Sunday, July 27, 2014

MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA


MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA
Matokeo ya marathon wanaume:
1. Michael Shelley - Australia
2. Stephen Chmelamy - Kenya
3. Abraham Kiplimo - Uganda
4. M Mutai - Uganda
5. J Kelai - Kenya
6. E Ndema - Kenya
7. L Adams - Australia
8. P Kiplimo - Uganda
9. D Hawkins - Scotland
10. S Way - England
11. Fabiano Naasi - Tanzania



Kipa Ospina asajiliwa Arsenal http://wp.me/p2FUKJ-4VF
















 image

Kipa Ospina asajiliwa Arsenal

*Mourinho aubeza mshahara wa Shaw
* Ferdinand aanza Queen Park Rangers

Wakati Arsenal wamekamilisha usajili wa golikipa wa Timu ya Taifa ya Colombia, David Ospina, Queen Park Rangers (QPR) wameanza kupata huduma za mabeki wa kati Rio Ferdinand na Steven Caulker huku Jose Mourinho akimvaa Luke Shaw.
Arsenal wamefanikisha usajili wa kipa ambaye aliruhusu mabao machache zaidi katika hatua za makundi kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil majuzi, taarifa hiyo ikiwa imetolewa na kocha wa klabu yake ya Nice, Claude Puel.
Ospina (25) amekuwa na klabu hiyo ya Ufaransa tangu 2008 na alisaidia nchi yake kufika hatua ya robo fainali na kocha Puel alisema Arsenal watafurahi kwani Ospina ni kipa mzuri sana.
image

Pasipo kuthibitisha usajili huo, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alijibu swali la waandishi wa habari kwa kusema aliamini kwamba kipa huyo alifanya vyema sana kwenye michuano ya Kombe la Dunia.
Wenger amepata kunukuliwa akisema kwamba kuna uwezekano wa Ospina kumpoka namba kabisa kipa namba moja wa Arsenal, Mpolishi Wojciech Szczesny. Ospina alicheza dakika zote za mechi zote za Colombia na nchi hiyo iliruhusu pia mabao machache zaidi miongoni mwa timu za Amerika Kusini wakati wa mechi za kufuzu.
Ospina ndiye alichukua mikoba ya Hugo Lloris aliposajiliwa na Tottenham Hotspur kutoka Lyon lakini kabla ya hapo alikuwa Nice.
  MOURINHO ASEMA SHAW GHALI MNO
20140402-155822.jpg 
Kocha wa Chelsea,  Jose Mourinho ameendelea kuzungumzia masuala ya wachezaji wa timu nyingine, akiwashangaa Manchester United kumsajili beki wa kushoto wa Southampton ambaye ni ghali sana.
Mourinho amedai kwamba madai ya mshahara mkubwa ya Shaw yangeweza ‘kuiua’ Chelsea. Shaw alisajiliwa kwa pauni milioni 27 na amekuwa akiwaniwa na timu nyingi, ikiwa ni pamoja na Arsenal na Liverpool.
Mreno huyo amedai Shaw kulipwa pauni 100,000 kwa wiki ni kiasi kikubwa mno, lakini Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amedai kwamba atakaa faragha na Mourinho kuzungumzia suala hilo.
“Tukimlipa kijana mwenye umri wa miaka 19 kile tulichotakiwa kumlipa, basi kumsajili Luke Shaw kungetuua. Tungeua uthabiti wetu huku tukitakiwa kuzingatia uungwana katika matumizi ya fedha, sasa ukimlipa kijana mdogo kiasi hicho basi kesho yake wengine watakuvamia kutaka nyongeza,” akasema Mourinho.
Mourinho anajenga hoja kwamba si sahihi mchezaji mpya na mwenye umri mdogo kiasi hicho kulipwa kuliko wakongwe ambao wamechezea klabu mechi hadi 200, kuiletea mataji na sifa nyingi.

FERDINAND, CAULKER WAANZA KAZI QPR
20140718-150851-54531954.jpg 

Mabeki wapya wa kati wa Queen Park Rangers (QPR), Rio Ferdinand na Steven Caulker wameanza rasmi majukumu katika klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu baada ya kuwa imeshuka msimu uliopita.
Waingereza hao wawili walicheza dakika 45 kila mmoja katika mechi ya kirafiki nchini Ujerumani kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu ya England inayoanza mwezi ujao. Ferdinand alianza kufundishwa soka ya kulipwa na kocha wa sasa wa QPR, Harry Redknapp.
Katika hatua nyingine, QPR wameamua kumrejesha kipa wao, Julio Cesar (34) wa Brazil aliyekuwa ametolewa kwa mkopo katika klabu inayocheza Ligi ya Marekani ya Toronto FC. Kipa mwingine katika QPR ni Mwingereza, Robert Green.
Wakati huo huo, West Ham United wamepata pigo kubwa, baada ya mshambuliaji wao wa kutegemewa kuumia enka na hivyo atakuwa nje ya dimba kwa miezi karibu minne, ikimaanisha ataanza kucheza Novemba.

Loga amvizia Hamis Kiiza

UONGOZI wa Simba umegawanyika wapo ambao hawataki kusikia usajili wa mchezaji yoyote kutoka Yanga lakini wapo mabosi watatu huwaambii kitu kuhusu Emmanuel Okwi.
Kocha wa Simba,Zdravko Logarusic ‘Loga’ alisema; “Nawajua hao wachezaji Okwi na Kiiza ni wachezaji wazuri niliwaona msimu uliopita, sina pingamizi kama nitaletewa hapa, ninachotaka ni mchezaji mzuri mwenye uwezo wa kunifanyia kazi ninayotaka.”
“Sina uhakika kama viongozi wangu wanataka kuwasajili, lakini mimi isingekuwa hii kanuni ya shirikisho hata ukiniletea wote hakuna shida, siwezi kumkataa mchezaji mzuri sababu ikiwa ni klabu anayotoka, nitamchukua mchezaji yeyote kutoka Yanga na hata Azam.” Mwanaspoti linajua kwamba Yanga wanafikiria kuachana na Hamis Kiiza ingawa na Okwi na mwenyewe yuko kwenye wakati mgumu.
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amesema hataki wachezaji wabinafsi kwenye kikosi chake na hababaishwi na majina makubwa hivyo atahitaji muda wa kuwatazama Okwi na Kiiza ili kuona uwezo wao uwanjani kabla ya kumtema mmoja.
“Nasubiri waje kwanza, wacheze ili niwaone wanavyocheza na uwezo wao kwa ujumla na baada ya hapo nitafanya maamuzi sahihi yatakayokuwa na mafanikio.
“Kwa kifupi sitaki mchezaji mbinafsi, mchezaji anayewaza nafsi yake pekee bali nataka mchezaji anayewaza mafanikio ya Yanga na anayejituma kuhakikisha timu inanyakua kombe kwani mchezaji anashinda mechi lakini timu ndiyo inayoshinda

laaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

TETESI ZA SOKA JUMAPILI

TETESI ZA SOKA JUMAPILI
West Ham wanataka kumsajili mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto'o, 33 ambaye aliondoka Chelsea msimu uliopita (Sun on Sunday), Inter Milan wanafikiria kumtoa Fredy Guarin, 28, kubadilishana na Javier Hernandez, 26, kutoka Manchester United (Sun on Sunday), Romelu Lukaku aliyecheza Everton kwa mkopo msimu uliopita, anataka uhamisho wa kudumu kwenda Goodison Park (Talksport), Arsenal wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Shakhtar Donetsk, Douglas Costa, 23 ambaye ameomba kuondoka Ukraine kwa sababu za matatizo ya kisiasa nchini humo (Caughtoffside), Atlètico Madrid wamefikia makubaliano ya kumsajili Antoine Griezmann, 23 kutoka Real Sociedad kwa pauni milioni 24 (AS), meneja wa. Manchester United bado ana nia ya kumsajili kiungo wa Roma Kevin Strootman, 24, licha ya mchezaji huyo kuwa majeruhi kutokana na kuumia goti (Sky Sports), Real Madrid wanapanga kumchukua Radamel Falcao, 28, kwa mkopo na uhamisho wa kudumu mwaka 2015 (AS), jaribio la Stoke City kumsajili Oussama Assaidi, 25, kutoka Liverpool kwa pauni milioni 7, huenda likashindikana kutokana na winga huyo kutaka mshahara mkubwa (Daily Express), mshambuliaji wa Lille Divock Origi, 19, anakaribia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 12.5 kwenda Liverpool (Sunday Mirror), Sami Khedira anataka mshahara wa pauni milioni 7.1 kwa mwaka ili kujiunga na Arsenal (La Sexta), Arsenal wanafikiria kupanda dau kumchukua kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin (Daily Star), Angel Di Maria anajiandaa kusaini mkataba wa miaka mitano siku chache zijazo na Paris St-Germain (Marca). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Adios!

 

pongezi za dhati kwa Msanii Lady Jay Dee kwa kuiwakilisha vyema nchi yetu kwa kutwaa tuzo ya msanii bora wa kike katika tuzo za AFRIMMA 2014 huko Marekani. vema sana

pongezi za dhati Msanii Diamond Platnumz kwa kuiwakilisha vyema nchi yetu kwa kutwaa tuzo mbili katika tuzo za AFRIMMA 2014 huko Marekani. Hongera Sana

Thursday, July 3, 2014

the.............................................................................mp3
Blogger Widgets