Friday, January 31, 2014

BABU MPENDA TOTOZ, AFUMWA UCH** WA MNYAMA NA KADENTI CHA SHULE, GUEST HOUSE.


YELEUUUWI! Ile tabia ya wazee ya kupenda dogodogo imemtokea puani mzee aliyetajwa kwa jina moja la mzee Omari, ni Ijumaa pekee lenye ubavu wa kuripoti sinema hiyo ya bure.
AIBU YA MWAKA: Babu akifunika uso wake baada ya kunaswa na denti gesti.
Mzee huyo alinaswa laivu akiwa gesti na denti wa shule moja ya sekondari jijini Dar (jina la denti na shule vinahifadhiwa kimaadili).
Tukio hilo la aibu lilijiri juzikati kwenye gesti moja iliyopo maeneo ya Kawe, Dar na kusababisha timbwili zito.
TAARIFA MEZANI KWA OFM
Hivi karibuni, kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, kilipokea lalamiko kutoka kwa mzazi wa denti huyo ambaye alieleza juu ya mabadiliko ya mwanaye kitabia na kushuka kitaaluma kutokana na kusumbuliwa na ‘mbaba’ huyo.
Mzazi huyo aliiambia OFM kuwa amekuwa akifuma mawasiliano ya kwenye simu ya mkononi ya mwanaye na mwanaume huyo ambaye alikuwa hamfahamu.
FUNDISHO KWA WAZEE: Babu akijiandaa kuvaa nguo yake ya ndani baada ya kunaswa gesti.
CHANZO
Mama huyo alisema kuwa kutokana na maendeleo ya mwanaye kuzidi kudorora shuleni, aliamua kumfuatilia kwa karibu kwa kuwa hakutaka apotee.
Mama huyo alitiririka kuwa, siku ya tukio, alimsikia mwanaye huyo akiwekeana miadi kwenye simu na mwanaume huyo ndipo akaamua kumuwekea mtego.
Alisema wakati mwanaye huyo akilonga kwenye simu, yeye alibana sehemu na kuyasikia yote ambayo alikuwa akiyaongea na kwamba walipanga kukutana baa.
“Nilichokifanya nilimpigia simu mjomba wake na kumweleza kila kitu, nikamwelekeza namna ya kumfuatilia. Alichukua bodaboda na kuanza kumfuatilia. Mimi na timu yangu tulifuata nyuma,” alisema mama huyo kwa uchungu.
CHINI YA ULINZI: Babu akiwa mikononi mwa wanausalama.
Alisema mzee huyo alikubaliana na mwanaye wakutane kwenye baa hiyo ambapo ndani yake kuna nyumba ya kulala wageni a.k.a gesti.
OFM YAITWA
Baada ya mpango wa mtego kukamilika ndipo mama huyo akawaita OFM ambao huwa hawalazi damu hivyo walifika mara moja.
TAARIFA POLISI
Kabla ya kuchukua hatua yoyote, walishauriana kutoa taarifa kituo cha polisi, jambo ambalo lilifanyika na kupatiwa msaada wa kiusalama.
NI SAWA NA BABU YAKE
Walipofika kwenye baa hiyo mama mtu alipigwa na butwaa kumuona mtu aliyekuwa akiwasiliana na mwanaye ni mzee sawa na babu yake.
“Yaani jamani kweli dunia imekwisha, mwanangu ni sawa na mjukuu wa huyu mzee, ama kweli tamaa mbaya sana,” alisema mama huyo kwa uchungu.
Huku wakifuatiliwa kwa karibu, mzee huyo na denti walipiga madikodiko na vinywaji ndipo wakatimba kwenye gesti hiyo.
Kilichofanyika ni kwamba polisi na mama wa denti walizama gesti hiyo na kuomba kumsaka mwanafunzi huyo, jambo ambalo halikupingwa.
FUMANIZI LAIVU
Baada ya kuzama ndani ndipo mtego ukafyatuka ambapo mzee Omari alibambwa katika moja ya vyumba vya gesti hiyo huku akiwa amejifunga taulo tu.
Mzee huyo alipatwa na taharuki kubwa asijue la kufanya kufuatia timbwili zito alilozua mama wa denti huyo.
“Kha! Kazi kuharibu watoto wa wenzenu, hivi angekuwa wa kwako ukakuta akifanyiwa hivi ungejisikiaje? Nasomesha kwa gharama kubwa wewe unataka kuniharibia. Hivi hujui mtoto anauma?” alihoji mama huyo kwa hasira huku akimtandika mwanaye vibao.
OMBI
Mara baada ya mzee huyo kunaswa, aliomba chondechonde kukaa na familia ya mwanafunzi huyo ili kuyamaliza yasifike mbali.
Hata hivyo, baada ya maombi ya muda mrefu walikubaliana kuandikishiana ambapo mzee huyo alitakiwa kulipa faini.
“Sisi hatuna maneno mengi, hatutaki kesi ila atulipe fidia ya kumsababishia mtoto wetu asiwe na mahudhurio mazuri shuleni kutokana na ulaghai wake,” alisema mzazi huyo.
MZEE AINGIA MITINI
Habari zilieleza kuwa mzee huyo alishindwa kulipa mara moja badala yake aliingia mitini kwa kigezo kuwa anakwenda kutafuta faini hiyo.
Hadi OFM inaondoka eneo la tukio mzee huyo alikuwa hajawasilisha faini waliyokubaliana hivyo tunafuatilia na tutakachobaini tutaandika katika matoleo yajayo.
FUNDISHO
Hivi sasa kumeshamiri tabia ya wazee kupenda kuharibu mabinti wadogo hivyo kunaswa kwa mzee huyo litakuwa fundisho kwa wengine kwani OFM ambao huwa haikosei, imeamua kulivalia njuga suala hilo. Subirini muone!

GPL.

No comments:

Post a Comment

Blogger Widgets