Showing posts with label Mapenzi. Show all posts
Showing posts with label Mapenzi. Show all posts

Thursday, February 13, 2014

T.I AKASIRISHWA NA TABIA YA MKEWE KUJIACHIA HOVYO MITANDAONI, ANGALIA ALICHOFUNGUKA HAPA.


Inaonekana T.I hakubaliani na vile ambavyo mke wake anavyojiachia na kuuonyesha mwili wake kwenye mitandao ya kijamii na watu wote kuona.

Rappa huyo milionea ambaye pia muandaaji wa muziki wa hip hop anaonekana kuchukizwa na vitendo hivyo vinavyofanywa na mke wake.
Toka tetesi zilipoanza juu ya T.I. na Tiny kuwa na matatizo kwenye mahusiano yao, Tiny amekuwa akiweka picha zinazoonyesha maumbile yake kupitia Instagram.

Mnamo siku ya jumapili, T.I alionekana kukasirishwa zaidi na kuamua kuandika kwenye sehemu ya comment katika kumkumbusha Tiny akimwambia, ana kitu ziada kukitoa zaidi ya makali0 yake.

Hizi ni comments za T.I kwenye posti ya Tiny...

DC.

OBAMA NA KA SKENDO KA KUJIMEGEA BEYONCE


Gazeti moja la nchini Ufaransa Le Figaro linaripoti kamba BeyoncĂ© na Rais Barack Obama wana mahusiano ya kimap#nzi. Ndio, umesoma sahihi. Pascal Rostain, mpiga picha wa Kifaransa, amelieleza gazeti hilo kwamba “kuna kitu kikubwa kinaendelea” kati ya wawili hao.

“Nakuhakikishia kwamba Dunia italizungumzia hili,” aliongeza. 

Soma habari na angalia picha zaidi hapo chini....

Gala, ambalo ni kama Jarida la People la Ufaransa, pia limetaarifu kwamba Rais huyo wa Marekani na mke wake Michelle Obama wanaelekea kuachana.


Hakuna taarifa zilizotolewa zaidi juu ya uthibitisho wa Jarida hilo kuweza kusapoti kile ilichokiandika, ila tutafahamu zaidi hapo kesho.

Huku habari hizo zikiwa zinasambaa Barani Ulaya, inaoneka kwamba The Washington Post linategemea kutoka na na taarifa nyingine zaidi juu ya habari hiyo. 

Kris Coratti ambaye ni msemaji wa gazeti hilo, alisema kwamba tetesi hizo juu ya mahusiano ya kimap#nzi kati ya Bey na Barack kuwa “sio za kweli kabisa” na wana mpango wa kufanyia uchunguzi wa kina juu ya tetesi hizo.

Friday, February 7, 2014

MUIGIZAJI HUYU WA MOVIES ZA NG0N0 AMEPANIA KUFANYA MAP#NZI NA WANAUME 23 KATIKA KUSHEHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA


Msanii chipukizi wa wa filamu za ng0n0 Heidi Van H0'rny ana mpango wa kufanya pati ya kipekee kwenye siku yake ya kuzaliwa ndani ya Montreal.

Kwa watu wengine huwa ni mishumaa na keki, na kwa baadhi ya watu huwa ni misosi, mitungi na shots za hapa na pale.

Ila kwa msichana huyu chipukizi wa filamu za ng0n0 yeye binafsi ana mpango wa kuwaalika wanaume waliowahi kuwa wap#nzi wake 23 kwa ajili ya kuwaenzi siku hiyo kwa tukio hilo la kipekee atakapokuwa akitimiza miaka 23.


DC.

Monday, February 3, 2014

LADY JAY DEE ADAI TALAKA KWA GARDNER, SOMA KISA KIZIMA HAPA.


UNAWEZA ukakataa lakini ndivyo ilivyotokea, ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteini’ na Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ iliyofungwa miaka 9 iliyopita inadaiwa kuingia kidudu kufuatia mke huyo kuomba aandikiwe talaka, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye uthubutu wa kuripoti mkasa wote.
Jide akiwa na jumewe Gardner.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Jide au Lady Jaydee alifikia uamuzi huo baada ya Gardner kupata kazi ya kutangazia redio moja nchini Kenya.
HABARI KAMILI
Mnyetishaji wa kisanga hiki, aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa mara baada ya mume huyo kupata mchongo mzima alirudi nyumbani akiwa na furaha na kumwambia mkewe kuhusu bahati hiyo.
“Baada ya Gardner kupata mchongo wote wa kazi alikwenda mbio nyumbani kwake Kimara (Dar) ili akamwambie mkewe.
“Pia katika safari ya kwenda Kenya kupiga mzigo ilikuwa aende na mkewe huyo kwa sababu lilikuwa suala la kuhamisha makazi yao Tanzania,” kilisema chanzo hicho.
Jide na Gardner siku ya ndoa yao.
JIDE AHAMAKI
Chanzo kikatoboa kwamba Gardner alipofika nyumbani kwake na kumweleza mkewe, alikumbana na kitu ambacho hakukitarajia.
“Komando (Jide) alihamaki na kumjia juu akisema yeye hawezi kuondoka Tanzania kwenda kuishi Kenya, kama Gardner analiona jambo hilo ni heri kwake, amuandikie talaka yake na kuachana ili kila mmoja achukue hamsini zake,” chanzo kilizidi kuporomosha maneno.
KWA NINI JIDE HAKUPENDA? 
Habari zilizidi kuanikwa kwamba Jide au Binti Machozi alifikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa kitendo cha kwenda kuishi Kenya kitaua bendi yake ya Machozi na sehemu ya biashara ya Nyumbani Lounge iliyopo Ada-Estate, Kinondoni, Dar.
MBAYA ZAIDI
Taarifa zikazidi kumiminika kwamba, mbali na Jide au Anakonda kuhofia biashara zake kufa, lakini pia hakupenda Gardner aondoke hata peke yake kwa sababu yeye ndiye meneja wa miradi hiyo miwili.
“Mimi nilipopata habari hizo nilikutana na Jide nikamuuliza, akanijibu ameamua iwe hivyo tu, kikubwa mumewe (Gardner) aamue moja kati ya hayo mawili kwani yeye ana haki akiwa kama mkewe wa ndoa,” kilisema chanzo kikimkariri Jide.
GARDNER AISHIWA NGUVU
Kufuatia majibu ya mkewe, taarifa zinasema mtangazaji huyo ambaye alishawahi kupiga mzigo kwenye kituo cha Radio Clouds FM cha jijini Dar alijikuta akiishiwa nguvu na kuachana na dili hilo mara moja.
“Gardner alisalimu amri kwa mkewe, akaamua kuachana na dili la kwenda kutangaza Kenya. Lakini alifikiri sana akasema ni kweli kuhamia Kenya kungeua miradi yao ya Tanzania maana ingekosa msimamizi wa kuaminika,” chanzo kiliweka wazi.
KAMA ANGEKWENDA KENYA
Siri hiyo iliyovujia mikononi mwa Ijumaa Wikienda haikuishia hapo, ilizidi kuanikwa kwamba kama Kapteini angekwenda Kenya na kuanza kazi, ilikuwa alipwe mshahara wa shilingi za Kenya laki 3 kwa mwezi (kama milioni 6 za Tanzania).

NAFASI YAKE BADO IPO
Mpashaji wetu alisema kwamba nafasi ya Gardner kwenye kituo hicho cha redio ambacho hakikutajwa, bado ipo lakini tamko la Jide nalo li hai, kwa vile hakubatilisha, endapo mumewe atataka kwenda hata kesho (Jumanne) aandike talaka.
WIKIENDA NA GARDNER
Baada ya kunyetishiwa taarifa nzima, juzi gazeti hili lilimsaka Gardner. Kwa njia ya simu lilimkosa, likamfuata Nyumbani Lounge. Lilipomkuta lilimsimulia kisanga chote cha ndoa yake kutikiswa na kitendo cha yeye kupata kazi Kenya ambapo alijibu hivi:
“Ndoa ni nzuri, ni kweli ilikuwa niende Kenya, nilipata kazi kule lakini kama familia ilikuwa lazima tukae na kupanga, mwenzangu hakuafiki.”
Wikienda: “Ni kweli shemeji ameomba uchague mawili, umwandikike talaka au uende Kenya?”
Gardner: “Ndiyo maana nimesema ndoa nzuri, lazima makubaliano yawepo, mke anaweza kuonesha msimamo wake na mume kama utakaa chini na kuufikiria ukapata jibu unakubaliana na mke wako wala hakuna ubaya.”
Wikienda: “Kule mshahara wako ungekuwa shilingi ngapi?”
Gardner: “Hiyo sasa ni siri ya makubaliano.”
Wikienda: “Kwa nini usiamue kwenda tu?”
Gardner: “Nimekwambia ndoa nzuri.”
JIDE BIZE
Juhudi za kumpata Jide ziligonga mwamba baada ya muda wote kuwa bize na shoo ya kukata na shoka aliyokuwa akiifanya siku hiyo kwenye ukumbi huo akikimbiza na nyimbo zake kali za zamani na hizi mbili zilizogeuka nyimbo za taifa, Joto Hasira na Yahaya.
RAFIKI WA GADNER AMCHAMBUA JIDE
Rafiki wa karibu na Gardner (jina tunalo) ambaye alisikia mahojiano ya mtangazaji huyo na Ijumaa Wikienda, alisubiri jamaa aondoke ambapo alianza kumchambua Jide.
“Nataka kuwaambia kitu, Jide ni mwanamke jasiri sana. Ana msimamo na anaposhikilia msimamo wake hatengui hasa kama atabaini kuwa yupo sahihi.
“Ni kweli jamaa (Gardner) alipata kazi Kenya tena mshahara mzuri tu, lakini mama (Jide) akaweka ngumu hakuna kwenda,” alisema rafiki huyo.
GPL

"NINGEMKOSA H BABA MAISHANI MWANGU NINGEYUMBA" FLORA


UA la Bongo Movies, Flora Mvungi amefunguka kuwa anashukuru Mungu kumpata mume mwema, Hamisi Baba ‘H.Baba’ kwani vinginevyo angeyumba kimaisha.
Flora Mvungi na mumewe H. Baba.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Flora alisema H. Baba ni mwanaume anayestahili sifa zote hivyo endapo angekutana na mwanaume mwingine basi angeyaona mapenzi machungu.
“Mungu hakukosea kuniletea H. Baba, nampenda sana kwani ni mtu anayenijali mimi na mtoto wetu Tanzanite yaani sijui kitu gani ambacho nakikosa kwake, bila huyu maisha yangeyumba,” alisema Flora.

RAYUU BADO ANATAMANI KUTEMBEA NA MUME WA MTU, ASEMA HAWEZI KUJIZUIA.


MSANII kinda kwenye tasnia ya filamu Bongo, Rahma Bagenzi ‘Rayuu’ amesema kuwa, kamwe hatokoma kutembea na waume za watu kwa kuwa sheria ya dini yake ya Kiislamu inamruhusu kuolewa na mume wa mtu.
Rahma Bagenzi ‘Rayuu’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Rayuu alisema kipindi cha nyuma aliwahi kutoka kimapenzi na mume wa mtu (hakumtaja jina) na kufikia hatua ya kufikishwa polisi na mwenye mke lakini haimaanishi kuwa hatatembea tena na mume wa mtu.
“Nikila kiapo cha kutotembea na waume za watu nitakuwa naongopa, kwanza dini yetu imeruhusu ndoa za uke wenza huenda  Mungu kaniandikia niolewe ndoa ya aina hiyo sina uwezo wa kupingana naye,” alisema Rayuu.

GPL.

Friday, January 31, 2014

BABU MPENDA TOTOZ, AFUMWA UCH** WA MNYAMA NA KADENTI CHA SHULE, GUEST HOUSE.


YELEUUUWI! Ile tabia ya wazee ya kupenda dogodogo imemtokea puani mzee aliyetajwa kwa jina moja la mzee Omari, ni Ijumaa pekee lenye ubavu wa kuripoti sinema hiyo ya bure.
AIBU YA MWAKA: Babu akifunika uso wake baada ya kunaswa na denti gesti.
Mzee huyo alinaswa laivu akiwa gesti na denti wa shule moja ya sekondari jijini Dar (jina la denti na shule vinahifadhiwa kimaadili).
Tukio hilo la aibu lilijiri juzikati kwenye gesti moja iliyopo maeneo ya Kawe, Dar na kusababisha timbwili zito.
TAARIFA MEZANI KWA OFM
Hivi karibuni, kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, kilipokea lalamiko kutoka kwa mzazi wa denti huyo ambaye alieleza juu ya mabadiliko ya mwanaye kitabia na kushuka kitaaluma kutokana na kusumbuliwa na ‘mbaba’ huyo.
Mzazi huyo aliiambia OFM kuwa amekuwa akifuma mawasiliano ya kwenye simu ya mkononi ya mwanaye na mwanaume huyo ambaye alikuwa hamfahamu.
FUNDISHO KWA WAZEE: Babu akijiandaa kuvaa nguo yake ya ndani baada ya kunaswa gesti.
CHANZO
Mama huyo alisema kuwa kutokana na maendeleo ya mwanaye kuzidi kudorora shuleni, aliamua kumfuatilia kwa karibu kwa kuwa hakutaka apotee.
Mama huyo alitiririka kuwa, siku ya tukio, alimsikia mwanaye huyo akiwekeana miadi kwenye simu na mwanaume huyo ndipo akaamua kumuwekea mtego.
Alisema wakati mwanaye huyo akilonga kwenye simu, yeye alibana sehemu na kuyasikia yote ambayo alikuwa akiyaongea na kwamba walipanga kukutana baa.
“Nilichokifanya nilimpigia simu mjomba wake na kumweleza kila kitu, nikamwelekeza namna ya kumfuatilia. Alichukua bodaboda na kuanza kumfuatilia. Mimi na timu yangu tulifuata nyuma,” alisema mama huyo kwa uchungu.
CHINI YA ULINZI: Babu akiwa mikononi mwa wanausalama.
Alisema mzee huyo alikubaliana na mwanaye wakutane kwenye baa hiyo ambapo ndani yake kuna nyumba ya kulala wageni a.k.a gesti.
OFM YAITWA
Baada ya mpango wa mtego kukamilika ndipo mama huyo akawaita OFM ambao huwa hawalazi damu hivyo walifika mara moja.
TAARIFA POLISI
Kabla ya kuchukua hatua yoyote, walishauriana kutoa taarifa kituo cha polisi, jambo ambalo lilifanyika na kupatiwa msaada wa kiusalama.
NI SAWA NA BABU YAKE
Walipofika kwenye baa hiyo mama mtu alipigwa na butwaa kumuona mtu aliyekuwa akiwasiliana na mwanaye ni mzee sawa na babu yake.
“Yaani jamani kweli dunia imekwisha, mwanangu ni sawa na mjukuu wa huyu mzee, ama kweli tamaa mbaya sana,” alisema mama huyo kwa uchungu.
Huku wakifuatiliwa kwa karibu, mzee huyo na denti walipiga madikodiko na vinywaji ndipo wakatimba kwenye gesti hiyo.
Kilichofanyika ni kwamba polisi na mama wa denti walizama gesti hiyo na kuomba kumsaka mwanafunzi huyo, jambo ambalo halikupingwa.
FUMANIZI LAIVU
Baada ya kuzama ndani ndipo mtego ukafyatuka ambapo mzee Omari alibambwa katika moja ya vyumba vya gesti hiyo huku akiwa amejifunga taulo tu.
Mzee huyo alipatwa na taharuki kubwa asijue la kufanya kufuatia timbwili zito alilozua mama wa denti huyo.
“Kha! Kazi kuharibu watoto wa wenzenu, hivi angekuwa wa kwako ukakuta akifanyiwa hivi ungejisikiaje? Nasomesha kwa gharama kubwa wewe unataka kuniharibia. Hivi hujui mtoto anauma?” alihoji mama huyo kwa hasira huku akimtandika mwanaye vibao.
OMBI
Mara baada ya mzee huyo kunaswa, aliomba chondechonde kukaa na familia ya mwanafunzi huyo ili kuyamaliza yasifike mbali.
Hata hivyo, baada ya maombi ya muda mrefu walikubaliana kuandikishiana ambapo mzee huyo alitakiwa kulipa faini.
“Sisi hatuna maneno mengi, hatutaki kesi ila atulipe fidia ya kumsababishia mtoto wetu asiwe na mahudhurio mazuri shuleni kutokana na ulaghai wake,” alisema mzazi huyo.
MZEE AINGIA MITINI
Habari zilieleza kuwa mzee huyo alishindwa kulipa mara moja badala yake aliingia mitini kwa kigezo kuwa anakwenda kutafuta faini hiyo.
Hadi OFM inaondoka eneo la tukio mzee huyo alikuwa hajawasilisha faini waliyokubaliana hivyo tunafuatilia na tutakachobaini tutaandika katika matoleo yajayo.
FUNDISHO
Hivi sasa kumeshamiri tabia ya wazee kupenda kuharibu mabinti wadogo hivyo kunaswa kwa mzee huyo litakuwa fundisho kwa wengine kwani OFM ambao huwa haikosei, imeamua kulivalia njuga suala hilo. Subirini muone!

GPL.

WOLPER APAGAWA NA PENZ* LA JAMAA WAKE MPYA, AWACHANA WATU WASIMSHOBOKEE!!


THE Ijumaa Sexiest Girl 2012, Jacqueline Wolper amesema kuwa, ana imani kubwa na mpenzi wake wa sasa aliyemtambulisha kwa jina la G Modo akiamini atampoza machungu aliyoyapata kutoka kwa mpenzi wake wa zamani, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ huku akiwatahadharisha mashosti zake kutoleta shobo (kuwa mbali naye).
Jacqueline Wolper.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Wolper alisema anafikia hatua ya kusema hayo kwa kuwa muda mfupi aliokuwa naye amegundua ni mwanaume anayejitambua na anayeheshimu mapenzi ila akawataka mashosti zake kutomsogelea.
“Tangu niwe na huyu kijana nimekuwa ni mwenye furaha kubwa, nasahau hata yale machungu niliyopata kwa mpenzi wangu wa zamani. Lakini najua wapo wanaomtolea macho, tusitafutane ubaya, kila mtu na maisha yake,” alisema Wolper.
GPL.

KILA MTU NA "ULEVI" WAKE, JE WAJUA STAREHE YA WASTARA NI NINI?!!!!


MSANII wa filamu, Wastara Juma amefunguka kuwa starehe yake kubwa duniani ni kukumbatiwa na anapofanyiwa kitendo hicho na mtu wa jinsia yoyote huwa hoi.
Wastara Juma.
Akistorisha na paparazi wetu, Wastara alisema: “Mimi napenda sana kukumbatiwa au kukumbatia, awe ni mwanaume au mwanamke, ndugu yangu au hata kama siyo ndugu yangu, tukikumbatiana tu najisikia raha sana.
“Unajua kila mtu anakuwa na kitu anachokipenda duniani sasa mimi starehe yangu ndiyo hiyo hata marafiki zangu wanajua kwamba mimi napenda kukumbatiwa.”

Wednesday, January 29, 2014

HATIMAYE SHILOLE ANASA KWA MCHUMBA WA KIZUNGU.

KWA mara ya kwanza msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa akiwa na mwanaume wa Kizungu anayedaiwa kuwa ndiye mchumba wake.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mchumba wake.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, safari za mara kwa mara za Shilole nchini Uingereza zimekuwa zikisababishwa na mchumba huyo wa Kizungu ambaye huwa anamuita kufurahia p#nzi lao pamoja na kumtafutia shoo mbalimbali.
“Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye shoo ya mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini Uingereza na hivi karibuni ataenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili limekuwa la kwanza kunasa picha kadhaa za Shilole akiwa katika mapozi tofauti ya kimahaba na Mzungu huyo.
Baada ya chanzo hicho kumwaga ‘upupu’ huo, mapaparazi wetu walimtafuta Shilole ili aweze kufunguka ambapo bila kuumauma maneno, alikiri kuwa amepata mchumba huyo aliyemtambulisha kwa jina la Ankar.
Akizidi kumwaga data za boifrendi wake huyo, Shilole alisema awali walikutana kwenye moja ya shoo zake nchini humo ndipo urafiki ulipoota mizizi na kufikia hatua ya kuwa wap#nzi.
“Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni raia wa Uingereza, nilipokuwa napataka nimefika, sipindui tena. Unajua muziki wangu na mauno yangu yanawavutia sana watu, siku ya kwanza aliniona kwenye shoo akanipenda ndipo tukaanzisha urafiki.



“Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini humo kwa mwaliko maalum alionipa, nitaenda peke yangu kwani safari nyingine zote zilizopita nilikuwa naenda na watu,” alisema Shilole.

MAMA WEMA SEPETU AWASAKA DIAMOND NA MWANAE ILI AWAANZISHIE VARANGATI.

HABARI mpya! Mama wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu anadaiwa kuingia rasmi mitaani akiwasaka wap#nzi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Wema, chanzo cha uhakika kimesema na Amani.
Wema na Diamond wakiwa katika pozi la kim@haba.
Kwa mujibu wa chanzo hicho makini, mama Wema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kusikia taarifa kutoka kwa watu kwamba, Diamond amekuwa akisambaza maneno mitaani kuwa haogopi vitisho vya mwanamke huyo kufuatia hatua yake ya kumrudia binti yake.
ILIKUWAJE KWANI?
Hivi karibuni, mama Wema alizungumza na gazeti tumbo moja la hili, Ijumaa Wikienda linalotolewa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kila siku ya Jumatatu na kusema kitendo cha Diamond kumrudia bintiye hakubaliani nacho.
Aliongeza kuwa, kufuatia hatua hiyo iko siku ataingia mtaani kumsaka Diamond na popote pale atakapomnasa, atamkata na panga.
Mama Wema, Mariam Sepetu anayewasaka wap#nzi hao.
TURUDI KWA CHANZO
“Jamani si mnakumbuka juzikati mama Wema alisema atamsaka Diamond? Sasa amesikia Diamond anatangaza mitaani kwamba, hatishiki na tamko la mama mkwe wake huyo na watakapokutana watajua nani zaidi.
“Hivi ninavyosema, mama Wema ameingia mtaani kuwasaka. Lengo lake awakute wote wawili ili awaanzishie timbwili la kufa mtu.
“Tangu Ijumaa iliyopita, kila siku anatoka kwenda mitaani kuwasaka, naamini siku akiwakuta pamoja kweli itakuwa vita kubwa,” kilisema chanzo chetu.
Gari la Wema na la Diamond yakiwa yameegeshwa nyumbani kwa Wema.
KWA NINI ASIENDE NYUMBANI?
Chanzo kilipoulizwa kama kweli mama Wema amepania kuwanasa wawili hao, kwa nini asiwafuate nyumbani kwa binti yake, Kijitonyama, Dar ambako wanapika na kupakua, kilijibu:
“Ameweka mtego wake pale, bahati mbaya sana Diamond naye anaishi kwa machale. Kuna siku anakwenda kulala kuna siku haendi. Huenda na yeye (Diamond) ameweka watu wake ndani kwa Wema wa kumpelelezea kama mama Wema atakwenda au ana dalili za kwenda.”
Chanzo kikaendelea: “Siku hizi Diamond anaweza kwenda kwa Wema, akaacha gari lake na kutoka na la Wema na kurudi kwake usiku sana.”
Paparazi wa GPL akiwa nyumbani kwa Diamond.
AMANI LAWASAKA WAHUSIKA
Baada ya kuzinyaka nyeti hizo, Amani liliamua kuutafuta ukweli ambapo Jumanne iliyopita lilimsaka mama Wema kwa njia ya simu lakini iliita bila kupokelewa.
Amani lilitumia simu zake mbili kumpigia mwanamke huyo.
Baada ya dakika tano, mama huyo mwenye ‘machungu’ na mwanaume yeyote anayemchezea bintiye alituma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) akisema: Nipo msibani tuma sms. Pia akatuma sms kwenye simu ya pili akisema: Nipo msibani, ulikuwa unasemaje?
Amani lilimtumia madai yote kuhusu yeye kuanza kuwatafuta Wema na Diamond, pia likamjulisha kwamba kama anawatafuta kweli, muda huo, wawili hao walikuwa wapo chumbani kwa Wema hawajaamka.
Hata hivyo, mama Wema hakujibu meseji yoyote kati ya hizo mbili hali iliyotafsiriwa na Amani kuwa, uchungu wa msiba ulimuondolea uwezo wa mawasiliano.
Paparazi wa GPL akiongea na mlinzi wa Wema nyumbani kwake.
NYUMBANI KWA DIAMOND
Mapaparazi wetu walitia timu nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori na kukutana na mtu mmoja aliyedai ni mjomba wa staa huyo ambaye alidai Diamond Platnumz alitoka asubuhi na mama yake, Sanura Kassim kwenda Tegeta, Dar.
NYUMBANI KWA WEMA
Baada ya kutoka nyumbani kwa Diamond huku wakiamini Mbongo Fleva huyo kaenda Tegeta kama alivyosema mjomba mtu, mapaparazi walikwenda nyumbani kwa Wema.
Baada ya kugonga geti kwa dakika moja, alitokea mlinzi na mambo yalikuwa kama ifuatavyo;
Paparazi: Mambo?
Wema.
Mlinzi: Poa, karibu.
Paparazi: Asante, nina shida na Wema, sijui nimemkuta?
Mlinzi: Wamelala, hawawezi kuamka muda huu.
Paparazi: Wamelala? Nani na nani?
Mlinzi: Madam (Wema) na Diamond.
Diamond.



Paparazi: Ina maana Diamond yumo ndani?
Mlinzi: Si nimekwambia wamelala?
Paparazi wetu alifanikiwa kupenyeza macho kwenye nafasi ya uzio na kuyaona magari ya wote wawili, la Diamond aina ya Toyota Land Cruiser V8 na la Wema, Toyota Lexus Harrier.

Tuesday, January 28, 2014

MASTAA WA BONGO MOVIE WAMPONDA WEMA SEPETU BAADA YA KUNYANG'ANYWA KILA KITU NA MP#NZI WAKE KIGOGO WA SERIKALINI.


MASTAA wa kike Bongo wamecharuka na kutoa yao ya moyoni baada ya nyota mwenzao, Wema Sepetu kubwagwa na aliyekuwa mpenzi wake, anayetambulika kwa jina moja la Clement na kumnyang’anya vitu alivyompa kama zawadi wakati wa mapenzi yao.
Wema Sepetu.
Kuhusu Wema kuporwa ofisi yake ya Endless Fame Film Production, kupewa notisi ya nyumba aliyokuwa amepangiwa na kigogo huyo anayeelezwa yupo serikalini na kunyang’anywa magari siyo stori kabisa mjini.
Risasi Mchanganyiko lilifanya mahojiano na mastaa hao wikiendi iliyopita, kwa njia ya simu na kuwahoji kuhusu kitendo alichofanyiwa mwenzao ambapo walifunguka bila wasiwasi wowote.
USENGENYAJI
Wakali hao, waliopata kuzungumza na waandishi wetu kwa nyakati tofauti, baadhi wamemponda Wema kwa kutokuwa makini wakati akiwa kwenye uhusiano na kigogo huyo kwa kutaka kukabidhiwa hati za vitu alivyopewa.
Wa kwanza kuzungumza ni Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye alisema: “Mimi namshukuru Mungu kwa sababu sijapangiwa nyumba na mwanaume.  Naishi maisha yangu simpo ya furaha na amani, sipendi kuigiza maisha. Hao wasanii wanaopenda mambo makubwa wakati hawana uwezo,  nawashauri wafanye kazi, filamu zinalipa sana. Wasipende vitu vya haraka, maana siku zote vizuri huja taratibu.”
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
“Mastaa tusijiachie sana kwa wanaume, kama ukipewa gari, upewe na kadi... tusidanganyike na tusipende kuhongwa, tutafute vya kwetu. Kama mtu anakupenda na anakusaidia kwa mapenzi mema, sawa mheshimu.”
WASTARA JUMA
“Inabidi tujitambue jamani, maana kuna watu wanatembea na mastaa makusudi ili wajulikane au kwa manufaa yao wenyewe. Tuache kuishi kwa kutegemea migongo ya wengine. Wengi hawana mapenzi ya kweli. Hata kama mmeachana, sasa kuna sababu gani ya kumnyang’anya mtu vitu ulivyompa?”
NURU NASSOR ‘NORA’
“Mimi najisikia vibaya sana... kama mtu unajiamini una kipaji, kwa nini usifanye kazi?  Mastaa tuache kujitangaza, kwa sababu tunatumika kama vyombo vya starehe tu.  Tutafute ndoa, tusitumie ustaa kufanya ufuska kwa sababu mali zinapita na mwisho wa siku tunaharibu maisha yetu.”
TAMRINA POSH ‘AMANDA’
“Utapeli ni mwingi, haya mambo ya kupewa vitu siyo vizuri kabisa, tuache.  Wanawake tuna akili fupi sana na tunajisahau tunapokuwa na wanaume wakati wenyewe wana kitu moyoni mwao, akishapata anachotaka anaanza matatizo.



“Bora nitembelee taksi au Bajaj kuliko kudhalilishwa... wanawake ni wajinga na huwa tunajidanganya kwa vitu visivyo vyetu, mwisho wa siku tunaumbuka. Tuache sifa za kijinga.”
Blogger Widgets