-->
Siku ya juzi maeneo ya mwenge jamaa mmoja mwenye mwili mkubwa alifanya tukio la ajabu pale alipompokonya Askari wa Usalama Barabarani Ufunguo wake wa gari na kumnyonga mkono huku akijijua kufanya hivyo ni kosa kisheria na kamera za kituo cha ITV zilikuwa zikimwonesha. Taarifa zinamnukuu Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Kinondoni akisema ya kwamba jamaa huyo amekamatwa na yupo kituo cha polisi Cha Salander Bridge akisubiri kufikishwa mahakamani.
Uamuzi huo ummfanya Raisi wa Gambia Yahya Jammeh kuonekana ana sera kali zaidi ya zile za Iran. Amesema ya kwamba Nchi yake ina misingi ya maadili na imani hivyo hawawezi kuvumilia tabia za kishenzi zikiendelea nchini humo. mwezi wa pili mwaka huu raisi huyo aliwafanya wenye tabia kama hiyo kukimbia nchi jirani na kuomba hifadhi pale alipowafunga wanandoa wawili wa jinsia moja.