Saturday, August 3, 2013

Angalia Jinsi Demu wa Angelo Alivyo Mzuri, Kwanini anababaika na Beverly?


Wadau wamewezamkuzipata picha za Mpenzi waMshiriki wa BBA The Chase kutoka South Africa Angelo Collins, pamoja na baadhi ya Tweet zake kuhusiana na Mapenzi yao, Kilichowaacha midomo wazi ni uzuri wa binti huyo ukifananisha na Mwanamke aliyemvagaa Kijana huyo, Beverly Osu Kutoka Nchini Nigeria.

Angalia Picha hapo chini Kisha useme mwenyewe.





 

CANDY MISSCOCA

 




 

VS 
Beverly



David Beckham Aingia Katika Filamu Baada ya Kustaafu Mpira



Aliyekuwa Mchezaji wa PSV Kabla ya Kustaafu, David Beckham ameonesha nia ya kuingia katika Uigizaji wa Filamu. Ingawa Mwenyewe hajatoa maamuzi ya mwisho rasmi,Becks anatarajiwa kuleta msisimuko na hasa pale atakapokuwa akiigiza Tamthiliya za Kipelezi na Kijasusi kama za James Bond.

New career path: David, who proved his one screen presence in the short film, could be set to star in his first proper acting role
Miongoni mwa spicha katika filamu ambayo Becks amewahi kuigiza kwa kipande kifupi mno.

Kuna Testesi za nyota huyo kuigiza kama Starring katika Filamu inayokwenda kwa jina la "Kick-Ass" ambapo mkali Samuel L. Jackson anatarajia kumpa Kampani akiigiza kama Adui Mkuu.
Moving on: David played his last game for PSG back in May as he retired form the sport
Mechi ya Mwisho ya Beckham Kucheza kabala ya Kustaafu May 2013.

"VIDEO" Jinsi Askari wa Marekani wanavyowapekua Raia Sehemu za Siri.

-->
Askari wa Texas DPS Trooper wamefunguliwa Mashtaka ya Udhalilishaji dhidi ya Raia kutokana na vitendo vya Upekuzi  Usiokuwa wa kimaadili wanapokuwa kazini.Angalia Video Hizo Mbili Tofauti ujionee mwenyewe jinsi hali ilivyokuwa ikiwakuta wahanga wa matukio hayo.





Serikali na Madawa ya Kulevya!!!

Unakubaliana na Mawazo haya ya Kipanya Kuhusu Madawa ya Kulevya Na Taifa Letu ?

Image Credit: Kipanya.

Gumzo kuhusu Sakata la Mzee Majuto Kuoa kwa Siri Dar!!!!

-->


Chande Abdallah na Haruni Sanchawa
AMINI usiamini, kuna taarifa kwamba gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’ almaarufu mzee Majuto amefunga ndoa ya siri ndani ya Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Tukio hilo limetokea Julai 8, mwaka huu pande za Mbagala Zakhem jijini Dar ambapo mzee Majuto alifunga ndoa na msichana mbichi aitwaye Rehema Omary.
Mzee Majuto aliambatana na wasanii wenzake Suleiman Barafu aliyekuwa mpambe wake na mwingine aliyefahamika kwa jina la utani kama mama Sharon.
Baada ya waandishi wetu kupata taarifa kuhusu tukio hilo, waliwahi kutia timu Mbagala, nyumbani kwa binti huyo.
Baada ya kufika, waandishi wetu walibaini kuwa ni kweli kulikuwa na shamrashamra za ndoa ambayo ilikuwa ikifanyika kwa siri huku watu wakizuiliwa kupiga picha.
Muda mfupi baadaye, gari aina ya Toyota Noah (namba za usajili tunazo) lililowabeba mzee Majuto na wapambe wake liliwasili.
Muoaji akaongozana na wakwe na mashehe kwenda Msikiti wa Aqswa uliopo jirani ambapo ndoa hiyo ilifungwa kisha wakarudi nyumbani ambako cherekochereko ziliendelea.
Paparazi wetu alifanikiwa kujipenyeza na kuonekana kama mmoja wa ndugu na kushuhudia mzee Majuto akikabidhiwa mkewe.
Baada ya robo saa, mzee Majuto na mkewe walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuingia kwenye gari hilo aina ya Noah.
Paparazi wetu alipojaribu ‘kufotoa’ picha kadhaa, alisababisha kuzuka kwa  kizaazaa kwa wanandugu waliomlazimisha kuzifuta picha hizo ambapo alitii.
Baada ya tukio hilo, waandishi wetu walijaribu kuzungumza na mzee Majuto kwa simu lakini kazi haikuwa nyepesi kwani simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
Alilipopigiwa simu mpambe wa bwana harusi, Barafu, alisema hana la kusema na kusisitiza atafutwe mzee Majuto.
Mwandishi wetu alirudi Mbagala kwa mama wa biharusi ambaye alikuwa mkali na kusema kuwa atafutwe mzee Majuto.
Siku hiyohiyo mzee Majuto alipokea simu na kuulizwa kama ni kweli amefunga ndoa na msichana aitwaye Rehema.
Katika hali ya kushangaza, mzee Majuto alicheka sana na kudai kwamba utafiti wake umekakilika. Alipohojiwa ni utafiti gani alisema:
“Nilikuwa nafanya utafiti wa kutaka kuigiza filamu ya ndoa ya siri ndiyo maana nikaenda kule Mbagala lakini sasa nimeamini kwamba hakuna ndoa ya siri,” alisema mzee huyo huku akikwepa kukubali.
Habari zinasema kwamba mzee Majuto anakwepa kukubali kwamba amefunga ndoa kwa kumhofia mkewe wa kwanza ambaye amemuacha jijini Tanga.

Source: GPL

Uhusiano wa Justin Bieber na Selena Gomez ni Kitandani tu!!


Hay yamedhihirishwa na Bibie Gomez baada ya kubwana na maswali ya waandishi wa habari waliokuwa wakimuhoji vipi anaweza kumwacha Justine Bieber Anatoka kwenda Night Clubs Peke yake na Kutombana kama wapenzi wengine wafanyavyo? Alijibu:-

“I’ve known him for a really long time and we enjoy each other’s company every now and then,” said Gomez. “But I’m definitely single and enjoying being that.”
“Enjoy each other’s company every now and then,” 

Akaulizwa Tena?

 Why don’t you just admit to your fans that you and the Biebs are bed buddies! See ya later" Selena.

Rais Kikwete Amvaa Kagame, Asisitiza kuhusu Umuhimu wa Amani kwa Mataifa yote.


Dar es Salaam: Kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Kikwete amemtolea uvivu Rais wa Rwanda, Paul Kagame kutokana na kitendo chake cha kumtolea lugha za matusi baada ya kumshauri kukaa meza moja na vikundi vya waasi wa nchi yake (FDLR), huku akimtaka kuacha kukuza mgogoro usiokuwepo.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo kwa Rwanda takribani miezi miwili iliyopita wakati akizungumza katika kikao cha Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika mapema mwaka huu, mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambao ulikuwa ukijadili suala la amani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Ukanda wa Maziwa Makuu.
Ushauri huo pia uliwagusa Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Joseph Kabila (DRC), ambao aliwataka kufanya mazungumzo na waasi wanaopingana na Serikali zao. Akizungumza katika hotuba yake ya kila mwezi Rais Kikwete alisema: “Ushauri ule niliutoa kwa nia njema kabisa, kwani bado naamini kuwa kama jambo linaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo njia hiyo ni vyema itumike,”
“Isitoshe, ushauri ule niliutoa pia kwa Serikali ya Congo , Serikali ya Uganda. Katika mkutano ule Rais Museveni wa Uganda aliunga mkono kauli yangu. Rais Kagame hakusema chochote pale mkutanoni. Baada ya kurudi nyumbani ndipo tukaanza kuyasikia maneno tuliyoyasikia na tunayoendelea kuyasikia.”
Alisisitiza, “Kwa upande wangu sijasema lolote kuhusu Rwanda pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli yanayotoka kwenye vinywa vya viongozi wa Rwanda dhidi yangu. Siyo kwamba siambiwi yanayosemwa au sijui kusema au sina la kusema, la hasha, sijafanya hivyo kwa sababu sioni faida yake.”
Rais Kagame alitoa lugha zisizostahili dhidi ya Rais Kikwete katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi ya maofisa 45 wa jeshi lake Julai mwaka huu, ambapo alisema ushauri wa kufanya mazungumzo na waasi wa FDLR ni ujinga na haupo katika historia ya Wanyarwanda.
“Nilinyamaza kimya kwa sababu sikupenda kusikiliza ushauri kuhusu FDLR, kwa sababu nafikiri ni upuuzi ulioambatana na ujinga. Hatuwezi kuacha maisha yetu kama Wanyarwanda tunavyoishi sasa. Ushauri wa Kikwete ni sawa na kucheza na makaburi ya watu wengi ambao ni ndugu zetu,” alisema Kagame.
Katika hotuba ya jana Rais Kikwete alisema uhusiano wa Tanzania na Rwanda unapitia katika wakati mgumu na mtikisiko, baada ya yeye kutoa ushauri kwa Serikali ya Rwanda kuzungumza na mahasimu wao na kwamba hilo linadhihirika katika kauli zinazotolewa na viongozi wa Rwanda.
“Napenda kuwahakikishia Watanzania wenzangu na ndugu zetu wa Rwanda kuwa mimi, Serikali ninayoiongoza na wananchi wa Tanzania ,tunapenda kuwa na uhusiano mzuri na ushirikiano wa karibu na Rwanda kama ilivyo kwa nchi zote jirani” alisema Rais Kikwete.
Alisema nchi hizo ni jirani na kila moja inamuhitaji mwenzake, hivyo lazima ziwe na uhusiano mwema na ushirikiano mzuri.
“Nasisitiza kuwa mimi na Serikali ninayoiongoza tutakuwa wa mwisho kufanya kitendo au vitendo vibaya dhidi ya Rwanda au nchi yoyote jirani au yoyote duniani. Hatuna sababu ya kufanya hivyo, kwani ni mambo ambayo hayana tija wala masilahi kwetu” alisema.
Alisema nchi hizo mbili zimekuwa zikijihusisha na mambo ya kukuza na kujenga ujirani mwema, kusisitiza kwamba hiyo ni moja ya nguzo kuu ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania.
Chanzo:- Mwananchi
Blogger Widgets