Showing posts with label Michezo na Burudani. Show all posts
Showing posts with label Michezo na Burudani. Show all posts
Friday, August 21, 2015
Uongozi wa Azam FC umesema hauna tatizo na uamuzi wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kumbadilisha mwamuzi wa mchezaji wa Ngao ya Jamii,
Jumamosi. Mchezo huo unawakutanisha Azam FC dhidi ya Yanga ambao
utarushwa moja kwa moja na runinga ya Azam TV, sasa utachezeshwa na
Martin Saanya. TFF imembadilisha Israel Nkongo ambaye ameelezwa kuwa na
matatizo ya misuli. Katibu wa Azam FC, Idrissa Nassor amesema wao
wanachotaka ni uchezeshaji wa kufuata sheria 17 za soka. “Kwa kweli
hatuna tatizo, kama sheria 17 za soka zitafuatwa sisi hatuna tatizo.
“Hiyo si kazi yetu, kikubwa ni maandalizi ambayo tumekuwa tukiendelea
kuyafanya,”
Sunday, July 27, 2014
MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA
MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA
Matokeo ya marathon wanaume:
1. Michael Shelley - Australia
2. Stephen Chmelamy - Kenya
3. Abraham Kiplimo - Uganda
4. M Mutai - Uganda
5. J Kelai - Kenya
6. E Ndema - Kenya
7. L Adams - Australia
8. P Kiplimo - Uganda
9. D Hawkins - Scotland
10. S Way - England
11. Fabiano Naasi - Tanzania
Kipa Ospina asajiliwa Arsenal http://wp.me/p2FUKJ-4VF
Kipa Ospina asajiliwa Arsenal
* Ferdinand aanza Queen Park Rangers
Wakati Arsenal wamekamilisha usajili wa golikipa wa Timu ya Taifa ya Colombia, David Ospina, Queen Park Rangers (QPR) wameanza kupata huduma za mabeki wa kati Rio Ferdinand na Steven Caulker huku Jose Mourinho akimvaa Luke Shaw.
Arsenal wamefanikisha usajili wa kipa ambaye aliruhusu mabao machache zaidi katika hatua za makundi kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil majuzi, taarifa hiyo ikiwa imetolewa na kocha wa klabu yake ya Nice, Claude Puel.
Ospina (25) amekuwa na klabu hiyo ya Ufaransa tangu 2008 na alisaidia nchi yake kufika hatua ya robo fainali na kocha Puel alisema Arsenal watafurahi kwani Ospina ni kipa mzuri sana.

Pasipo kuthibitisha usajili huo, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alijibu swali la waandishi wa habari kwa kusema aliamini kwamba kipa huyo alifanya vyema sana kwenye michuano ya Kombe la Dunia.
Wenger amepata kunukuliwa akisema kwamba kuna uwezekano wa Ospina kumpoka namba kabisa kipa namba moja wa Arsenal, Mpolishi Wojciech Szczesny. Ospina alicheza dakika zote za mechi zote za Colombia na nchi hiyo iliruhusu pia mabao machache zaidi miongoni mwa timu za Amerika Kusini wakati wa mechi za kufuzu.
Ospina ndiye alichukua mikoba ya Hugo Lloris aliposajiliwa na Tottenham Hotspur kutoka Lyon lakini kabla ya hapo alikuwa Nice.
MOURINHO ASEMA SHAW GHALI MNO
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ameendelea kuzungumzia masuala ya wachezaji wa timu nyingine, akiwashangaa Manchester United kumsajili beki wa kushoto wa Southampton ambaye ni ghali sana.
Mourinho amedai kwamba madai ya mshahara mkubwa ya Shaw yangeweza ‘kuiua’ Chelsea. Shaw alisajiliwa kwa pauni milioni 27 na amekuwa akiwaniwa na timu nyingi, ikiwa ni pamoja na Arsenal na Liverpool.
Mreno huyo amedai Shaw kulipwa pauni 100,000 kwa wiki ni kiasi kikubwa mno, lakini Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amedai kwamba atakaa faragha na Mourinho kuzungumzia suala hilo.
“Tukimlipa kijana mwenye umri wa miaka 19 kile tulichotakiwa kumlipa, basi kumsajili Luke Shaw kungetuua. Tungeua uthabiti wetu huku tukitakiwa kuzingatia uungwana katika matumizi ya fedha, sasa ukimlipa kijana mdogo kiasi hicho basi kesho yake wengine watakuvamia kutaka nyongeza,” akasema Mourinho.
Mourinho anajenga hoja kwamba si sahihi mchezaji mpya na mwenye umri mdogo kiasi hicho kulipwa kuliko wakongwe ambao wamechezea klabu mechi hadi 200, kuiletea mataji na sifa nyingi.
FERDINAND, CAULKER WAANZA KAZI QPR
Mabeki wapya wa kati wa Queen Park Rangers (QPR), Rio Ferdinand na Steven Caulker wameanza rasmi majukumu katika klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu baada ya kuwa imeshuka msimu uliopita.
Waingereza hao wawili walicheza dakika 45 kila mmoja katika mechi ya kirafiki nchini Ujerumani kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu ya England inayoanza mwezi ujao. Ferdinand alianza kufundishwa soka ya kulipwa na kocha wa sasa wa QPR, Harry Redknapp.
Katika hatua nyingine, QPR wameamua kumrejesha kipa wao, Julio Cesar (34) wa Brazil aliyekuwa ametolewa kwa mkopo katika klabu inayocheza Ligi ya Marekani ya Toronto FC. Kipa mwingine katika QPR ni Mwingereza, Robert Green.
Wakati huo huo, West Ham United wamepata pigo kubwa, baada ya mshambuliaji wao wa kutegemewa kuumia enka na hivyo atakuwa nje ya dimba kwa miezi karibu minne, ikimaanisha ataanza kucheza Novemba.
Loga amvizia Hamis Kiiza
UONGOZI wa Simba umegawanyika wapo ambao hawataki kusikia
usajili wa mchezaji yoyote kutoka Yanga lakini wapo mabosi watatu
huwaambii kitu kuhusu Emmanuel Okwi.
Kocha wa Simba,Zdravko Logarusic ‘Loga’ alisema;
“Nawajua hao wachezaji Okwi na Kiiza ni wachezaji wazuri niliwaona msimu
uliopita, sina pingamizi kama nitaletewa hapa, ninachotaka ni mchezaji
mzuri mwenye uwezo wa kunifanyia kazi ninayotaka.”
“Sina uhakika kama viongozi wangu wanataka
kuwasajili, lakini mimi isingekuwa hii kanuni ya shirikisho hata
ukiniletea wote hakuna shida, siwezi kumkataa mchezaji mzuri sababu
ikiwa ni klabu anayotoka, nitamchukua mchezaji yeyote kutoka Yanga na
hata Azam.” Mwanaspoti linajua kwamba Yanga wanafikiria kuachana na
Hamis Kiiza ingawa na Okwi na mwenyewe yuko kwenye wakati mgumu.
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amesema hataki
wachezaji wabinafsi kwenye kikosi chake na hababaishwi na majina makubwa
hivyo atahitaji muda wa kuwatazama Okwi na Kiiza ili kuona uwezo wao
uwanjani kabla ya kumtema mmoja.
“Nasubiri waje kwanza, wacheze ili niwaone
wanavyocheza na uwezo wao kwa ujumla na baada ya hapo nitafanya maamuzi
sahihi yatakayokuwa na mafanikio.
“Kwa kifupi sitaki mchezaji mbinafsi, mchezaji
anayewaza nafsi yake pekee bali nataka mchezaji anayewaza mafanikio ya
Yanga na anayejituma kuhakikisha timu inanyakua kombe kwani mchezaji
anashinda mechi lakini timu ndiyo inayoshinda
TETESI ZA SOKA JUMAPILI
TETESI ZA SOKA JUMAPILI
West Ham wanataka kumsajili mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto'o, 33 ambaye aliondoka Chelsea msimu uliopita (Sun on Sunday), Inter Milan wanafikiria kumtoa Fredy Guarin, 28, kubadilishana na Javier Hernandez, 26, kutoka Manchester United (Sun on Sunday), Romelu Lukaku aliyecheza Everton kwa mkopo msimu uliopita, anataka uhamisho wa kudumu kwenda Goodison Park (Talksport), Arsenal wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Shakhtar Donetsk, Douglas Costa, 23 ambaye ameomba kuondoka Ukraine kwa sababu za matatizo ya kisiasa nchini humo (Caughtoffside), Atlètico Madrid wamefikia makubaliano ya kumsajili Antoine Griezmann, 23 kutoka Real Sociedad kwa pauni milioni 24 (AS), meneja wa. Manchester United bado ana nia ya kumsajili kiungo wa Roma Kevin Strootman, 24, licha ya mchezaji huyo kuwa majeruhi kutokana na kuumia goti (Sky Sports), Real Madrid wanapanga kumchukua Radamel Falcao, 28, kwa mkopo na uhamisho wa kudumu mwaka 2015 (AS), jaribio la Stoke City kumsajili Oussama Assaidi, 25, kutoka Liverpool kwa pauni milioni 7, huenda likashindikana kutokana na winga huyo kutaka mshahara mkubwa (Daily Express), mshambuliaji wa Lille Divock Origi, 19, anakaribia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 12.5 kwenda Liverpool (Sunday Mirror), Sami Khedira anataka mshahara wa pauni milioni 7.1 kwa mwaka ili kujiunga na Arsenal (La Sexta), Arsenal wanafikiria kupanda dau kumchukua kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin (Daily Star), Angel Di Maria anajiandaa kusaini mkataba wa miaka mitano siku chache zijazo na Paris St-Germain (Marca). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Adios!

Saturday, March 8, 2014
Ommy Dimpoz ashoot video na muongozaji wa ‘Caro’ ya Wizkid, Azonto ya Fuse ODG na ‘Skelewu’ ya Davido.TAZAMA PICHA MBALIMBALI
Ommy Dimpoz ashoot video na muongozaji wa ‘Caro’ ya Wizkid, Azonto ya Fuse ODG na ‘Skelewu’ ya Davido.TAZAMA PICHA MBALIMBALI
Ommy Dimpoz anatarajia kuupeleka muziki wa Tanzania ‘next level’
baada ya wiki hii kushoot video ya wimbo wake mpya jijini London,
Uingereza.

Ommy akiwa na model atakayeonekana kwenye video hiyo

Ommy ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa ni mapema kutaja jina la wimbo huo lakini amedai ni moto wa kuotea mbali.

Ommy akiwa location ya video hiyo
Video hiyo imeongozwa na muongozaji wa video kutoka Nigeria anayeishi nchini Uingereza, Moe Musa. Muongozaji huyo ameongoza video za wasanii wengi wakubwa na nyimbo nyingi ni hits. Video hizo ni pamoja Azonto na Antenna za Fuse ODG, Skelewu ya Davido, Caro ya Starboy ft L.A.X na Davido, Ukwu ya Timaya na zingine nyingi.

Thursday, February 13, 2014
RONALDO AZIDI KUKIMBIZA, ASHIKA NAMBA MOJA KATIKA ORODHA YA WACHEZAJI NA WENZA WANAOVUTIA ZAIDI, ANGALIA 9 WALIOSALIA.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na mpenzi wake ambaye pia ni mwanamitindo, Irina Shayk, wamechaguliwa kuwa kapo yenye mvuto zaidi miongoni mwa wachezaji wa mpira wa miguu na wap#nzi wao, hii ikiwa ni mbele ya David na Victoria Beckham.
Ronaldo na patna wake walipata 18% ya kura zote kwenye utafiti uliofanywa na mtandao wa BetNegotiator.com.
Shuka chini upate listi kamili na picha zao....
Top 10 ya kapo zenye mvuto kwa wachezaji soka
1. Cristiano Ronaldo and Irina Shayk – 18 %
2. David Beckham and Victoria Beckham - 14 %
3. Lionel Messi and Antonella Roccuzzo – 11 %
4. Steven Gerrard and Alex Gerrard – 9 %
5. Gerard Pique and Shakira – 8 %
6. Frank Lampard and Christine Bleakley – 7 %
7. Iker Casillas and Sara Carbonero – 6 %
8. Wayne Bridge and Frankie Sandford – 5 %
9. Gareth Bale and Emma Rhys-Jones – 4 %
10. Peter Crouch and Abbey Clancy – 3 %
DC.
Friday, February 7, 2014
ETI HIZI NDO NYWELE ZA ASILI ZA NICK MINAJ, MCHEKI HAPA.
Monday, February 3, 2014
SNURA ALIA NA WABAYA WAKE, WANAOTAMANI AANGUKE.
STAA aliyeliteka soko la mduara kwa kibao chake cha Majanga, Snura Mushi amesema watu wenye chuki na yeye wamepanga njama za kumshusha kwenye chati kutokana na maendeleo yake.
Akipiga stori na paparazi wetu juzi, Snura alisema: “Nashangaa sana ninapofanya jambo zuri halafu watu wanaligeuza kuwa baya ili nichafuke jina na kunipunguzia mvuto kwa mashabiki wangu.”
Chanzo cha yote ni baada ya mwanadada huyo kupiga shoo kwenye Ukumbi wa Buliyaga, Temeke, Dar siku chache zilizopita, kundi la watu wasiojulikana walianza kueneza taarifa kuwa alifanya vibaya na mashabiki wakamtaka ashuke jukwaani jambo ambalo alisema halikuwa na ukweli wowote.
DR CHENI APANIA KUIRUDISHA KAOLE SANAA GROUP.
MWENYEKITI Msaidizi wa Bongo Movie Unity, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amesema amekumbuka na kutamani kurudisha Kundi la Sanaa ya Maigizo la Kaole ‘Kaole Sanaa Group’ liwe na nguvu kama zamani.
Dk. Cheni alisema japo kundi hilo limeonekana kupoteza mvuto wake wa awali, lakini anaamini wasanii wengi wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya filamu kwa sasa wametoka katika kundi hilo maarufu.
Hata hivyo, pamoja na kupotea kwa kundi hilo, Dk. Cheni anatamani sana kulirejesha kwenye ulingo wa sanaa na kwamba kuna mikakati anayoiandaa ili kukamilisha azimia hiyo.
“Naitamani Kaole ya zamani, nahisi kama kuna vionjo vinakosekana siku hizi. Wasanii wengi wenye majina makubwa kwa sasa wametoka kwenye kundi hilo, lakini nitajitahidi kulirudisha, naamini nitafanikiwa,” alisema Dk. Cheni.
BAADA YA KUJIINGIZA KIAINA NA SIASA, WANA BONGO MOVIES WAMTAKA STEVE NYERERE AJIUZULU.
Hali si shwari katika klabu ya wasanii wa filamu za Kibongo, Bongo Movie Unity ikidaiwa kuwa baadhi ya ‘memba’ wake wanashinikiza mwenyekiti wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ajiuzulu.
Habari zilizoifikia Stori Extra wikiendi iliyopita zilidai kuwa, baadhi ya wasanii wa klabu hiyo akiwemo mwenyekiti huyo walilamba mshiko kutoka kwa mwanasiasa mmoja wa CCM mkoani Mbeya ili wamfanyie kampeni katika uchaguzi ujao jambo ambalo wenzao walilipinga vikali kwa kuwa wao hawajihusishi na siasa bali wasanii na jamii.
Alipotafutwa Steve kujibu tuhuma hizo hakupatikana lakini katibu wake, William Mtitu alikiri kuwepo kwa ishu hiyo.
GPL.
Monday, January 27, 2014
MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA
Sudi Mohamed, 'MCD' (pichani, juu ) ambaye ni mpinga tumba maarufu nchini Tanzania amefariki dunia usiku huu akiwa Moshi ambako alikwenda kwa ajili ya matiabu zaidi yapata miezi mitatu iliyopita. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Meneja Hassani, MCD alipelekewa nauli ya kurudi jijini Dar esalaam leo ili arejee kesho lakini mauti yakamfika usiku mida ya saa tano na nusu. MCD amewahi kupiga katika bendi kadhaa za muziki wa dansi ikiwemo Mashujaa Band na African Stars ambako alirejea tena. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - ameen!
Saturday, January 25, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)