Showing posts with label Uswazi.. Show all posts
Showing posts with label Uswazi.. Show all posts
Friday, August 2, 2013
Majanga ONA Majanga!!!! Mpaka Kieleweke Leo!!
Kama kawaida, Cheka Upate Afya, leo nakuletea Picha niliyoipata katika mtandao wa kijamii huku ikiwa Commented ya Kwamba Mpare Utamjua Tu!!!! Walionaje hili?
Monday, July 29, 2013
Ajali!!!!Akuta Panya Ndani ya Wali Rost Nyama Aliouagiza.
Hali ya Sitofahamu imejitokeza katika Mgahawa mmoja huko Africa Magharibu baada ya Mteja aliyekuwa ameagiza Wali Rost nyama ya kukaanga kukutana na "KAPANYA" Kadogo kameiva ndani ya chakula alichokiagiza.
Mteja huyo alikumbwa na bumbuwazi na hasa ukizingatia alikuwa ameshakula chakula hicho kwa zaidi ya Asilimia 90.
Sunday, July 28, 2013
Za mwizi, 40.!!! Kibaka achezea kipigo huko Kawe, ni baada ya kuruka geti.
Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja inadaiwa alikutwa akiruka geti kuingia ndani kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
Source:GPL
Saturday, July 27, 2013
Ndege Abadilika na kuwa Binadamu baada ya Kudondoka Chini Mchana Kweupee!!!
-->
Walioshuhudia tukio hilo wamesema ilikuwa kama sinema au mchezo wa kuigiza kwani walikuwa ndege watatu wanapaa angani, ghafla mmoja akadondoka na akatumbukia katika ki mfereji cha maji, hapo ndipo alipojaza watu kwani alibadilika kutoka kuwa ndege na kuwa binadamu.
Ilibidi polisi waingilie kati na kumchukua mwanamke huyo ambaye alijieleza ya kwamba anatokea Ikole na Ni Mkazi wa Jimbo hilo la Ekiti Huko Nigeria.
Polisi hawaamini uchawi, sijui suala la mwanamke huyo watalishughulikiaje!!!!

Angalia Jinsi Bongo Movie Wanavyopondwa na Kutathminiwa hapa
UTAJUAJE NI BONGO MOVIE?
1.Jini akifika barabarani
anaangalia
pande zote ndo avuke barabara.
2. Matajiri majumba yao yana askari
badala ya electric
fence &
gates.
3.Trailer inachukua
dakika 40.
4.Part2 ya movie ukiiona
mwanzo unajua part1
ilikuwaje.
5.Madem wanaamka wanamake ups
usoni na hereni kabisa.
6.Wakifika hotelini imezoeleka ni juice
inaagizwa au wine
isiyofunguliwa.
7.Nusu saa mtu anatembea,anafanya
mazoezi,anakimbizwa au ananunua vitu.
8.Wimbo wa malavidavi
unaimba
mpaka unaisha.
9.Mtu yupo
village,life gumu ana wave kichwani.
10.Wote wanaouwawa kwa risasi
hupigwa kifuani au
tumboni sio kichwani.
11.Jambazi
lazima awe anavaa miwani nyeusi,koti
kubwa na mvuta sigara mwenye sauti
nene na sura ya kutisha
12Tajiri anakuja kumpenda maskini.
13. Jina La Movie La Kingereza, Ndani
Mazungumzo Ni Kwa Kiswahili.
14.Editor Roy Kijusi, Camera man
Inosenti Kijusi, graphic designer Roy
Kijusi, Location manager Happy Kijusi,
Mavazi Suzy Kijusi.
15.Movie inapart1 na part2,lakn
ukiangalia unagundua ni disc.1 na disc.2
16.movie inaitwa life is harder (mfano)
afu kwenye kava watu wameweka
mapozi ya mamodo na warembo."
Hii nimeikuta face book, huku ikipata Comment zaidi ya 30, Likes ndo Usiseme, Vipi ndugu Msomaji wangu, unalionaje hili?
Nabii Achezea Kipacho, Baada ya Kutuhumiwa kuwa na Uhusiano na Mume wa Mtu, Mchungaji.
-->
Stori:Gladness Mallya na Sanchawa
MWANAMKE anayejulikana kwa jina la Nabii Juliana wa Kanisa la Miracle Assemblies of God, amepigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kuingilia ndoa ya Mchungaji Richard Kiondo.
Tukio hilo la aina yake ambalo lilikusanya umati wa watu, lilitokea hivi karibuni maeneo ya Ukonga Mazizini, jijini Dar ambapo nabii huyo alipigwa hadi kuchaniwa nguo.
Akielezea mkasa huo, mtoto wa mchungaji wa kanisa hilo, Christina Kiondo alisema baba yake alikuwa akishirikiana kwa huduma ya kanisa na Nabii Juliana lakini katika ushirika huo anaamini wawili hao walikuwa na uhusiano usiofaa.
Alisema kisa cha nabii huyo kupigwa, hivi karibuni mwanamke mmoja alikwenda nyumbani kwa Mchungaji Kiondo na kuwaeleza watoto hao kwamba anamdai baba yao shilingi 40,000, kitu ambacho kiliwashitua sana kwa kuwa baba yao anaishi kwa nabii na pia hawakujua fedha hizo alikopa kwa ajili ya familia gani.
Mtoto mkubwa wa mchungaji huyo, alimtuma mdogo wake nyumbani kwa nabii huyo kwa lengo la kwenda kumuita baba yao ili aje kuzungumza na mwanamke huyo.
Ilidaiwa kuwa, mtoto huyo alipofika alikutana na nabii na kumwambia amemfuata baba yake lakini alimfukuza.
“Baadaye alikuja hapa nyumbani na kuanzisha varangati kitu ambacho hakikukubalika kwa majirani kwani tangu siku nyingi wanajua uhusiano wake wa baba.
“Majirani walitoka kwa wingi baada ya kumsikia nabii akitufanyia fujo, walianza kumshushia kipigo mpaka alipokuja kuokolewa na mjumbe wa eneo hili na kupelekwa polisi,” alisema Christina.
Akizungumza na mapaparazi wetu, mjumbe wa eneo hilo Joseph John ‘Mzee Kasheshe’ alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Kwa upande wake, mke halali wa mchungaji huo ambaye yuko Mbagala kwa matibabu, alisema alizipata taarifa za nabii huyo kupigwa.
Aliongeza kuwa tangu zamani mama huyo alikuwa akienda na mumewe nyumbani hapo akidhani kuwa wote ni watumishi wa Mungu hivyo hakuwahi kuwatilia shaka hadi baadaye sana aliponyetishiwa na watu.
Kufuatia kipigo hicho, Nabii Juliana alipofika polisi alitoa malalamiko yake na kufungua kesi yenye kumbukumbu: MAZ/RB/2246/2013 KUHARIBU MALI.
![]() |
| Nabii Juliana Aliyechezea Kichapo |

Mwanafunzi Ashikiwa Uchawi, Akutwa na zana kibao za uchawi huku akiwa na Nguo ya Ndani Tu!!!
Stori:Gladness Mallya na Haruni Sanchawa
AMINI usiamini, duniani kuna uchawi! Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Pasco (21) ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Samaritan iliyopo wilayani Rorya mkoani Mara amekutwa getini kwa kaka’ke, Edward Raphael akiwa amefungwa kamba na matunguri.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Pasco alikuwa amefungwa kamba mikononi na miguuni huku akiwa na nguo ya ndani pekee.
Habari zilieleza kuwa pia kijana huyo alikuwa amepakwa unga na kuandikwa maandishi ya Kiarabu mwilini huku kiunoni akiwa na shanga, hali iliyowashangaza wengi.
Akizungumza na wanahabari wetu juu ya tukio hilo, kaka wa kijana huyo alisema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili, wiki mbili zilizopita ambapo aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zake lakini alipofungua geti alishangaa kumuona mtu akiwa amelala akiwa hajitambui.
Alisema baada ya tukio hilo, alirudi ndani haraka na kumwita mpangaji wake ili akashuhudie alichokiona.
Mazagazaga aliyo kutwa nayo
Alisimulia kuwa baada ya mpangaji huyo kuamka, waliamua kwenda polisi lakini wakiwa huko, mkewe aliamua kwenda kumchunguza mtu huyo kwa makini usoni ambapo aligundua kuwa ni shemeji yake, jambo ambalo lilizidi kuwachanganya watu.Alisema aliporudi alikuta umati mkubwa wa watu umemzunguka Pasco.
Kaka mtu alisema kuwa alitimba na askari ambao walimfungua kamba na safari ya kuelekea kituo cha polisi ikaanza lakini wakiwa njiani, kijana huyo alikuwa akiongea maneno ya ajabu kama vile mtu mwenye majini.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Nyumba Kumi, Shina la Mube, Joseph Paja alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema naye alikuwa miongoni mwa mashuhuda.
Alisema kuwa alipofika, alikuta kijana huyo aliyewahi kuishi mtaani hapo kwa kipindi kirefu akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hali ambayo ilimshangaza kila mtu.
Mchungaji wa Kanisa la Church of World, Steven Paul ambaye naye alishuhudia tukio hilo, alisema kuwa baada ya ndugu kuamua kumpeleka polisi aliambatana nao hadi kituoni lakini walipofika, askari walimtema kwa kigezo kuwa hakuwa na kesi ya kufunguliwa, wakashauri apelekwe hospitali.
Ilielezwa kuwa zoezi la kumpeleka hospitali lilifanyika lakini walipofika huko, madaktari walimkataa kwa kigezo kuwa hawakuona ugonjwa wowote, jambo lililosababisha hofu kutanda.
Akizungumza na waandishi wetu, mchungaji huyo alisema kutokana na kote huko kushindikana, aliamua kumchukua kijana huyo na kuishi naye nyumbani kwake kwa lengo la kumfanyia maombi.
Baada ya kumchukua, alianza dozi ya maombezi ya nguvu ambapo hivi sasa anaendelea vizuri.
Katika mahojiano na waandishi wetu, Pasco alisema hajui kilichotokea hadi akajikuta amefika Dar, tena getini kwa kaka yake akiwa uchi.
Alisimulia kuwa siku hiyo, alienda benki kutuma ada ya shule na baada ya hapo, alirudi nyumbani kwa bibi yake na kumkuta akiandaa ugali ambapo alikula kidogo kwani alikuwa akihisi maumivu makali ya kichwa.
Baada ya kushindwa kula vizuri, bibi yake alimtaka ale chungwa ambapo alichukua moja na kwenda nalo chumbani, akachukua panga kisha kulikata vipande viwili lakini alipoanza kula, kabla ya kumaliza kipande kimoja alihisi usingizi mzito ambapo alikuja kushtukia akiwa sehemu tofauti yaani getini kwa kaka yake akiwa amezingirwa na watu kibao.
Alieleza kuwa kutokana na kusumbuliwa na mauzauza ya kichawi ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kaka yake amhamishie Rorya mkoani Mara ambako alienda kuanza kidato cha pili wakati huku Dar alikuwa ameshafika kidato cha nne.
Chanzo: GPL
Friday, July 26, 2013
Tathmini ya Vikao Vya Zabuni Serikalini na Taasisi Mbalimbali, Mtazamo wa Kipanya.
--> Kama Picha Inavyoonesha, ni hali ya kuashiria jinsi gani mambo yalivyo siku hizi katika Vikao vingi vya Zabuni Aidha katika Halmashauri zetu au Taasisi Mbali mbali, Tutafika Tu.!!
Image Credit: Kipanya.
Image Credit: Kipanya.
"UFUSKAA" Angalia Madanguro yalivyogunduliwa, Wanawake wanajiuza Hadharani.
ILE Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ chini ya Global Publishers ipo kazini! Safari hii imekutana na tukio la aina yake baada ya kumnasa kikongwe mmoja anayedaiwa kumiliki idadi kubwa ya madanguro katika uwanja wake na kuwapangisha makahaba katika eneo maarufu kwa jina la Kijiji cha Makahaba.
Awali kachero wa OFM alipokea ujumbe mfupi ulioelezea ufuska unaofanywa na mabinti ambao hupewa eneo na kujenga vibanda kisha kujiuza kwa bei chee katika kijiji hicho maeneo ya Kigamboni jijini Dar.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, eneo hilo linalofanyiwa ufuska huo linamilikiwa na kikongwe aliyejitambulisha kwa jina la mzee Matutu akidaiwa kuendesha maisha kwa biashara hiyo ya madanguro.
Baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuwa ni kweli jambo hilo linafanyika eneo hilo, OFM ililivamia ikiwa na mjumbe wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina la Abbas na kujionea madanguro yaliyojengwa kwa mstari ambapo milango yake iliachwa wazi huku ndani wakionekana mabinti wakiwa wamejilaza kihasarahasara wakiwatega wateja wanaopita katika mtaa huo.
Madanguro hayo ambayo kwa hesabu ni takriban kumi na nane, yamejengwa kwa aina yake ambapo mengi kati ya hayo yana ukubwa wa kutosha kuingia kitanda kidogo pekee.
“Sina kazi nyingine ya kuniingizia kipato zaidi ya hii ya wasichana licha ya kwamba sijawaruhusu wafanye biashara hiyo. Fedha hiyo ndiyo inanisaidia kwa mahitaji yangu,” alisema kwa tabu mzee Matutu huku akimtaja msimamizi wa madanguro hayo kuwa ni mpwa wake.
Alipoulizwa hatua waliyoichukua kwa mmiliki wa madanguro hayo ambaye ni mzee Matutu, kiongozi huyo alibakia kusikitika asijue hatua gani ya kumchukulia mzee huyo ambaye hata wakimpeleka kwenye vyombo vya sheria anahisi itakuwa ni uonevu kwa kuwa hana msaada mwingine wa kifedha zaidi ya fedha kutoka kwa mabinti hao.
SOURCE: GPL
Sunday, July 21, 2013
Saturday, July 20, 2013
Patricia, 45 lakini bado anajiachia, mwendo wa Bikin na Swim Suit tu!!!
Huyo ndo Patricia Krentcil, 45, akila bata ufukweni baada ya kumaliza mwezi mmoja katika Rehab kutokana na matatizo ya kulewa kupita kiasi, Kwa kupitia picha hizi utakubaliana na usemi wa waswahili:-
"Ng'ombe Hazeeki Maini"

"Ng'ombe Hazeeki Maini"
UMAARUFU WA WASANII WENGI WA KIKE UNATOKANA NA SKENDO ZA PICHA CHAFU
NCHI za wenzetu staa kupiga picha za utupu si kitu kigeni lakini Tanzania sheria na maadili ya Mtanzania hayaruhusu kufanya hivyo.
Pamoja na sheria kutoruhusu, wasanii wetu hasa wa kike wamekuwa wakihaha usiku na mchana kuusaka umaarufu wa kujulikana kwa jamii kwa njia za panya,....
Wengi wao wamepoteza sifa za uwajibikaji na badala yake wamejikita katika Skendo chafu ili jamii iwajue...
Hali hii imewafanya wasanii wengi wa kike wawe na umaarufu wa skendo chafu....
Friday, July 19, 2013
Video ya CCTV yamuonesha JINI/MZIMU ukikatisha na Kupotelea kusikojulikana!!!
Video hiyo iligunduliwa na Mwangalizi wa Eneo hilo ambapo wakati yupo katika TV akiangalia Camera zake, ghafla aliona kama kitu kimepita katika moja ya camera za mlango wa mbele kikielekea nyuma, akaamua kutoka nje ili kufuatilia, cha kushangaza ni kwamba kila upande alioenda hakufanikiwa kuona kitu na ndipo alipoamua kurudi ndani na kui download sehemu ya video katika camera hiyo na hicho ndicho alichokiona.
Angalia Video Hiyo hapa:-
-->
Hatimaye "MATONYA" wa England Warudishwa Kwao Romania
![]() |
| Safari Imeiva baada ya kuvamiwa Alfajiri |
![]() |
| Makazi yao hata kwa Mtogole kuna nafuu |
![]() |
| Waliokubali kuondoka, na mifuko ya Ki Nigeria kama uswazini kwetu |
Asubuhi ya Leo kundi la Askari Polisi walifika katika eneo hilo na kuwaeleza ya kwamba kwa hiari yao waondoke kwao na ndege ipo ya bure au wanaotaka kubaki basi wataenda jela. Katika Umati huo wote, ni watano tu waliokuwa na kibali ya kuishi na kufanya kazi nchini humo.
Haya sasa" Nani Kasema Ulaya Hakuna Omba Omba?"
Maajabu!!! Mbuzi azaliwa akiwa na "Vichwa" Viwili!!
Kuanzia Saa 10 Alfajiri zilisikika kelele za Maumivu kutoka kwa mbuzi jike ambaye alikuwa anajifungua, Kelele zilikuwa kubwa mno kuashiria maumivu makali alikuwa anayapata kiumbe huyo, palipozidi kupambazuka ilibidi majirani waende kushuhudia kulikoni kwa mbuzi kuwa na kelele kiasi kile, na ndipo walipojionea maajabu baada ya mbuzi jike huyo kujifungua watoto watatu, wawili kati ya hao wakiwa ni wa kawaida kabisa na mmoja akiwa na vichwa viwili.
Hayo ndio yaliyojiri Alhamisi ya jana tarehe 18 July 2013 Huku katika Jimbo la Irolini Kwara, Nigeria. Hata hivyo mbuzi huyo alizaliwa na vichwa viwili alifariki saa chache baadae.
Tuesday, July 16, 2013
Monday, July 8, 2013
Uwoya yamkuta, Aambulia Matusi ya Nguoni Baada ya Kumfananisha Diamond na Michael Jackson
-->
Wiki iliyopita Muigazaji wa Filamu Inchini, Mwanadada Irine Uwoya aliandika katika Ukurasa wa Istagram ya kwamba msanii wa Bongo Fleva, Diamond ndiye wa pekee ambaye anaweza kumrithi mkali wa Pop Mareheme Michael jackson kwa Jinsi msanii huyo alivyojuu kwa sasa. Maneno hayo ya mtazamo wake yaliwakera baadhi ya mashabiki na kuanza kumporomoshea matusi ya nguo kwa mtazamo wake huo, wengine walihoji huku wakimtukana, iweje amananishe aliyekufa na aliye hai au sababu Diamond aliku...!!! Ndo mambo ya Wabongo hayo.

Mganga achezea kichapo baada ya kula njama za Kuua.
Sangoma Mmoja amecheze kichapo cha mbwa mwizi kutoka kwa Raia wenye hasira baada ya kugundulika ya kwamba alikula njama za kumuua binadamu mwingine na ndio alikuwa katika maandalizi. Nusura yake ilipatika baada ya Jeshi la Polisi Kutokea Eneo la Tukio Na Mpaka sasa bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Subscribe to:
Posts (Atom)