Showing posts with label Ujana. Show all posts
Showing posts with label Ujana. Show all posts

Tuesday, January 21, 2014

VIDEO MPYA YA JUX YAPIGWA STOP KIANA KURUSHWA HEWANI KUTOKANA NA KUSHEHENI MAMBO YA KIKUBWA


Ni mara chache kusikia video flani ya bongofleva haichezwi kwenye vituo vya TV kwa sababu ya wamiliki wa vituo hivyo kuona haina maadili hivyo haiwezi kuruhusiwa kuonyeshwa kwa mamilioni ya Watanzania.

Video ya Jux toka mwaka 2013 mwishonimwishoni stori zilikua zinazunguka kwamba hii video imefungiwa kwenye vituo vya TV za bongo sababu picha zinazoonekana ndani yake zimezidisha kuvuka mipaka ya kimaadili. 

Kwa sababu taarifa hizi ‘inadaiwa’ hazikutokea BASATA, wengi walisubiria Jux mwenyewe akirudi Tanzania atasema nini kuhusu hii ishu manake labda ni vituo vya TV vyenyewe ndio vimeamua kuisimamisha bila agilo la BASATA hivyo kama ni TV zenyewe basi vingekua vimemwambia. 

Anachosema ni hiki >>> ‘Mimi nilikua China ndio B12 akaniambia video yako imefungiwa, nilivyorudi Tanzania BASATA tulipoulizia wakasema hawana hizo taarifa na ni lazima wapitiwe kwanza wao kwenye ishu kama hii… na lazima wakichukua hatua wanatoa taarifa kwa muhusika, wakasema kuna vitu viwili inawezekana kuna michezo imechezwa’ 

Swali : Toka umerudi bongo umeshawahi kuiona hii video ikichezwa kwenye TV?
 Jux : ‘hapana ila kuna watu waliniambia wameshawahi kuiona EATV, pia mimi sio mtazamaji wa TV sana’
Angalia Video hapo chini:-


Monday, January 20, 2014

DENTI WA UDSM MWAKA WA PILI ADATA NA PENZ LA LECTURER WAKE, YUPO NJIA PANDA


Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24 sasa. Ninasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka wa pili.

Tatizo langu ni kwamba, kadri siku zinavyozidi kwenda nahisi kumpenda mmoja kati ya maprofesa wangu. Lakini hadi sasa ninachoona ni kwamba bado hajajua hisia zangu nifanyeje?

Monday, January 6, 2014

MAMBO YA UJANA HAYO, CHUP! LIMETOBOKA NA MLEGEZO JUU.


PICHA HII IMENASWA MOJA YA VIJIWE VYA VIJANA MANISPAA YA MOROGORO KAMA INAVYOONEKA, KIJANA AKIWA AMESHUSHA SURUALI ILI NGUO YA NDANI IWEZE KUONEKANA
VYEMA NA KIURAHISI LAKINI CHA KUSTAJABISHA NGUO HIYO IMELIWA NA MENDE NA KUACHA PENGO LILILOONYESHA SEHEMU YA MWILI KATIKA KALIO LA UPANDE WA KULIA, HAIKUWA KAZI RAHISI KUULIZA SWALI KWA KIJANA HUYO KWANINI AMEVAA NGUO YA NDANI ILIYOTOBOKA ?, BILA SHAKA SWALI HILO ALIPASWA KUULIZWA NA MZAZI WAKE. 

                                                                                                                      PHOTO/MTANDA BLOG

Sunday, August 4, 2013

Wanawake wenye jinsia Mbili, Huoa na Kuolewa.



Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa michezo ya ajabu kufanywa na Wasichana, pia wavulana hususan katika suala zima la kujibadilisha jinsia kutoka aliyokupa Mola wako na kujipachika Unayoihusudu wewe kwa matamanio yako.

Pia hiyo ni hali halisi ya mambo yalivyo hivi sasa kwani kuna wasichana wamegeuka wanaume na wengine wanabakisha zote mbili, huu ni mwisho wa dunia.

Mwalimu wa Miaka 22 ajihusisha kimapenzi na Mvulana wa miaka 15.

Kalee Warnick


Mwalimu wa Somo la Kiingeeza katika Shule ya Wall huko New Jersey anakabiliwa na shitaka la matumizi mabaya ya madaraka na kumlazimisha mapenzi mwanafunzi wake wa miaka 15.

Kalee Warnick,22, alikamatwa Jumanne iliyopita kwa kosa hilo la kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mtoto, kesi yake imepangwa kusikilizwa Alhamisi Ijayo hata hivyo wakili wa mwalimu huyo Amesema ya kwamba mteja wake amepanga kukana mashtaka yanayomkabili.

Shule hiyo ambayo mwalimu huyo pia alisoma na kumaliza mwaka 2008

Saturday, August 3, 2013

Eniola Auliza Mashabiki kuhusu kuwa Dada yake Rick Ross!!


Yule mwanamke mnene na anayekula kushinda wanawake wa Nigeria, Eniola Badmus ameandika katika page yake ya Instagram ikiwauliza wadau ya kwamba vipi kila mtu anamfananisha na Mwanamuziki kutoka Marekani, Rapper Rick Ross, yawezekana akawa dadake? Angalia picha mwenyewe kisha toa tathmini yako.

Friday, August 2, 2013

Majanga ONA Majanga!!!! Mpaka Kieleweke Leo!!


Kama kawaida, Cheka Upate Afya, leo nakuletea Picha niliyoipata katika mtandao wa kijamii huku ikiwa Commented ya Kwamba Mpare Utamjua Tu!!!! Walionaje hili?

Thursday, August 1, 2013

Ex-Lover wa Pokello, Mshiriki wa BBA Amjibu kwa Nyimbo.


Mwanamuziki, Rapper Stunner ameachia Single yake mpya inayokwenda kwa jina la "Bye Bye" ambayo kiundani inamjibu Aliyekuwa Mpenzi wake, Mwakilishi katika jumba la BBA The Chase, Pokello ambaye uhusiano wao ulivunjika baada ya mwanamke huyo kuanzisha mahusiano na Mshiriki Mwenzie Elikem wa Mjengoni hapo

Pokello alimkacha Stunner live katika mahojiano na kiyuo kimoja cha Television cha nchi hiyo, wengi wamesema mbinu ya mwanadada huyo kujiweka karibu na Stunner ilikuwa ni kujijengea Umaarufu tu.

Justin Bieber Awatemea Mate Mashabiki walikuwa wamejazana kumshangaa!!!


Kweli majuu hapaishiwi vituko, Mkali wa Pop Kijana mwenye asili ya Canada, Justin Bieber amefanya Kufuru ya aina yake baada ya kuwatemea mate mamia ya mashabiki waliokuwa wamejazana chini katika ghoroma moja alipokuwa amekwenda kwa rafiki zake Alhamis ya Tarehe 25 July. Angalia Picha zaidi Chini..

Monday, July 29, 2013

Angalia Alichokiandika Selly katika Ukurasa wa Twitter Baada ya Nando Kutimuliwa BBA The Chase.

-->   Mshiriki kutoka Ghana aliyewahi kukashifiwa ya kwamba amemwambukiza magonjwa ya zinaa mshiriki wa Tanzania, Selly ameandika Kauli ya Kufurahia kutolewa kwa Nando katika Jumba hilo la BBA.

Angalia Mwenyewe:-


@therealsellygh
My God has fought my battle! All the stigmatization..hmm!! Fanx 2 all my friends and fans! Fanks to Africa!!

 

Saturday, July 27, 2013

Justin Bieber Awatemea Mate Mashabiki walikuwa wamejazana kumshangaa!!!


Kweli majuu hapaishiwi vituko, Mkali wa Pop Kijana mwenye asili ya Canada, Justin Bieber amefanya Kufuru ya aina yake baada ya kuwatemea mate mamia ya mashabiki waliokuwa wamejazana chini katika ghoroma moja alipokuwa amekwenda kwa rafiki zake Alhamis ya Tarehe 25 July. Angalia Picha zaidi Chini..

Maskini, Msichana wa Chuo Akutwa Amefariki katika Nyumba ya Kulala Wageni.





Msichana Aliyetambuliwa kwa jina la Florence Ngwu, Mwanafunzi katika chuo kikuu cha Nigeria Amepatwa na Umauti Katika Hotel Moja Mjini Lagos, Nigeria. Mwili wa Msichana Huyo Ulikutwa sakafuni.

Mpaka Sasa hakuna taarifa za ziada zilizotolewa, pia haijajulikana ni kitu gani kilimtoa Chuoni na Kwenda Lagos.


Friday, July 26, 2013

Lulu Ajipanga Kurudi Darasani Tena


STAA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekazia nia yake ya kutaka kurudi shule siku chache zijazo.
Lulu aliandika hayo juzikati alipokuwa akichati na mashabiki wake kupitia ukurasa wa facebook ambapo alikuwa akiulizwa maswali na kuyajibu live kupitia Runinga ya East Africa.
Mmoja wa mashabiki wake alimuuliza Lulu kuhusu mipango yake ya kurudi shuleni ambapo alimjibu kuwa yupo katika mipango  hiyo hivyo hivi karibuni atarudi darasani.
“Am on process..soon mpenzi nitarudi darasani,” aliandika Lulu ambaye awali alidaiwa kukatisha masomo yake ya sekondari.
Source: GPL

Wednesday, July 24, 2013

Mlemavu wa Miguu amvua Papa Mwenye Kilo zaidi ya 250.


Kijana Mlemavu wa miguu, Matt Sechrist, 19 juzi aliandika kumbukumbu ya maisha yake baada ya kumkamata Papa mwenye uzito wa zaidi ya kilo 250 katika Fukwe za Vilano huko Florida.

Matt alifanikiwa kumkamata Papa huyo akisaidiwa na Baba yake pamoja na Rafiki wa Babab yake, Iliwachukua takribani saa moja kuhangaika na kiumbe huyo mpaka kumtoa nchi kavu, hata hivyo baada ya kupiga nae(Papa) picha za ukumbusho pamoja na watu wengine walimrudisha katika maji.

Monday, July 22, 2013

Huyu ndiye Msichana Mrembo kuliko wote, kwa mwaka 2013, Ashinda zaidi ya Million 4 Naira, Kuiwakilisha Nigeria Indonesia

-->

Anna Ebiere Banner, 18 ndio mshindi wa lile shindano la Mrembo Mzuri kuliko wote kwa Nigeria 2013. Msichana huyo aliweza kuibuka kidedea na kuwabwaga washindani wengine 31 na kujizolea kiasi cha shilingi za Kinageria 4 Million(Naira) 

Mshindi huyo anatarajia kuiwakilisha Nigeria katika kinyang'anyiro cha kumsaka Mrembo Mzuri wa Dunia mnamo Septer 28 huko Jakarta Indonesia.

AGNESS MASOGANGE KUPANDA KIZIMBANI TENA TAREHE 13 AGOSTI, HUKO AFRICA YA KUSINI



Hatima ya msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wabongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, waliokamatwa Afrika Kusini na dawa za kulevya kesi yao inatarajiwa kusomwa tena tarehe 13 Agosti mwaka huu nchini humo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliweka wazi kuwa wanadada hao wawili tayari walishapandishwa kizimbani wiki iliyopita.

Alisema kuwa kutokana na ushahidi kutokukamilika ndiyo sababu ya akinadada hao kusubiri kupanda kizimbani tena tarehe 13 ya mwezi ujao.

Kamanda Nzowa aliweka wazi kuwa nchi zote mbili zinashirikiana kwa ajili ya kufanya upelelezi wa jambo hilo: "Nchi zote mbili tunategemeana kwa upelelezi, hivyo sisi huku tunafanya wa kwetu na wao wanafanya wa kwao mwishoni tunaulizana tulipofikia hivyo ndivyo tunavyofanya kazi," alisema Nzowa.

Wadada hao ambao walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakitokea Tanzania, walikutwa na dawa za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazina matumizi nchini,  zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni sita.



Source: Mpekuzi

Saturday, July 20, 2013

UMAARUFU WA WASANII WENGI WA KIKE UNATOKANA NA SKENDO ZA PICHA CHAFU


NCHI za wenzetu staa kupiga picha za utupu si kitu kigeni lakini Tanzania sheria na maadili ya Mtanzania hayaruhusu kufanya hivyo.

Pamoja  na sheria  kutoruhusu, wasanii  wetu  hasa  wa  kike  wamekuwa  wakihaha  usiku  na  mchana  kuusaka  umaarufu  wa  kujulikana  kwa  jamii  kwa  njia  za  panya,.... 

Wengi  wao  wamepoteza  sifa  za  uwajibikaji  na  badala  yake  wamejikita  katika  Skendo  chafu  ili  jamii  iwajue...


Hali  hii  imewafanya  wasanii  wengi  wa  kike  wawe  na  umaarufu  wa  skendo  chafu....

Friday, July 19, 2013

Video: Angalia jinsi jamaa alivyopambana na Papa kwa Mikono yake tu!!!


Kama itatokea kwa wakazi Connecticut kumwona papa, basi haitakuwa vibaya kwani watamuita Elliot Sudal aje kuokoa jahazi maana mwanaume huyo ni maarufu na mashughuri kwa uwezo wake wa kucheza na kuwakamata viumbe hao hatari wa baharini, na ndo hapa tunauthibisha ule usemi wa waswahili usemao "AVUMAYE BAHARINI PAPA KUMBE........"

Angalia Video Ikimwonesha mambo yake hapa chini:-
-->

Thursday, July 18, 2013

Vijana waandamana kwa kuvaa "SKETI" wakishinikiza pendekezo la kuvaa "KAPTURA" Kipindi cha Majira ya Joto!!


Vijana hao pichani, ni wanafunzi kutoka Whitchurch High School ambao walifanya mgomo baridi ili kushinikza uongozi wa shule uwaruhusu wavae kaptura kipindi cha majira ya joto maana suruali zinakuwa ni mateso kwao, baada ya kitendo chao hicho, uongozi wa shule hiyo kupia kwa mkuu wa shule ulitoa ahadi ya kulizingatia ombi lao hilo na kwamba walitakiwa waendelee kuvaa suruali wakati mabadiliko yanapitishwa.


Monday, July 15, 2013

Wasichana wa Tanzania Wazidi kusota na Kesi za Madawa ya Kulevya, angalia full list hapa!!




 Mwandishi Wetu
MTANDAO wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda’ wa biashara hiyo haramu, Ijumaa Wikienda lina mtiririko wote.
Mrembo aliyehukumiwa miaka mitano Sandra Khan 'Binti Kiziwi'.
Hivi karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange’ amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ akiwa na kilo mia moja na hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda kortini mara moja Ijumaa iliyopita.
Wakati Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’, Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata la ‘unga’.
HABARI YA MJINI KWA SASA NI BINTI KIZIWI
Kuanzia Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo, mitandao hiyo haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi kufa au la! Sheria za hukumu hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi kufa.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
UKWELI WA BINTI KIZIWI NI HUU
Baada ya kusambaa kwa manenomaneno hayo, Ijumaa Wikienda liliingia mtaani kuisaka familia ya Binti Kiziwi lakini bila mafanikio.
Kwenye makazi ya mama yake, Buguruni, Dar, majirani walisema mzazi huyo amehama baada ya kufunga ndoa siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
IJUMAA WIKIENDA LAZIDI KUCHIMBA
Ijumaa Wikienda lilizidi kuzama ndani katika kuchimbua tetesi hizo ambapo lilifanikiwa kumpata ndugu wa kiume wa Binti Kiziwi na kufanya naye mazungumzo kama ifuatavyo:
Wikienda: Samahani, nimeambiwa wewe ni ndugu wa Binti Kiziwi, ni kweli?
Ndugu: (huku akitaja uhusiano wao) Ni kweli, nikusaidie nini?
Wikienda: Kuna manenomaneno kwamba Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya, ni kweli?
Ndugu: Sijui hizo habari watu wanazipatia wapi?! Watanzania wana maneno sana. Si kweli ndugu mwandishi.
Wikienda: Ukweli ni upi?
Ndugu: Kwanza kabisa Binti Kiziwi hakukamatiwa China, alikamatiwa Hong Kong, kwa sheria za kule mtu akipatikana na hatia ya kukutwa na ‘unga’ anahukumiwa jela tu.
“Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka.”
Wikienda: Nashukuru sana kwa ushirikiano ndugu yangu.
Ndugu: Asante, waambie Watanzania waache kuongeaongea sana.
Saada Ally Kilongo (26), maarufu kama ‘Demu wa Kanumba’.
DEMU WA KANUMBA NAYE ASOTA RUMANDE
Msichana anayejulikana kwa jina la Saada Ally Kilongo (26), maarufu kama ‘Demu wa Kanumba’ yeye bado anasota kwenye Gereza la Segerea, Dar kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170.
Saada alidakwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Juni 24, mwaka huu.
Kesi yake ilisikilizwa kwa mara ya kwanza, Juni 29, mwaka huu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.
Mdada huyo mkazi wa Mbezi Beach, Dar aliwahi kutoka kwenye Gazeti la Ijumaa la Desemba 9, 2011 ukurasa wa mbele kwa kichwa cha habari kisemacho: SAA 7 USIKU KANUMBA AGANDANA NA DEMU.
Demu huyo ambaye wakati huo alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar (alimaliza mwaka jana), picha yake akiwa na marehemu Kanumba ilipigwa Desemba 2, 2011 ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar ambapo kulirindima Tamasha la Usiku wa Kiafrika lililopambwa na mkali wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ipupa Nsimba ‘Fally Ipupa’.
Sharifa Mahamoud (27).
MSANII BONGO MUVI ‘ASUBIRI KITANZI’ MISRI
Wakati mlolongo wote ukiwa hivyo, mrembo aliyewahi kushiriki filamu Bongo, Sharifa Mahamoud (27) naye anashikiliwa katika gereza moja nchini Misri wakati kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya ikirindima nchini humo.
BALOZI WA TANZANIA -MISRI AZUNGUMZA
Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mohammed Haji, Mei 18, mwaka huu, Sharifa na nduguye, Abdallah Salum (28), wote wakazi wa Magomeni, Dar, walinaswa na unga jijini Cairo wakitokea Dar.
Mei 26, walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza. Madawa waliokutwa nayo ni heroine kilo saba (gharama ya fedha haikutajwa).
Kwa sheria za Misri, kosa la kukutwa na madawa ya kulevya ni kunyongwa hadi kufa. Lakini kwa mujibu wa Balozi Salum, hana kumbukumbu za raia wa kigeni aliyewahi kuhukumiwa kunyongwa nchini humo kwa kosa hilo.
Balozi alisema: “Endapo watapatikana na hatia kwamba kweli dawa hizo zilikuwa zao, hili litakuwa doa la kwanza kwa nchi yetu (Tanzania) hapa Misri.
Kwa mujibu wa Sharifa wakati akihojiwa na TV ya Misri, alishangaa kuona begi lake likiwa na madawa ya kulevya baada ya kukamatwa na kwamba aliingia nchini humo kumtafuta binamu yake.

Source: GPL
Blogger Widgets