, Location manager Happy Kijusi,
Mavazi Suzy Kijusi.
15.Movie inapart1 na part2,lakn
ukiangalia unagundua ni disc.1 na disc.2
16.movie inaitwa life is harder (mfano)
afu kwenye kava watu wameweka
mapozi ya mamodo na warembo."


Hii nimeikuta face book, huku ikipata Comment zaidi ya 30, Likes ndo Usiseme, Vipi ndugu Msomaji wangu, unalionaje hili?

Friday, July 26, 2013

Lulu Ajipanga Kurudi Darasani Tena


STAA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekazia nia yake ya kutaka kurudi shule siku chache zijazo.
Lulu aliandika hayo juzikati alipokuwa akichati na mashabiki wake kupitia ukurasa wa facebook ambapo alikuwa akiulizwa maswali na kuyajibu live kupitia Runinga ya East Africa.
Mmoja wa mashabiki wake alimuuliza Lulu kuhusu mipango yake ya kurudi shuleni ambapo alimjibu kuwa yupo katika mipango  hiyo hivyo hivi karibuni atarudi darasani.
“Am on process..soon mpenzi nitarudi darasani,” aliandika Lulu ambaye awali alidaiwa kukatisha masomo yake ya sekondari.
Source: GPL

"BIFU" la Uwoya kuibiwa Mume na Lucy Komba ni Kutokana na Movie hii" Kwanini Nisimuoe" Angalia Picha Humu.

-->

Na Imelda Mtema
LILE sakata la staa wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya kutuhumu kumshika ugoni staa mwenzake aliyemtoa kwenye gemu, Lucy Francis Komba limeingia sura nyingine kuafutia picha za filamu inayodaiwa kuchezwa na wawili hao kunaswa na Ijumaa, twende hatua kwa hatua.
Katika baadhi ya matoleo ya Magazeti ya Global Publishers zilichapishwa habari za mastaa hao kuzua bifu zito kufuatia Lucy kumchukua mwanasoka wa Rwanda ambaye ni mume wa ndoa wa Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ na kucheza naye filamu jambo ambalo Uwoya alilipinga.
KWA NINI UWOYA ALIPINGA?
Uwoya alipinga mumewe kushiriki filamu hiyo kwa sababu aliambiwa washiriki ni wawili tu, mumewe Ndikumana na Lucy. Filamu inaitwa Kwa nini Nisimuoe?
Kwa mujibu wa Uwoya, hajawahi kuona filamu ya kawaida inachezwa na watu wawili tu, akasema Lucy alitumia nafasi hiyo kuwa na mumewe kimapenzi.
Hata hivyo, Uwoya alisema akiviona vipande vya picha za filamu hiyo atajua ukweli.
Wiki iliyopita aliviona vipande hivyo na kuweka msimamo wake kwamba hakuna filamu ni mapenzi tu.
IJUMAA LAFUKUNYUA, LAIBUKA NA PICHA
Kama kawaida ya Magazeti ya Global Publishers, liwe Ijumaa, Uwazi, Ijumaa Wikienda, Amani, Championi au Risasi ni kuchimba mambo kwa undani na kuupata ukweli wa jambo, hivyo timu ya wanahabari wetu ilizama mitaani na kuzisaka picha za filamu hiyo.
Julai 23, 2013, Ijumaa lilifanikiwa kuzipata picha hizo ambazo moja baada ya nyingine zinawaonesha Lucy na Ndikumana wakiwa katika mapozi mbalimbali ndani ya filamu (angalia picha).
MWANZO, MWISHO NI WAWILI TU!
Katika picha hizo ambazo ziko mikononi mwa dawati la Ijumaa, wasanii walioonekana ni Lucy na Ndikumana tu hivyo kushibisha yale maswali ya Uwoya kuwa ni kwa nini filamu nzima ichezwe na watu wawili tu?
HADITHI YA FILAMU YADAIWA NI KISA CHA KWELI CHA UWOYA NA NDIKU
Habari za hivi karibuni zilisema kuwa,   cha ajabu, kisa kinachosimuliwa katika filamu hiyo ni cha kweli.
Ilidaiwa kuwa kisa hicho kilimpata Ndiku baada ya kukutana na Uwoya kwa mara ya kwanza kabla ya kufunga ndoa.
Madai hayo yanaongeza chachu katika moyo wa Uwoya na kuzidi kuamini kuna kitu kinaendelea kati ya mumewe na Lucy.
UWOYA AKATISHA ZIARA SWAZILAND
Uwoya alipotafutwa na Ijumaa juzi ili kumsikia msimamo wake kuhusu hali tete katika ndoa yake baada ya hisia zake kuwa anaibiwa mumewe na Lucy, alisema atapasua jipu atakapotua Bongo akitokea nchini Swaziland ambako alikwenda kwa ziara binafsi.
Alisema kuwa amelazimika kukatisha ziara na kurudi Tanzania kwa vile suala la Lucy na mumewe linamnyima raha kuendelea kuwepo ugenini.
“Narudi Bongo Jumatano (juzi). Unajua hili suala limeninyima raha kabisa. Siwezi kuendelea kuwepo huku ugenini. Nikifika nitatoa la moyoni,” alisema Uwoya.
 
LUCY AZUNGUMZA KUTOKEA DENMARK
Wakati Uwoya akizungumza kutokea jijini Mbabane, Swaziland, Lucy yeye alitoa sauti yake akiwa nchini Denmark kwenye Jiji la Copenhagen.
Alipoulizwa kuhusu tambo za Uwoya baada ya yeye kucheza filamu na mumewe Ndikumana, alijibu:
“Mimi sina cha kusema, yeye anajua mimi ni nani katika filamu. Mumewe kaonesha mapenzi ye kucheza filamu yangu, sasa anaposema ningemtaarifu yeye kama nacheza filamu na mumewe ili iweje? Kwa nini asimlaumu mume wake ambaye ndiye alipaswa kumtaarifu?” alisema Lucy.
Lucy aliongeza: Kama Ndiku angekuwa mtoto chini ya miaka kumi na nane nataka kucheza naye filamu hapo kweli, ningepaswa kumtaarifu Uwoya kama mama mtu, lakini mume, si sahihi kunilaumu.
MADAI YA HADITHI YA FILAMU KUWA KISA CHA KWELI
Kuhusu madai kwamba hadithi ya kwenye filamu hiyo ni kisa cha kweli kati ya Uwoya na Ndiku, Lucy alijibu:
“Teh! Teh! Si kweli bwana. Kama Uwoya ndiyo kasema hivyo basi ana kisa kinachofanana na cha filamu yangu. Mimi filamu ni yangu na hadithi ni yangu.”
WAONGOZA FILAMU BONGO WANASEMAJE KUHUSU WATU WAWILI TU?
Ili kujifunza juu ya wasanii wawili kucheza filamu nzima, Ijumaa liliwatafuta baadhi ya waongoza filamu Bongo.
Jumanne Kihangala ‘Mr Chuz’: Kusema kweli ni vigumu sana. Labda kama zile filamu za porini, mtu anakimbizwa na wanyama (documentary).
“Lakini kucheza filamu za mjini halafu wawili tu, mnagombana wenyewe mnapatana wenyewe ni kazi sana,” alisema Chuz.
Jacob Steven ‘JB’: Du! Labda kama utakuwa umekusudia kupunguza bajeti, lakini pia haitakuwa filamu nzuri, wawili tu?! Kwanza ni filamu gani hiyo ya watu wawili tu?
Ijumaa lilimkatia simu.
Mahsin Awadh ‘Dk Cheni’: Mh! Zipo kama mtu mwenyewe atakuwa ameamua, lakini sidhani kama sokoni itakubalika. Ni nani huyo kwani?
Ijumaa likamkatia simu.
Wazoefu wengi wa filamu walisema documentary ndizo zinaweza kuwa na watu wawili lakini si filamu.


source: GPL

Kumekucha "BONGO MOVIE", Nisha naye Akimbia na Samani za Ndani za Rafiki yake.

-->



Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ametupiwa tuhuma nzito za utapeli wa samani za ndani baada ya kupewa hifadhi na shoga’ke aitwaye Amina Mrisho anayeishi Ilala jijini Dar, Ijumaa limetonywa.
Salma Jabu ‘Nisha’.
Kwa mujibu wa Amina, tukio hilo limetokea mwaka 2011 baada ya msanii huyo kukosa fedha za kulipia kodi na kuomba hifadhi kwake.
“Alitakiwa kuondoka katika nyumba aliyopanga akaomba hifadhi kwangu nikamsitiri kwa kuwa alikuwa ni rafiki yangu, akahamia na vitu vyake vyote vya ndani,” Amina alianza kushusha madai hayo na kuendelea:
“Baada ya muda alitangaza kuziuza samani zake kwa shilingi 750, 000 ili apate fedha za kuendeshea maisha, nikaahidi kuzinunua na nikamtangulizia shilingi 500,000 kama malipo ya sofa, meza ya runinga, dressing table na meza ya jikoni.”
Hata hivyo, msichana huyo alisema kwamba kabla mwezi haujaisha, Nisha alibadilika na kutaka fedha zilizobaki kwa nguvu huku akimpa vitisho kwa kumwambia kuwa atamkomesha kwa kuwa risiti zote za samani hizo alikuwa nazo.
Amina Mrisho.
Inazidi kudaiwa kwamba Nisha alienda kutoa taarifa polisi na kudai kwamba Amina alimwibia samani zake.
“Pamoja na kujieleza polisi muafaka ulifikiwa kwamba Nisha achukue samani zake na miye sikuambulia chochote,” alisema Amina.
Baada ya malalamiko hayo, paparazi wetu alimtafuta Nisha ili kupata ukweli, naye alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza huyo Amina simfahamu na katika maisha yangu sijawahi kukaa kwa mtu kwa sababu ya kuishiwa hela ya kulipia kodi. Mama yangu ana nyumba kubwa tu, ningewezaje kuiacha na kwenda kukaa kwa mtu baki?”
“Ukishafanikiwa lazima kuna watu wataibuka na kusema maneno mabaya ili wakushushe kama huyu miye wala simfahamu ni muongo tu.”


SOURCE: GPL

Wednesday, July 24, 2013

Aibuu "SHILOLE" Aiba Simu za "Daimond", Alipewa na Ndugu wa Daimond South Africa, Hajampa Mwenyewe Hadi Leo!!!!



Stori:Shakoor Jongo na Musa Mateja
STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.
Mfano wa aina ya simu anazo daiwa kuiba Shilole
Msanii huyo alikumbwa na kasheshe hilo Julai 19, 2013 nyumbani kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sinza Mori, Dar.
Siku hiyo Diamond alikuwa akifuturisha na aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo mastaa lakini nusura futuru iingie doa kufuatia zogo hilo.
ISHU ILIKUWAJE?
Ndugu wa Diamond aitwaye Majaliwa Majuto ‘Q Boy’ alidai ndiye mwenye simu hizo. Alisema miezi kadhaa iliyopita, Shilole alikwenda nchini humo kufanya shoo ya muziki. Wakati wa kuondoka alimpa simu tatu, Ipad, Samsung Galaxy na Blackberry ili akifika Bongo ampe Diamond lakini msanii huyo hakufanya hivyo.
“Alikuja Sauzi kufanya shoo, wakati wa kuondoka nilimpa simu tatu amletee Diamond lakini nashangaa hakufanya hivyo na mimi tangu nirudi Bongo simpati, kila nikimpigia simu hapokei, leo ndiyo tumekutana hapa kwa Diamond,” alilalama Q Boy.
DIAMOND ALIAMBIWA SIMU ANAZO SHILOLE
Alisema awali akiwa nchini humo baada ya kumkabidhi mali hizo, alimpigia simu Diamond na kumtaarifu kuwa ‘mzigo’ anao Shilole, akashangaa staa huyo kujibu kwamba hajazipata wala hajamwona Shilole.

SHILOLE AJITETEA
Katikati ya mzozo huo, Shilole alijitetea kwa kusema: Mi namdai rafiki yake fedha yangu ya shoo iliyobaki, kama shilingi laki nane hivi ndiyo maana nikaamua kuzizuia simu za huyu (Q Boy) hadi nimaliziwe pesa yangu.
Hata hivyo, katika sakata hilo ilielezwa kuwa Shilole na Q Boy hawakuwa na makubaliano yoyote kuhusu shoo hiyo na simu hizo hivyo madai ya mwigizaji huyo ni ‘usanii’ tu.

MAMA DIAMOND AINGILIA KATI KUOKOA
Zogo hilo lilipopamba moto na kuashiria kuvurugika kwa amani, mama mzazi wa Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ aliamua kuingilia kati na kuagiza suala la kudaiana simu lifanyike kesho yake (Jumamosi) kwa vile siku hiyo haikuwa muafaka.
“Jamani! Jamani! We nani, Shilole na we Majaliwa, naomba kwa leo muepusheni shetani kwani hapa si mahali pake, ila kesho tutaitana na kumaliza suala hili, mimi mwenyewe nitalisimamia,” alisema bi mkubwa huyo na kumaliza henyahenya iliyoibuka.

JUMAMOSI YAFIKA, KIKAO VIPI?
Jumamosi, mapaparazi wetu walifuatilia ishu hiyo nyumbani kwa akina Diamond na kuulizia ili kujua kama kikao cha usuluhishi kilifanyika kama mama Nasibu alivyoagiza.
“Mh! Sijaona kikao chochote, kwanza Shilole mwenyewe akipigiwa simu hapokei,” alisema ndugu mmoja wa Diamond huku akiomba hifadhi ya jina lake.

MSIKIE DIAMOND
Juzi, Diamond alipopigiwa simu na kuulizwa kama anaijua ishu ya simu, alikubali.
Staa huyo alisema anashindwa kuingilia kati sakata hilo kwa sababu wahusika wote ni watu wake wa karibu kikazi.
“Yeah! Ishu ni kweli ipo, lakini mimi nilijiweka kando mapema, nikamwambia dogo (Q Boy) afuatilie mwenyewe baada ya kuona Shilole haeleweki.
“Unajua Shilole ni mwanamuziki mwenzangu, dogo yupo ndani ya Kampuni ya Wasafi Entertainment (ya Diamond), sasa kukomaa na ishu za simu tu nahisi itanishushia hadhi, napiga shoo za hela nyingi halafu leo nakomaa kwa hela ndogo, inakuwa siyo,” alisema Diamond.

SHILOLE TENA
Baada ya kuzungumza na Diamond, Shilole alipigiwa simu na kuomba kufafanua kwa undani ishu hiyo ambapo katika hali isiyotarajiwa, alimlalamikia paparazi wetu akidai anapendelea katika sakata hilo.
“Nyiye mnamtetea tu yule dogo, mimi sina tatizo, kama rafiki yake (aliyemuitia shoo Afrika Kusini) akinilipa hela yangu nawapa simu zao,” alisema Shilole.
Msanii huyo alikwenda mbele zaidi kwa kumwambia paparazi kuwa atatia timu kwenye Ofisi za Global Publishers ili kuzungumzia suala hilo na viongozi.
Baadaye Shilole alifika ofisini kwetu na kufafanua juu ya sakata hilo ambapo alirudia kukiri kuzuia simu hizo akidai kwamba anamdai Q Boy hivyo mpaka atakapomlipa ndiyo atampa simu zake.

Q BOY NAYE TENA
Kwa upande wake, Q Boy alipozungumza na paparazi wetu siku hiyo alisema amekusudia kwenda kufungua kesi kituoni ili apewe msaada zaidi wa kisheria kwa vile simu hizo zinamuuma hasa ukizingatia kuwa yeye siye aliyempeleka Shilole Afrika Kusini kufanya shoo.
“Mimi leo (Jumatatu) nimebanwa sana, kuna sehemu nakwenda na Diamond, nadhani nitamaliza jioni. Lakini kesho (Jumanne) nitaamkia polisi kufungua kesi nione watanisaidiaje?” alisema Q Boy.

POLISI AGUSIA ISHU
Risasi Mchanganyiko lilizungumza na askari mmoja kutoka Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kummegea mtiririko wote, kisha kumuuliza kama kuna kesi ambapo alijibu:
“Japokuwa mimi si msemaji wa jeshi (la polisi), lakini ishu kama hiyo shitaka lake lipo, ni wizi wa kuaminiwa. Unajua wengi wanadhani kuibiwa lazima mtu uwe hujui, lakini mtu akifanya kama hivyo alivyofanya huyo msanii nani sijui (Shilole), kama ni kweli, kosa linakuwa wizi wa kuaminiwa endapo atafikishwa polisi.”

DIAMOND, Q BOY WALIFANYA MCHEZO?
Hata hivyo, baadhi ya watu walioshuhudia sakata hilo walikuwa na maswali kibao yaliyokosa majibu.
Swali la kwanza: Shilole alikwenda kufuturu kwa mwaliko wa Diamond na alijua staa huyo na Q Boy ni wamoja na simu alizopewa ilikuwa amletee msanii huyo, kwa nini alikwenda huku akijua ana msala?
Swali la pili: Kama Shilole alikwenda akijua Q Boy hayupo Bongo, je! Si kwamba ulikuwa mpango wa wawili hao kumwita ili wampe kibano ateme simu zao?
Swali la tatu: Je, ni kweli Shilole alizuia simu ili amaliziwe deni lake kwa mtu aliyemuitia shoo Afrika Kusini au shetani alimwingia baada ya kutua Bongo na kuamua kuzitumia hasa ikizingatiwa kuwa siku hizi mambo ya Instagram ndiyo habari ya mjini?

SOURCE: GPL

Uwoya Amtuhumu Lucy Komba Kumchukulia Mumewe, Soma Kisa Kizima Hapa!!!


Stori:Imelda Mtema
NYOTA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krrish’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake, Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu.
Lucy Komba anayedaiwa kushikwa ugoni na Irene Uwoya.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea nchini Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na Kataut walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake.
Irene Uwoya anayedai kumshika ugoni Lucy.
“Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka kusema  ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.
Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Bongo akiigiza filamu na Lucy.
“Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa karibu angenieleza vizuri kwa sababu hata yeye angeweza kunipigia simu na kunifahamisha ushiriki wa mume wangu kwenye filamu hiyo kwa kuwa namba zangu anazo, ilikuwaje hakufanya hivyo?” alihoji.
Kuonesha kwamba amechukizwa na kitendo hicho, Uwoya alisema kwamba akitua Bongo atamtafuta Lucy ili aweze kumshughulikia vizuri na ikiwezekana amuoneshe hiyo filamu waliyoigiza watu wawili tu.
“Nitatua Bongo siku si nyingi na cha kwanza ni kumtafuta Lucy, anieleze vizuri kuhusu filamu hiyo waliyocheza na mume wangu,” alisema Uwoya.
Filamu hiyo ambayo imekuwa maumivu makubwa kwa Uwoya, imechezwa na Lucy na Ndikumana tu mwanzo hadi mwisho na imepewa jina la Kwa Nini Nisikuoe.


SOURCE: GPL

Saturday, July 20, 2013

"WANAUME WALIO MSAIDIA SAJUKI WAMENIGEUKIA NA KUNITAKA KIMAPENZI"-WASTARA JUMA



Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa mgonjwawanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi. 
  
Akizungumza kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.

Bishosti huyo alisema kuwa tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa sapoti kipindi hicho, bado wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya nchi ambao wanatuma maombi kwake lakini anawaona wote ni matapeli na wanamtamani tu hivyo hayupo tayari kuingia kwenye uhusiano wa aina hiyo.

“Kweli ninaumia sana kwa sababu ninakaa na kujiuliza hawa wanaume walikuwa wanasubiri mume wangu afariki dunia ndiyo wanitongoze?
 

“Kusema kweli inanishangaza, hata watu ambao sikuwadhania kabisa eti nao wananitaka, watu wajue kwa sasa sipo tayari kuwa na mwanaume.
 

“Sitaki kukurupuka kwa sababu naweza nikaingia kwenye shimo la taka kwani jamii itanikimbia kutokana na kunuka, natamani kumpata mwanaume anayefanana na mume wangu kitabia.

“Uvumilivu wangu na uzuri ulitokana na kutunzwa siyo aje mtu anayetaka nikavumilie shida, hilo sitaki litokee, namuomba Mungu sana,” alisema Wastara.


Source:- Mpekuzi

YALIYOJIRI KWENYE HARUSI YA MSANII WA BONGO MOVIE LEO HII TAZAMA PICHA HAPA:




 
  Natasha akiwa  anawekwa gauni vizuri na mpambaji wa saluni ya Partners.
 
  Natasha akijiangalia kama yuko sawa.
  …Akitengenezwa vizuri na mtaalamu wa nywele kwenye saluni hiyo.
 
  …Akiendelea kupambwa vizuri.
 
  …Akiwa na mpambe wake Neema wakiwekwa vizuri.
 
  …Akiwa amepozi katika saluni hiyo.
 
  … Akiwa katika picha ya pozi na mpambe wake.
Muigizaji mkongwe wa tansia ya filamu hapa Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ leo hii amefunga ndoa  kwenye Kanisa la Mtakatifu  Joseph lilipo Posta jijini Dar na mume wake Alex Humbila .
Kabla ya kutinga kanisa kamera yetu ilimnasa Natasha katika suluni moja maarufu kwa kupamba mastaa mbalimbali hapa Bongo , Partners Wedding iliyopo Sinza  Mori akiwa anaandaliwa kwaajili ya kwenda kanisani. Kufunga ndoa
 

Source: Boss Ngasa.

Friday, July 19, 2013

Wema Sepetu Hatiani, Heunda akaenda Jela Safari Hii.






Na Waandishi Wetu

KUNA kila dalili kwamba mrembo anayetamba kwenye filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au Madam jela inamwita na anatakiwa kufanya maombi ili kukwepa kifungo maishani mwake.

Hali hiyo inafuatia staa huyo kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena Jumatano iliyopita, pale alipopanda katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar kwa kosa la kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni meneja wa hoteli moja iliyopo Kawe Beach jijini Dar, Godluck Kayumbu.…
Na Waandishi Wetu
KUNA kila dalili kwamba mrembo anayetamba kwenye filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au Madam jela inamwita na anatakiwa kufanya maombi ili kukwepa kifungo maishani mwake.
Hali hiyo inafuatia staa huyo kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena Jumatano iliyopita, pale alipopanda katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar kwa kosa la kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni meneja wa hoteli moja iliyopo Kawe Beach jijini Dar, Godluck Kayumbu.
Kabla ya  kupandishwa  kwa ‘pilato’,  staa huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame alikuwa akisakwa na askari kwa siku kadhaa na kufanikiwa kuwapiga chenga za hapa na pale.

ANASWA AKIFUTURU
Hata hivyo, mbio zake ziliishia ukingoni Julai 16, mwaka huu, alipokamatwa saa mbili usiku akiwa anafuturu na wageni wake nyumbani kwake, Kijitonyama Dar.
MTITI KIDOGO
Askari saba walifika nyumbani kwake wakiwa ndani ya Land Rover ‘difenda’ kwa ajili ya kumkamata, hata hivyo walipata upinzani kidogo kutoka kwa mlinzi wa staa huyo ambaye alikuwa akizuia bosi wake asikamatwe ambapo ilibidi askari hao wakaze msuli na kutuliza mtiti uliokuwa ukitaka kutokea.
WEMA AGEUKA MBOGO, ALALA SELO
Baada askari kumfikia staa huyo, walimtaka kwenda naye kituo cha polisi kwa kutumia difenda walilofika nalo ambapo Wema alipinga na kugeuka mbogo kwa kudai kwamba hawezi kupanda difenda kutokana na hadhi yake.



Pamoja na askari kutaka kumpandisha kwa nguvu, staa huyo alipinga na ikakubaliwa apande gari lake aina ya Audi Q7 huku akiwa chini ya ulinzi wa askari.
Safari ikaishia Kituo cha Polisi cha Kawe ambako staa huyo aliandikisha maelezo na baada ya zoezi hilo akatupwa selo.

WEMA HAUOZI
Kama lilivyo jina lake, wema hauozi, staa huyo alipata dhamana saa 5 za usiku baada ya kudhaminiwa na msanii  mwenzake wa filamu, Kajala Masanja.
Kajala aliwahi kutolewa katika mdomo wa jela na Wema siku za nyuma baada ya kukutwa na hatia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar alipotakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 13 au kwenda jela, Wema alimlipia kiasi hicho cha fedha.
WAPAMBE FULL SHANGWE
Wapambe wa Wema waliokuwa wamejazana nje ya kituo hicho cha polisi, walilipuka kwa shangwe baada ya bosi wao kuchomolewa kutoka selo. Staa huyo aliondoka na gari lake lililokuwa likiendeshwa na meneja wa kampuni yake aitwaye Petit Man.

ATEMBEZWA KWA MIGUU
Julai 17, asubuhi Wema alirudi kituoni hapo na kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kupelekwa mahakamani kusomewa mashitaka yake.
Katika hatua ya kushangaza, staa huyo alitembezwa kwa miguu umbali wa mita 200 kutoka kituo cha polisi hadi Mahakama ya Mwanzo ya Kawe.
APANDISHWA KIZIMBANI
Wema alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake na Mh. Hakimu, Bernice Ikanda na kudaiwa kufanya vurugu, kushambulia kwa kumpiga makofi na kumtukana Kayumbu.
Mbele ya hakimu, Wema alikana mashitaka na hakimu aliiahirisha kesi hiyo mpaka Julai 31, mwaka huu.

IKO SIKU WEMA ATAFUNGWA GEREZANI
Kumbukumbu kutoka kwenye makabrasha yetu zinaonesha kuwa, mrembo huyo ni mtu wa majanga, mara kwa mara amekuwa akifikishwa polisi na mahakamani kutokana na ugomvi.
ALIVUNJA KIOO CHA GARI LA KANUMBA
Mwaka 2009, Wema alidakwa na Polisi Kituo cha Magomeni na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya Kinondoni, Dar kwa Hakimu Emilius Mchalu kwa kosa la kuvunja kioo cha gari la aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Marehemu Steven Kanumba chenye thamani ya shilingi milioni moja. Hata hivyo, Kanumba aliifuta kesi hiyo.

ALIMTISHIA MAISHA BOB JUNIOR
Kama vile haitoshi, mwaka 2011, Wema huyohuyo alikamatwa na Polisi wa Oysterbay jijini Dar na kufikishwa Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kumtusi na kumtishia maisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rahem Nanji ‘Bob Junior’.
Katika kesi hiyo, Hakimu Mariam Masamalo alimtia hatiani Wema kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya shilingi 40,000 ambapo alilipa fedha hizo.
ALIMTUSI REHEMA FABIAN
Aidha, mara baada ya Wema kuachiwa huru mahakamani hapo alikamatwa tena na polisi kwa kile kilichodaiwa kumtusi Miss Kiswahili 2008, Rehema Fabian. Wema alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar kwa maelezo zaidi.

ALIMTUKANA MSANII
Aidha, Wema amewahi kulala kituo cha Polisi Oysterbay, Dar akiwa na mashoga zake, Kajala na Dida kwa madai ya kumshambulia mwigizaji mmoja wa Bongo, kwenye pati iliyofanyika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar. Kesi hiyo iliisha kwa mazungumzo nje ya polisi. 

Imeandikwa na Musa Mateja, Mwaija Salum, Makongoro Oging’ na Shakoor Jongo.
SOURCE: GPL.
Blogger Widgets