Monday, January 20, 2014

WIVU WA KIMAPENZ WAMPELEKEA WAZIRI KUMPOTEZA MKEWE KWA KIFO CHA GHAFLA



Kimetokea kifo cha gafla cha mke wa waziri mmoja huko India baada ya utata kati yake na umma ambapo alimtuhumu  mume wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine ambapo kifo hicho kilikua cha ajabu na ghafla, hiyo ni kauli ya msemaji wa hospitali.

Kifo cha Sunanda Pushkar kilikuja siku chache tu baada ya vyombo vya habari huko India kutoa taarifa kwamba aliingia kwenye akaunti ya twitter ya mumewe Shashi Tharoor na kuandika ujumbe kwamba yeye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwandishi wa habari wa Pakistan.

Pushkar alikutwa amefariki kwenye chumba chake katika hoteli ya nyota tano huko New Delhi ambapo CNN-IBN ilitoa taarifa hiyo Ijumaa na mwili wake ulipelekwa kwenye kituo kiitwacho All India Institue of Medical Sciences kufanyiwa uchunguzi zaidi. 

Postmortem imekamilika, tunatuma sampuli kwa ajili ya toxicology uchambuzi wa utawala wa sumu,” Dk Sudhir Gupta, mkuu wa bodi ya autopsy katika hospitali, aliiambia CNN.
“Hii ni ripoti ya awali lakini tunaweza kusema kilikua kifo cha ghafla na sio cha kawaida kwakua kulikuwa na majeraha fulani kwenye mwili wake lakini hatuwezi kutoa maelezo ya kina kwa sasa ila ripoti ya mwisho itatolewa baada ya siku chache’Wanandoa hawa walikuwa wanakaa kwenya hoteli hiyo kwa siku chache kwa mujibu wa Abhinab Kumar, msaidizi wa Tharoor.
.
.
Mwandishi wa habari wa Pakistan aliyetuhumiwa na Pushkar , Mehr Tarar alikanusha hizi stori kwenye makala ya website moja ya New Delhi Television.
Siku ya Alhamisi, siku moja kabla ya kifo Pushkar, Tarar alisema ujumbe uliowekwa kwenye akaunti ya twitter ni “madai pori. ” na kwamba “tweets zake kwangu ni za ukichaa na nnachoweza kufanya ni kucheka tu, ” Tarar alisema.
Baada ya kifo cha Pushkar kutangazwa, Tarar alieleza kushtushwa na tukio hilo kwenye akaunti yake ya Twitter.
“Mimi nimeamka na kusoma taarifa hii, nimeshtushwa sana na tukio hilo. inasikitisha sana na inaleta huzuni sana nakosa cha kusema, Mungu ailaze mahali pema roho ya Sunanda”
.
.
Tarar alizungumza na CNN siku ya Ijumaa akielezea huzuni juu ya kifo Pushkar haya yakiwa maneno yake >>> “usiku mzima nimekosa usingizi, nimeshindwa kula hata kunywa maji, tulikua na ugomvi kwenye akaunti ya twitter baada ya hapo nasikia amekufa, sikuweza hata kupata nafasi ya kumpigia simu tuongee kumaliza tofauti zetu, alionekana mtu mwenye furaha muda wote na tabasamu zuri, lakini namna ambayo yeye alikufa imeniuma sana na itaniuma kwa muda mrefu.”
Tarar pia alisema madai ya Sunanda yalikuwa ya uongo. “Mimi nlikutana na waziri mara mbili tu katika maisha yangu yote na daima mbele ya watu wengine, tulikuwa tukiwasilaina hadi Juni na kisha alikuwa akinitumia barua pepe mara moja au mbili katika wiki. Pushkar, mfanyabiashara kutoka Dubaina Tharoor walifunga ndoa mwaka 2010.
Tharoor ni waziri wa rasilimali za binadamu na maendeleo India na ni mbunge pia, alikuwa waziri wa zamani wa mambo ya nje na wa zamani wa Umoja wa Mataifa chini ya katibu mkuu.

No comments:

Post a Comment

Blogger Widgets