Wednesday, February 27, 2013

Steve Nyerere Apata Ajali kisha atupwa Rumande

-->
Nyota wa filamu za Kibongo nchini, Steve Mengele, maarufu kama Steve Nyere amekutwa na mkasa wa aina yake pale alipopata ajali jumatatu ya wiki iliyopita maeneo ya kijitonyama ambapo Steve akiwa ndani ya gari yake aina ya Toyota Verosa aliligonga gari lililokuwa limesimama ghafla mbele yake aina ya Toyota Fun Cargo na kulisababisha litumbikie mtaroni. Baada ya tukio kulitokea majibizano baina ya madereva hao ambapo walipofika askari kutuliza ghasia inasemekana kulitokea kupishana kauli kati ya askari na nyota huyo ndipo alipopigwa "Tanganyika jeki" na kupelekwa kituoni,

Thursday, February 21, 2013

Sista Aliyefumaniwa Atozwa Faini ya Laki Saba

MAHAKAMA ya Mwanzo mjini hapa, imemtia hatiani aliyekuwa mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani, kwa kufumaniwa na mume wa mtu na kuamriwa kumlipa fidia ya Sh 700,000 mlalamikaji.
Katika kesi ya msingi ya madai, mlalamikaji Asteria Mgabo alimtaka Sista Yasinta amlipe Sh milioni 3 baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa, Martin Msangawale (39) ambaye pia ni mkazi wa mjini hapa.
-->
Sista huyo ambaye ni daktari katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa, kwa sasa anaishi nje ya nyumba ya utawa eneo la Kantalamba.
Katika hati ya awali ya madai, inadaiwa mshitakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa na mumewe Msangawale wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Chipa iliyopo eneo la Katandala mjini hapa, Desemba 24 mwaka jana majira ya saa 7 usiku ikiwa ni siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas.
Akisoma hukumu hiyo juzi, hakimu wa mahakama hiyo, Jaffar Mkinga alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mlalamikaji ulikuwa mzito wenye kuondoa shaka zote kuwa mdaiwa alitenda kosa hilo tofauti na utetezi uliotolewa na mdai kuwa ulikuwa dhaifu.
Awali katika utetezi wake mdaiwa aliiambia mahakama hiyo kuwa kwanza alikuwa hajui kuwa Martin alikuwa mume wa mtu na kukiri mbele ya mahakama hiyo kuwa alimweleza kuwa hana mke hivyo alimwomba amuoe.
Lakini Hakimu Mkinga alipinga utetezi huo kwa sababu usiku huo wa mkesha wa Krismas mwaka jana, saa saba na robo usiku, mlalamikaji akiongozana na mwenyekiti wa mtaa wakiwa na mashahidi wengine watatu, walimkuta mdaiwa na Martin wakitoka katika moja ya vyumba katika nyumba ya kulala wageni ya Chipa, akasainishwa.

“Kama hukufahamu kuwa Martin alikuwa hana mke ilikuwaje ukakubali kusaini karatasi hiyo ya fumanizi iliyoandaliwa na mwenyekiti huyo?” alihoji hakimu, akamhukumu kulipa sh 700,000.


source: mpekuz

Mama aliyemtesa mtoto ahukumiwa

HATIMAYE haki imetendeka, hayo ni maneno waliyoyasema baadhi ya wakazi wa Mbeya waliohudhuria katika Mahakama ya Wilaya na kushuhudia Wilvina Mkandara (24) akihukumiwa kifungo cha maisha jela kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili ya kumtesa hadi kumsababishia ulemavu mtoto, Aneth Johannes (4) aliyekuwa akimlea.


--> Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa Jumatatu iliyopita na hakimu mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Gilbert Ndeuruo, wananchi walionekana kufurahi na wengi wakitaka japo kumgusa mfungwa huyo mpya lakini ulinzi wa polisi ulikuwa imara.
“Huyu mama angenyongwa tu,” alisikika akisema mama mmoja aliyeonesha kuwa na hasira na mfungwa huyo aliyekuwa amezungukwa na askari polisi.

Akisoma hukumu hiyo iliyozusha cherekochereko kutoka kwa baadhi ya wakazi hao wa Mbeya mahakamani hapo, Hakimu Ndeuruo alisema mshitakiwa amehukumiwa kutokana na kifungu cha 235 cha mwenendo wa makosa ya jinai cha mwaka 1985.

Akaongeza kuwa mahakama hiyo imeona mshtakiwa anastahili adhabu kutokana na mtuhumiwa huyo kama mzazi kushindwa kujali afya ya mtoto wakati alikuwa mama mlezi ikiwa ni pamoja na kumpeleka hospitali kwa wakati ili apatiwe matibabu.

Hakimu Ndeuruo amesema mahakama hiyo haikuridhishwa na ushahidi wa utetezi wa mtuhumiwa alioutoa mahakamani kuwa majeraha yaliyokutwa mwilini mwa mtoto Aneth yalitokana na kuugua tetekuwanga, jambo ambalo alisema si la kweli.

Aidha, mshtakiwa Wilvina alipotakiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu kabla ya kusomewa hukumu alisema: “Naiomba mahakama inipunguzie adhabu kwa kuwa mimi ni mjamzito pia sijui mwanangu niliyemzaa alipo kwani sina mawasiliano na familia yangu.”

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Ndauruo alisema amesikitishwa na kitendo cha mtuhumiwa huyo kutotaka kujua alipo mtoto aliyemkosea na badala yake kumjali wake. Mwanamke huyo alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Novemba 16, mwaka jana.
Blogger Widgets