Showing posts with label Habari za Kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Habari za Kimataifa. Show all posts

Thursday, February 13, 2014

PATA MUDA KUANGALIA PICHA ZA MWANAMKE MWENYE KIUNO CHEMBEMBA ZAIDI DUNIANI.


Mwanzoni nilikuwa natia shaka juu ya hili mpaka nilipokuja kuona kuwa naye yumo miongoni mwa watu kwenye kitabu maarufu cha kumbukumbu za Guinness world.

Cathie Jung ana miaka 77 na ndiye mwanamke mwenye kiuno chembamba zaidi Duniani. Hakika hii inashangaza kimtindo.

Cheki picha zaidi hapo chini...



lla unadhani hii ni hali ya kawaidia au ni ugonjwa...? DC.

Friday, February 7, 2014

HILI NDO VAZI LA HARUSI LILILOTENGENEZWA KWA C0ND0M


Vazi la harusi ambalo limetengenezwa kwa kutumia mipira ya kiume (C0nd0m) limewekwa kwenye jengo la maonyesho nchini Australia.

Vazi hilo limebuniwa kwa lengo la kuhamasisha watu kuelewa juu ya athali za magonjwa yatokanayo na kujamiiana, UKIMWI ikiwa ni moja wapo.

Na limewekwa kwenye Kituo cha Burudani cha Halmashauri ya Jiji la Shoalhaven lililopo nchini Australia.

Kituo cha Illawarra Shoalhaven cha eneo hilo kinachohusika na huduma za HIV na magonjwa yanayoendana nayo kimetengeneza vazi hilo la harusi lote likiwa na cond0m kwa lengo la kuhamasisha matumizi yake kama namna ya kujikinga na maambukizi.

Monday, February 3, 2014

SHERIA YA KUWANYONYESHA WATOTO KWA MIAKA MIWILI YAPISHWA HUKO UARABUNI.


Wanawake wa Umoja wa nchi za Kiarabu wanatakiwa kuwanyonyesha watoto zao kwa kipidi cha miaka miwili, sheria mpya ya kutetea haki za watoto ambayo imeanza kutumika rasmi mwezi huu imeeleza.

Sehemu ya sheria hiyo mpya, inawataka wamama kuwanyoyesha watoto zao kwa miaka miwili kamili au waume zao wataweza kuwashtaki kama watashindwa kufanya hivyo.
DC Blog.

Wednesday, January 29, 2014

MFANYA BIASHARA APIGWA RISASI 3 NA KUFA PAPO HAPO NDANI YA GARI LAKE.

Mwili wa marehemu Ahmed Bakhshuwein baada ya kupigwa risasi.
Mfanyabiashara, Ahmed Bakhshuwein ameuawa kwa kupigwa risasi tatu kichwani akiwa kwenye gari eneo la Malindi, Mombasa karibu na Al-R azaak Stores nchini Kenya.
CREDIT: Michuzi Issa.




BILIONEA WA KIKE "OPRAH WINFREY" ATIMIZA MIAKA 60 LEO.


MWIGIZAJI, mmiliki wa vyombo vya habari, mtangazaji, prodyuza kutoka nchini Marekani, Oprah Gail Winfrey leo ametimiza umri wa miaka 60. Oprah ambaye amejishindia tuzo mbalimbali kupitia kipindi chake cha 'The Oprah Winfrey Show' alizaliwa Januari 29, 1954 Mississipi nchini Marekani. Oprah ni bilionea namba moja ambaye ni Mmarekani mweusi wa karne ya 20.

Monday, January 27, 2014

BABA AMSHTAKI MWANAE KWA KUOA MWANAMKE MASKINI,ADAI ANAMHARIBIA SIFA,KWAO MWIKO KUOA WALALAHOI


Mwanamme mmoja nchini India amemshtaki mwanawe wa pekee wa kiume katika mahakama kwa kumharibia sifa, alipoamua kumuoa mwanamke wa tabaka la chini. 
Alisema kwamba kitendo hicho kimemharibia sifa na hadhi yake katika jamii.

Mzee Sidhnath Sharma mkazi wa Patna nchini India anataka alipwe rupia 10,000,000 (KSh13,638,900) na mwanawe Sushant Jasu, na anataka mahakama iamuru kwamba kijana huyo asitumie tena jina la familia.

Sharma, ambaye ni wakili kutoka ukoo wa familia ya watu wanaojiweza ya Bhumihar, alisema ndoa aliyofunga mwanawe mwishoni mwa mwaka jana ilivunja mwiko ambao umedumishwa kwa miaka 400, kwamba mtu wa familia ya hadhi ya juu hafai kumwoa wa walalahoi.

“Kwa miaka mingi, sheria hii imekubaliwa na kwamba ndoa ni lazima zipangwe na wazazi kwa sababu ya kuwa mtu amuoe wa hadhi yake. Lakini mwanangu pekee ameamua kumaliza utamaduni huu. Sio tu kwamba nimepigwa na butwa, bali pia kitendo chake kimetia doa hadhi yangi katika jamii,” aliambia shirika la Habari la Ufaransa, AFO nyumbani kwake mjini Danapur, viungani mwa jiji la Patna.

Mtindo huo wa kuwagawa watu katika makundi kulingana na hadhi zao, umerithiwa mno nchini India kiasi kwamba umekita mizizi hata miongoni mwa wasomi na watetezi wa haki za binadamu.

Cha kushangaza ni kwamba, unafuatwa hata katika jimbo la Bihar, mojawapo ya maeneo maskini zaidi na yenye idadi kubwa ya watu nchini India.

Itikadi hiyo ndiyo dira hasa ya maisha ya watu wengi wa India, na inaweza kuamua kuhusiana na masuala ya ndoa, elimu, ajira na umiliki wa ardhi, japokuwa sharia za nchi hiyo zinapiga marufuku kuwabagua watu kwa misingi ya hadhi zao.

Watu wanaokwenda kinyume na wazazi wao na kuamua kuoa nje ya matabaka yao, mara kwa mara wamekuwa wakiuawa, katika kinachotajwa kuwa 'mauaji ya kuhifadhi hadhi’ ili wanandoa wasiharibu heshima na sifa za wazazi wao. Sharma aliwasilisha keshi dhidi ya Jasu mwezi uliopita na mahakama mjini Danapur inatarajiwa kuanza kuisikiza kesi hizo mwezi huu.

Jasu, ambaye ni afisa mkusanyaji mapato katika jimbo la Gujarat, alimwoa mke huyo anayefanya kazi katika benki mjini Danapur mwezi Novemba mwaka jana. Sharma anasema iwapo mwanawe ataendelea kutumia jina la familia kwenye jina lake, ataomba alipwe rupia 10,000 kama ada ya hakimiliki, kila mara atakapotajwa au kusikika akiitwa na mtu.

“Nimeiomba mahakama imwagize anilipe kwa kuniumiza hisia zangu, kisaikolojia na pia kwa kuniharibia hadhi yangu katika jamii. Ninataka anilipe gharama yangu yote niliyopata kumfanya awe mtu aliye sasa,” akasema.


Jasu alikataa kuzungumza kuhusu kesi hiyo.

UNAKUMBUKA YULE MKALI WA "MARLBORO" AMEFARIKI DUNIA AKIWA NA MIKA 72.

Eric Lawson maarufu kwa jina la Marlboro enzi za uhai wake.
MWIGIZAJI wa Marekani, Eric Lawson maarufu kwa jina la Marlboro baada ya kutokea katika matangazo ya sigara miaka ya 1970 amefariki kwa ugonjwa wa mapafu akiwa na umri wa miaka 72.
Lawson alifariki Januari 10 mwaka huu akiwa nyumbani kwake San Luis Obispo kwa ugonjwa wa mapafu, kwa mujibu wa mkewe Susan Lawson.
Lawson aliyeanza kuvuta sigara akiwa na umri wa miaka 14, alionekana katika vipindi kadhaa vya TV vikiwemo, Baretta na The Streets of San Francisco ambapo baadaye alikodiwa kutangaza matangazo ya Marlboro kuanzia mwaka 1978 mpaka 1981 yaliyompatia umaarufu mkubwa.



Wakati wa uhai wake, Eric alicheza katika vipindi vilivyojizolea sifa vya Charlie's Angels, Dynasty na Baywatch.

Sunday, January 26, 2014

KUTANA NA KIJANA ANAEISHI KWA KULA MIFUKO YA PLASTIKI, AMEANZA TABIA HIYO TANGUA AKIWA NA MIAKA 7, SASA ANA MIAKA 23.


Oakland.Kijana mwenye umri wa miaka 23 amejikuta katika wakati mgumu, baada ya kuathiriwa na tabia ya kula mifuko na bidhaa za plastiki.
Kijana huyo, Robert kutoka huko Oakland, Tennessee nchini Marekani alianza tabia hiyo kama mzaha akiwa na umri wa miaka saba tu, ambapo alipendelea zaidi plastiki za rangi ya bluu ambazo kwa mtazamo wake alikuwa akiona rangi hiyo ina utamu.
Kadiri miaka ilivyozidi kuongezeka, tabia hiyo ilimwathiri na hata kujikuta akilazimika kutumia mbinu za ziada kuipata, ikibidi kwa kuiba kwenye maduka makubwa au kwenye maduka ya mitaani.
Si hivyo tu, mara nyingine huchukua hatua ya kuiba mifuko ambayo huhifadhiwa matunda kwa ajili ya maonyesho kwenye maduka na kuyamwaga kisha kutokomea na mifuko hiyo.
Tangu alipoanza tabia hiyo, imeelezwa kwamba tayari ameshatafuna zaidi ya mifuko 60,000 ya plastiki ambayo kwa wingi wake inaweza kujaza uwanja wa kuchezea mpira wa miguu.
Kwa mujibu wa maelezo yake, huanza siku yake kwa kula mfuko wa kwanza kama kifungua kinywa na hupendelea zaidi mifuko ya rangi ya bluu ambayo hutumiwa kufunga magazeti.
Alieleza kwamba muda mwingine hulazimika kuanza kurandaranda kwenye nyumba za jirani akitafuta mifuko hiyo ambayo wengi wa majirani huitupa ovyo baada ya kufungua na kuchukua magazeti yao ili kukidhi haja yake.
Robert anaamini kwamba mifuko yenye rangi nyingine tofauti na rangi ya bluu pia ina ladha tofauti, hivyo wakati wa majadiliano yake na kituo cha TLC katika kipindi chake cha Tabia Yangu ya Ajabu alisema anaona bluu ni tamu zaidi.
Mara nyingine hulazimika kukaa hadi siku moja na nusu bila kula chakula iwapo atapata dozi ya kutosha ya mifuko hiyo, ambapo baada ya kujisaidia hali yake hurejea kama kawaida na kuendelea na shughuli zake.
Kitendo hicho kimewashangaza wengi kwa kuwa hata baadhi ya majirani hawakuwahi kujua kwamba kwa miaka yote alikuwepo kijana ambaye alikuwa akiwasaidia kupunguza taka za mifuko ya plastiki majumbani kwao.
Hata hivyo, mchumba wake, Ashley alisema amekuwa akisumbuliwa sana na tabia hiyo ya Robert na amekuwa akijaribu kufanya kila juhudi ili aachane nayo kabla ya ndoa yao inayotarajiwa kufungwa miezi sita ijayo.
Not happy: Fiancee Ashley is concerned over his addiction and wants him to stop consuming so many
Jambo la kushangaza ni kwamba, japokuwa kitaalamu ulaji wa plastiki kwa binadamu husababisha kuziba kwa utumbo na kuharibu ini, vipimo alivyochukuliwa Robert vinaonyesha kwamba hana athari zozote katika maeneo hayo.
Katika mtiririko wa matukio yake, Ashley alisema aliudhika zaidi siku walipokwenda kutafuta keki kwa ajili ya harusi yao, ambapo Robert alipotakiwa kuonja alishindwa akisema kwamba ameshiba kupita kiasi kutokana na plastiki alizokula.
Muda mfupi baadaye alilalamika kwamba ana maumivu ya tumbo na baada ya kushauriwa kwa muda ndipo alipokubali kwenda kumwona daktari kwa ajili ya vipimo.
Check-up: Even though eating plastic can cause liver damage and intestinal blockages, Robert's tests come back OK but he is going to try and cut down
Japokuwa Ashley amefahamu kuathirika huko kwa mchumba wake tangu walopoanza uhusiano zaidi ya miaka miwili iliyopita, anasema aliona ni jambo linalohitaji ukaribu na msaada zaidi ili kumwepusha na tabia hiyo.
Kwa ajili ya upendo na map#nzi yake kwa Ashley, Robert kwa sasa amemwahidi mchumba wake huyo kwamba atafanya kila linalowezekana kuacha tabia hiyo ili kuwezesha ndoa yao iwe ya amani mara wakati utakapofika.
Mwananchi/Daily Mail.

Friday, January 24, 2014

ANGALIA MAKAMUZI YA PITBUL, JLO NA CLAUDIA WA BRAZIL KATIKA NYIMBO YA KOMBE LA DUNIA 2014


Ebwana shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kushirikiana na Sony Music wametangaza kwamba ‘We Are One’ ndio jina la wimbo wa kombe la dunia 2014 litakalochezwa Brazil ambapo mastaa watatu wa muziki walioteuliwa kuimba huo wimbo ni Pitbull, Jennifer Lopez pamoja na Mbrazil Claudia Leitte.
Single itaachiwa na Sony miezi michache ijayo na itatumika pia kwenye ufunguzi wa mashindano hayo Sao Paulo Brazil June 12 huku pia video yake ikifanyiwa kazi kwa sasa.
Hao hapo juu ni J.Lo na Pitbul, na hizi picha hapa chini ndio za huyu mrembo mwenyewe wa Kibrazil.


Thursday, January 23, 2014

PATA MUDA KUANGALIA PICHA ZA MJENGO WA RICK ROSS WENYE VYUMBA 109 HAPA, NI SHIDAAA!!!


Big Boss wa MayBach Music Group Rick Ross, amemwaga mamilioni ya dola kununua jumba la kifahari lenye vyumba 109 kwaajili ya makazi yake, ambayo kwa huku kwetu hiyo ni hotel kabisa tena kubwa tu.
Jumba hilo lililoko Atlanta, Georgia, Marekani hapo kabla lilikuwa likimilikiwa na bondia Evender Holyfield.
rick h-2
Mansion hiyo yenye ukubwa wa 54,000 square feet ina kila kitu unachoweza kutamani kuwa nacho kwenye nyumba, ikiwa ni pamoja na swimming pool kubwa, home movie theatre, uwanja wa basetball, na dinning room yenye uwezo wa kuchukua watu 100 kwa pamoja.
rick h-3
Haijawekwa wazi kiasi ambacho Rozay ametoa kununua mansion hiyo, lakini July,2012 Evender aliweka sokoni mjengo huo kwa dola milioni 14.
rick h-1

Inasemekana gharama za kuendesha mjengo huo haipungui dola milioni 1 kwa mwaka, pamoja na bill za umeme zinazofika $17,000.

rick h-4

MWANDISHI HUYU MAHIRI KUTOKA KENYA AJITANGAZA HADHARANI KWAMBA NI "SHOGA"


Hii inamfanya Binyavanga kuwa mmoja wa wafrika mashuhuri kujitokeza hadharani.
Matendo ya kimap#nzi kwa watu wa jinsia moja hayakubaliwi nchini Kenya, na nchi nyinginezo za Afrika.
Alifichua hali hii katika taarifa yake kupitia kwa mtandano wa kijamii wa Twitter iliyowiana na siku ya kuzaliwa kwake.Ana umri wa miaka 43.

Hii inakujia wakati ambapo kuna mjadala mkali nchini Kenya na katika baadhi ya mataifa ya Afrika kuhusiana na suala la haki za wap#nzi wa jinsia moja.

Hivi karibuni, Nigeria ilipitisha sheria ambayo inatoa adhabu kali kwa makundi ya watu wanaoshiriki map#nzi ya jinsia moja, ilhali Rais wa Uganda alikataa kuhalalisha mswada kama huo uliopitishwa bungeni.

Uamuzi wa Binyavanga kujitokeza hadharani umepokelewa kwa hisia mbali mbali nchini Kenya. Kunao waliompongeza ingawa baadhi wanahisi kuwa huenda jamii ikamnyanyapaa.

Binyavanga aliwahi kushinda tuzo la mwanadishi bora zaidi Afrika la Caine mwaka 2002.
Watu wanaoshiriki map#nzi ya jinsia moja nchini Kenya wanaweza kuadhibiwa kifungo cha miaka kumi jela ikiwa watapatikana na hatia.

Wednesday, January 22, 2014

PATA MUDA KUANGALIA SIMU MPYA ZA SAMSUNG S5, TOLEO JIPYA KABISA NI NOMA.


Angalia Picha zaidi ya mzigo mpya wa Samsung S5 Concept, ni noumah sana.





PICHA YA MZUNGU ALIYEKALIA KITI CHENYE TASWIRA YA MWANAMKE WA KIAFRICA YAZUA MTAFARUKU.


Russian Socialite ambae ni muhariri wa jarida la Garage magazine, Dasha Zhukova akiwa pia ni patner wa mmiliki wa club ya Chelsea Roman Abramovich, ameingia kwenye maporomoko ya matusi na maoni mengine mazito ya watu mbalimbali mtandaoni baada ya kusambaa kwa picha inayomuonyesha akiwa amekaa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa mfano wa Mwanamke wa Kiafrika.

Mwanamke huyu ambae anasema ana mapenzi na fashion pamoja na usanii wa vitu kama hivi amekosolewa na wengi ambapo baadhi ya Wanawake hata wenye ngozi kama ya Dasha, wamemkosoa huku wengine wakiuliza ‘bado tunafanya vitu hivi mpaka huu mwaka wa 2014?’

Kiti hiki kimedizainiwa na msanii raia wa Norway Bjarne Melgaard ambapo baada ya kupostiwa kwa picha hii kwenye mitandao akiwa anafanyiwa interview na tovuti ya Buro 24/7 , muda mfupi baadae waliitoa hii picha na kuomba radhi kwa kitendo hicho.

Sehemu ya maelezo yao ilisema ‘sio nia yetu kuendeleza au kufanya ubaguzi kwa binadamu yeyote’

KAMA ULIKUWA HAUJAWAHI KULIONA BASI HILI NDO TANGAZO ALILOFANYA MKE WA OBAMA.




Wiki iliyopita Miami Heat walitembelea Ikulu ya Marekani kusherehekea uchampion wao wa mwaka 2013 ambapo wakiwa hapohapo Ikulu waliungana na first lady kusupport kampeni ya let’s move kwenye tangazo la TV ili kusisitizia umuhimu wa kula vizuri, kula kwa afya na kunywa maji ili kuwa imara kama champion.
Tangazo hili la TV lililowekwa Youtube January 21 2014 linaihusu kampeni hii ya kuimarisha afya.

WATUHUMIWA WA WEST GATE WAPELEKWA ENEO LA TUKIO CHINI YA ULINZI MKALI



Ripota wangu wa nguvu Julius Chemitei kutoka Nairobi anaripoti kwamba Hakimu na pande husika dhidi ya washukiwa wa shambulio la Westgate wametembelea eneo la tukio kutekeleza amri iliyotolewa na hakimu mkuu Daniel Ojenja wiki iliyopita kabla ya kesi hiyo kuahirishwa.
Hakimu Daniel Ochenje alizungumza na waandishi kwenye hii ziara na kusema umuhimu wa ziara hiyo ni kuwezesha pande husika kupata taswira ya eneo hilo wakati Mashahidi wanapolihusisha eneo la tukio kwenye ushahidi wao Mahakamani.

Mawakili wa washukiwa wanaendelea kusimamia kwamba wateja wao hawana hatia yoyote na baada ya ziara hiyo walikua tayari kuendelea na kushirikiana na Mahakama wakati wakisubiri uamuzi kutolewa.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tarehe 27 & 28 January 2014 wakati upande wa mashtaka ukitarajiwa kuwasilisha mashahidi wengine 28 ambapo hata hivyo kumekuwa na malalamiko kutoka kwa mawakili wa upande wa Washukiwa kwamba viongozi wa mashtaka hawajawapa taarifa za polisi zilizoandikishwa na mashahidi.

Dwayne 'The Rock' Johnson Amnunulia Mfanyakazi wake wa ndani gari lenye thamani ya zaidi ya Milioni 65 za Kibongo.


Hii ni kuonesha jinsi gani staa huyu anathamini mchango wa watu mbali mbali wanaogusa maisha yake kwa namna moja ama nyingine, ameweza kuishi na mama huyu kwa miaka zaidi ya 10 na hii ndo suprize kwake.

Gari aina ya Ford Edge Limited Edition. 

Tuesday, January 21, 2014

OBAMA AITETEA BANGI, ASEMA BORA BANGI KULIKO POMBE


Rais wa Marekani Barack Obama anaamini kwamba bangi sio kitu hatari ukilinganisha na pombe na kwamba hicho ni kifungo kisichotenda haki kwa baadhi ya watu wengi wenye maisha ya chini waliopo kwenye majimbo mbalimbali nchini Marekani.

Kwenye mahojiano na New Yorker, Rais huyo ameeleza kwamba matumizi ya bangi sio kitu anachoweza kuwashauri watoto wake au mtu yeyoe kutumia, ila tahadhali kimekuwa ni tatizo kubwa ndani ya nchi hiyo.

"Kama ilivyowahi kuelezwa, nilikuwa navuta kama mtoto, na nikaona kuwa ni tabia mbaya na kinyume chake pia, haina tofauti na sigara ambayo niliivuta kama kijana mdogo mpaka nilipofika kuwa mtu mzima. Sidhani kama ni kitu hatari," Bwana Obama alisema.

Bangi imekuwa ni mwiko wa viongozi wengi wa kisiasa, na hata kuna kipindi ilizua matatizo kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Bill Clinton katika kipindi alichokuwa akigombea Urais mnamo mwaka 1992 pale ilipowekwa wazi alikuwa ni mvutaji katika kipindi alichokuwa akisoma nchini Uingereza, na alijibu kuwa hakuwahi na wala kujaribu kufanya hivyo'


Kwa upande mwengine Rais Obama yeye amekuwa mkweli zaidi, akikiri kuwa alikuwa akivuta na hata kutumia cocaine mnamo mwaka 1995 kwenye kumbukumbu za ndoto ya baba yake.

"Nadhani kwamba, kwenye hatua hii, maisha yangu ni kitabu cha wazi, kwa maneno na vitendo.


Wapiga kura wanaweza kufanya maamuzi ya kupotezea mambo ambayo niliwahi kuyafanya katika kipindi nilichokuwa kijana na kulingansha na kazi niliyoifanya toka kipindi kile." -


DC.

Monday, January 20, 2014

LETTIE MATABANE, MUIGIZAJI WA ISIDINGO ALIYEKUWA AIKIISHI NA VVU AFARIKI DUNIA.


Lesego Motsepe (Lettie Matabane), enzi za uhai wake
 
Mwaka 2011 Lettie aliwahi kujitangaza kuwa anaishi na Virusi vya Ukimwi
 

Aliyekuwa muigizaji maarufu katika Tamthilia ya Isidingo The Need ya Afrika Kusini, Lesego Motsepe maarufu zaidi kwa jina la Lettie Matabane, amefariki dunia nchini mwake Afrika Kusini mapema leo. 

Lettie, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa katika tamthilia hiyo kuanzia mwaka 1998 hadi 2008 alipoamua kuondoka, alikuwa akiishi na virusi vya Ukimwi kwa zaidi ya miaka 15. Mwaka 2011, aliwashitua mashabiki wake baada ya kuwatangazia kuwa yeye ni muathirika wa ukimwi. Hata hivyo wengi walimpongeza kwa kuwa na ujasiri wa kujitangaza hadharani, kwani kwa miaka mingi alikuwa akifanya kazi ya ubalozi wa mambo ya ukimwi. Aliianza kazi hiyo ya ubalozi kabla hajaathirika na hata alipoathirika hakushituka sana ingawa hali hiyo ilibadili maisha yake kabisa.
Tamthilia ya Isidingo ni miongoni mwa tamthilia kongwe na maarufu nchini Tanzania ambayo imekuwa ikioneshwa na televisheni ya ITV kwa zaidi ya miaka kumi sasa bila kuchosha watazamaji wake.
 
Mungu ailaze roho yake mahala pema - AMEEN!

WIVU WA KIMAPENZ WAMPELEKEA WAZIRI KUMPOTEZA MKEWE KWA KIFO CHA GHAFLA



Kimetokea kifo cha gafla cha mke wa waziri mmoja huko India baada ya utata kati yake na umma ambapo alimtuhumu  mume wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine ambapo kifo hicho kilikua cha ajabu na ghafla, hiyo ni kauli ya msemaji wa hospitali.

Kifo cha Sunanda Pushkar kilikuja siku chache tu baada ya vyombo vya habari huko India kutoa taarifa kwamba aliingia kwenye akaunti ya twitter ya mumewe Shashi Tharoor na kuandika ujumbe kwamba yeye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwandishi wa habari wa Pakistan.

Pushkar alikutwa amefariki kwenye chumba chake katika hoteli ya nyota tano huko New Delhi ambapo CNN-IBN ilitoa taarifa hiyo Ijumaa na mwili wake ulipelekwa kwenye kituo kiitwacho All India Institue of Medical Sciences kufanyiwa uchunguzi zaidi. 

Postmortem imekamilika, tunatuma sampuli kwa ajili ya toxicology uchambuzi wa utawala wa sumu,” Dk Sudhir Gupta, mkuu wa bodi ya autopsy katika hospitali, aliiambia CNN.
“Hii ni ripoti ya awali lakini tunaweza kusema kilikua kifo cha ghafla na sio cha kawaida kwakua kulikuwa na majeraha fulani kwenye mwili wake lakini hatuwezi kutoa maelezo ya kina kwa sasa ila ripoti ya mwisho itatolewa baada ya siku chache’Wanandoa hawa walikuwa wanakaa kwenya hoteli hiyo kwa siku chache kwa mujibu wa Abhinab Kumar, msaidizi wa Tharoor.
.
.
Mwandishi wa habari wa Pakistan aliyetuhumiwa na Pushkar , Mehr Tarar alikanusha hizi stori kwenye makala ya website moja ya New Delhi Television.
Siku ya Alhamisi, siku moja kabla ya kifo Pushkar, Tarar alisema ujumbe uliowekwa kwenye akaunti ya twitter ni “madai pori. ” na kwamba “tweets zake kwangu ni za ukichaa na nnachoweza kufanya ni kucheka tu, ” Tarar alisema.
Baada ya kifo cha Pushkar kutangazwa, Tarar alieleza kushtushwa na tukio hilo kwenye akaunti yake ya Twitter.
“Mimi nimeamka na kusoma taarifa hii, nimeshtushwa sana na tukio hilo. inasikitisha sana na inaleta huzuni sana nakosa cha kusema, Mungu ailaze mahali pema roho ya Sunanda”
.
.
Tarar alizungumza na CNN siku ya Ijumaa akielezea huzuni juu ya kifo Pushkar haya yakiwa maneno yake >>> “usiku mzima nimekosa usingizi, nimeshindwa kula hata kunywa maji, tulikua na ugomvi kwenye akaunti ya twitter baada ya hapo nasikia amekufa, sikuweza hata kupata nafasi ya kumpigia simu tuongee kumaliza tofauti zetu, alionekana mtu mwenye furaha muda wote na tabasamu zuri, lakini namna ambayo yeye alikufa imeniuma sana na itaniuma kwa muda mrefu.”
Tarar pia alisema madai ya Sunanda yalikuwa ya uongo. “Mimi nlikutana na waziri mara mbili tu katika maisha yangu yote na daima mbele ya watu wengine, tulikuwa tukiwasilaina hadi Juni na kisha alikuwa akinitumia barua pepe mara moja au mbili katika wiki. Pushkar, mfanyabiashara kutoka Dubaina Tharoor walifunga ndoa mwaka 2010.
Tharoor ni waziri wa rasilimali za binadamu na maendeleo India na ni mbunge pia, alikuwa waziri wa zamani wa mambo ya nje na wa zamani wa Umoja wa Mataifa chini ya katibu mkuu.

Blogger Widgets