Wednesday, January 1, 2014

Ajiua Baada ya Kuachwa na "SUGAR MUMY"




Kijana wa miaka 22, Michael Jaja, mkazi wa Tema huko Ghana ameamua kuyamaliza maisha yake matamu na kujiua kufuatiwa kuachwa solemba na Sugar Mumy wake wa miaka 48.

Jaja ambaye alikuwa alifikia uamuzi huo baada ya Jimama hilo kumtema na kumweleza ya kwamba raha zote zimefikia ukingoni kufuatia ujio wa mwanaume wa Jimama hilo aliyekuwa nje ya nchi(Ulaya).

Mbali na hayo ilimpasa kuhama katika mjengo wa Sugar mamy huyo na kurudisha gari alilokuwa akitembelea, Michael ambaye alilewa maisha ya anasa mbali na safari za mara kwa mara za Dubai na China alishindwa kuukubali ukweli ya kwamba atarudi katika maisha ya msoto tena.

Alitishia kujiua mbele ya mwanamke huyu ambapo alitaka kunywa tindikali na akawahiwa na mwanamke huyo tukio lililopelekea mwanamke huyo kumwagikiwa kidogo na Tindikali Hiyo.

Hili ni Fundisho na Tahadhari kwa vijana wengine ambao wanapenda maisha ya dezo.


Sheria ya Kuwatoza Faini Wateja wa Makahaba Yapitishwa, Ole wako ukamatwe




Mnamo siku ya Jumatano watunga sheria nchini Ufaransa walipitisha muswada ambao utawafanya wateja wa makahaba kutozwa faini kuanzia kiasi cha €1 500.

Sheria ya kupinga ukahaba ilipitishwa na mkutano mkuu ambapo Manaibu 268 wakipiga kura ya kukubali, 138 walipinga na 79 hawakupiga.

Sheria hiyo ambayo kwa sasa inahitaji kukubaliwa na Bunge la nchi hiyo, imekuja mara baada ya kupitishwa nchini Sweden ambapo kwa sasa inatumika ambapo wateja wa makahaba hutozwa faini kwenye nchi hiyo katika kile kinachoonekana kutaka kuitokomeza taaluma hiyo kongwe.

WAZIRI WA FEDHA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR. WILLIAM MGIMWA AMEFARIKI DUNIA


Waziri wa Fedha, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Iringa, William Mgimwa amefariki dunia leo akiwa hospitali ya Mediclinic Kloff, Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa!

Marehemu Mgimwa alizaliwa Januari 20, 1950 na amefariki akiwa na umri wa miaka 63.

Alipata Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) na Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam.

Alisoma Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Fedha (MBA) katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.

NI MASAA 48 YA MATESO KWA JACK CLIFF, DADA MTU ALIMUONYA LAKINI HAKUSIKIA.


HABARI ya kufungia mwaka 2013 na kufungua pazia la mwaka mpya wa 2014 ni madai ya mwanamitindo kiwango Bongo, Jacqueline Patrick kukamatwa katika  Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akiwa na mzigo wa madawa ya kulevya aina ya heroin lakini Risasi Mchanganyiko linaangaza mapya zaidi juu ya sakata hilo.
Mwanamitindo Jacqueline Patrick.
Macho na masikio ya Wabongo wengi kwa sasa ni juu ya mwenendo wa madai hayo, wakati gazeti hili likiendelea kupekenyua limenasa mpya kuwa, Jack yupo kwenye mateso makali kutoka kwa askari wapelelezi nchini humo wanaotaka kujua mtandao unaomuunganisha katika mchezo huo.
SAUTI KUTOKA CHINA
Chanzo chetu makini kilichopo China ambacho kinapiga kitabu kilieleza kuwa, katika kufuatilia ishu hiyo, juzi Jumatatu, Desemba 30, 2013, alikutana na kizingiti cha kushindwa kuonana na Jack katika mahabusu aliyowekwa kwa maelezo kwamba, uchunguzi bado unaendelea.
Dawa za kulevya zilizokutwa tumboni mwa Jack.
Raia huyo wa Tanzania aliyedai ana ukaribu na Jack, kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini, alisema mengi kuhusiana na mateso anayopata mrembo huyo hivi sasa.
“Ni kweli Jack amekamatwa hapa Macau. Hilo halina ubishi kabisa. Sheria za huku zinatofautiana kati ya jimbo na jimbo. Nilifika mahabusu aliko kwa lengo la kutaka kumwona lakini nilikataliwa. Nimeambiwa hawezi kuonana na mtu yeyote hadi Machi, mwakani (mwaka huu). Bado wanaendelea na uchunguzi kwanza.
Jack akiwa na mwenzake.
“Unajua wanajaribu kufichaficha mambo ili polisi waweze kufanya upelelezi wao vizuri lakini nimepenyezewa taarifa kuwa ataingizwa chumba cha mateso ili abanwe na kutaja mtandao wake. Wanajua yeye wameshamkamata, lakini wanataka kufahamu mzigo alitumwa na nani, ameutoa nchi gani na unakwenda nchi gani?
“Lengo la kufanya hivyo ni kukomesha mtandao mzima wa madawa ya kulevya. Si ajabu akawa kwenye mateso kwa kipindi chote hicho kama hatakuwa mkweli lakini kwa sasa ataingizwa kwenye kikosi cha kwanza.
Jack akiwa chini ya ulinzi.
“Hapo atakalishwa kwenye chumba cha mateso kwa siku mbili mfululizo (akimaanisha saa 48). Ni mateso makali sana. Wataalam wanajua wanafanyaje ili mtuhumiwa aweze kuzungumza ukweli kwa muda mfupi. Sasa hapo ikishindikana ndipo anaweza kuhamishiwa kwenye kikosi kingine,” alipasha mtoa habari wetu na kuongeza:
“Ni kama huko Bongo tu. Unaposikia chumba cha mateso ya wapelelezi maana yake shughuli yake siyo ndogo. Mimi namuonea huruma sana Jack, lakini najiuliza, hivi ni kwa nini huwa hawajifunzi kupitia wenzao?
“Si juzi tu wengine (Agnes Gerald ‘Masogange’ na Melisa Edward) wamekamatwa kwa madawa hayohayo na walisota kwa muda mrefu? Kwa nini hawasikii jamani? Namuhurumia sana kwakweli.”

KUMBE DADA YAKE ALIMUONYA
Habari kutoka kwa mtu wa karibu na dada wa Jack zinasema kuwa, wakati akitaka kusafiri akitokea Bongo, alimweleza dada yake juu ya mpango wake huo, akamuonya lakini modo huyo alikataa.
“Alimfuata dada yake na kumweleza mchongo mzima kuwa alitaka kwenda na mzigo China, dada yake akamwambia aachane na hizo biashara, akakataa. Jack alifikia hatua akamwambia dada yake kuwa hana mtoto, hana mume wala ndugu anayemtegea kwa hiyo yupo tayari kwa lolote kwani hakuwa na cha kupoteza.
“Kama angemsikiliza dada yake (jina linahifadhiwa) haya yote yasingemkuta na asingeingia kwenye mateso ya namna hii,” alisema mtoa habari wetu huku akiendelea kusisitiza jina lake lisionekane mahali popote kwenye ukurasa huu.
ABEBESHWA MZIGO, ALIPWA MALIPO YA AWALI
Ilizidi kusemekana kuwa, alipokaribia kuondoka Bongo, Jack alimwambia dada yake kwamba anakwenda kambini (kituo cha kuingiza mzigo tumboni) ambapo aliporejea kwa dada’ake alimuonesha dola za Kimarekani 21,000 (zaidi ya shilingi milioni 33) ambazo ni malipo ya awali huku akimwambia alishabebeshwa nusu ya mzigo.
Hata hivyo, habari zinasema Jack alimwambia dada yake huyo kuwa hakuwa akijisikia kusafiri lakini kwa kuwa anatafuta maisha aliamua kuondoka baada ya mzigo kukamilika wote siku iliyofuata.
INA MAANISHA NINI?
Kwa mujibu wa maelezo hayo, Jack aliondoka na unga hapahapa Bongo kwenda Thailand kupitia Nairobi, Kenya na baadaye Macau, China ambako alinaswa.
MASTAA WAFUNGUKA
Watu wamekuwa na mitazamo tofauti kulingana na ishu hiyo lakini Risasi Mchanganyiko lilipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya mastaa wa Bongo ambao wameeleza maoni yao kuhusiana na sakata hilo la Jack.



Katika mahojiano na waandishi wetu, tulitaka kusikia kutoka kwao namna wanavyolinganisha tabia ya kujihusisha na biashara za kusafirisha madawa ya kulevya na vitendo vya umalaya ambapo wametoa maoni tofauti.

JACQUELINE WOLPER:
“Mh! Mwenzangu, bora uwe na mabuzi (wanaume wenye mkwanja) 40 kuliko kufanya biashara ya madawa ya kulevya. Nawaomba mastaa wenzangu wasikubali kubebeshwa madawa kwa kudanganywa eti na dola 30,000, kamwe haiwezi kubadili mfumo wa maisha yako.”

REHEMA CHALAMILA ‘RAY C’:
 “Madawa ya kulevya hayakubaliki, yalinitenda sana haya madude! Kabisa tulinde vizazi vijavyo kwa kupiga vita madawa ya kulevya. Fanya yote lakini siyo madawa ya kulevya.”

SHAMSA FORD:
 “Nasema hivi, bora umalaya japo pia si mzuri kuliko kudili na biashara ya madawa ya kulevya. Nawaomba waachane na vitu hivyo kwani vinatumaliza kisanii... lakini nasisitiza kutulia na bwana mmoja ni vizuri sana kuliko kurukaruka.”

JOKATE MWEGELO:
 “Hakuna aliye mkamilifu lakini kama kitu ni kiovu ni kiovu tu hata kama mimi na wewe tunakifanya, kimsingi hakuna bora na anayesema kuna ubora basi hajitambui. Vyote vinadhalilisha utu na thamani ya mwanamke. Mwili si wa kuchezewa.”

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’:
“Tukitumia majina yetu vizuri, hakuna atakayejihusisha na yote hayo... tujitume kufanya kazi, umalaya unaweza kuwa bora kuliko kufanya biashara ya madawa ya kulevya kama utabanwa kuchagua maovu hayo. Maisha ya Ughaibuni yatatumaliza kwani tunaiga kwa kukurupuka bila kuelewa.”

TUMETOKEA HAPA
Jack anatuhumiwa kukamatwa na madawa ya kulevya Desemba 19, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Macau, China akitokea jijini Bangkok, Thailand akiwa safarini kwenda Guangzhou nchini China.
Ilielezwa kuwa unga aliokutwa nao una uzito wa kilo 1.1  ndani ya kete 57 huku thamani yake ikitajwa kuwa ni  zaidi ya shilingi milioni 223.
Bado yupo mikononi mwa polisi wa China wakati upelelezi wa awali ukiendelea ambao utafikia tamati Machi, mwaka huu kabla ya kuingia hatua inayofuata.
GPL

ANGALIZ PICHA 15 ZA MAKAMUZI YA SNURA KATIKA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA



Snura Mushi na kundi lake wakifanya makamuzi katika usiku wa mwaka mpya 2014 ndani ya Dar Live.…
Snura Mushi na kundi lake wakifanya makamuzi katika usiku wa mwaka mpya 2014 ndani ya Dar Live.
Snura akisema na mashabiki wake.
Wanenguaji wa Snura wakiwa kazini.

Snura na kundi lake wakizidi kupagawisha mashabiki wa Dar Live.
GPL

MKE ATOWEKA KIMIUJIZA, USHIRIKINA WATAJWA



Katika hali inayotafsiriwa kuwa ni imani za kishirikina, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Merry Patrick  au Mama Jack, mkazi wa Magole B Ilala jijini Dar es Salaam, ametoweka kimiujiza nyumbani kwake usiku wa manane wiki iliyopita.
Merry Patrick  au Mama Jack aliyetoweka kimiujiza
Chacha Muhochi, mume wa mwanamke huyo, aliliambia gazeti hili kuwa siku ya tukio, saa tisa usiku akiwa nje ya nyumba akilinda mifugo yake, aLimwacha mkewe amelala ndani, ghafla alisikia sauti ya mtoto wake wa mwisho akilia, hali iliyomfanya akimbilie ndani kutazama kilichotokea.
Baada ya kuingia ndani, alishangaa kutomuona mkewe kitandani kwani mtoto alikuwa peke yake. Alipojaribu kuchunguza, mlangoni mwa nyumba yake, aliona damu. Aliingia katika vyumba vyake vyote pasipo kumuona mkewe huyo, ambaye pia alikuwa ni mwanakwaya wa SDA.
“Sikujua nini kilimkuta mke wangu, nilihangaika kila kona sikumuona, nikaona niende kwa mjumbe na kutoa taarifa polisi, hadi ninavyozungumza na wewe bado hajaonekana,” alisema Chacha na kuonesha hati ya Polisi (RB) STK/RB/23241/2013.
Lakini katika hali ya kushangaza, baadhi ya majirani na waimba kwaya wenzake, wanadai mwanamke huyo huwa anaonekana nyakati za usiku na kwamba simu yake ikipigwa inaita bila kupokelewa, lakini baadaye hutuma ujumbe usioeleweka.
Mmoja wa waimba kwaya ambaye pia ni jirani na mama Jack, alisema wamekuwa wakikesha katika kufanya maombi kila siku, lakini wamekuwa wakishangazwa na ujumbe wanaopata wanapojaribu kupiga simu ambayo huwa haipokelewi.
“Tuache kwanza, kwa sasa ana majukumu, yuko bize, ila mchawi wenu hataki akae hapa, anaweza kuja muda wowote, yuko bomba kinoma,”  huu ni mmoja wa ujumbe unaotajwa kuandikwa kupitia simu ya mwanamke huyo anayedaiwa kutoweka kimiujiza.
Mwanakwaya mmoja alidai siku moja wakiwa katika maombezi, ujumbe mwingine kutoka simu ya mwenzao huyo uliingia katika simu ya wanamaombi hao na uliosomeka hivi; “Wachawi wakubwa mkiongozwa na huyo aliyejuu, ng’ombe wakubwa nyie, pigeni magoti chini.”



Mjumbe wa shina namba saba Bi. Fatuma Juma alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la aina yake ambalo limewatia hofu kubwa wakazi wa eneo hilo.

Inapendeza: Mapacha wa Kike na Wa Kiume Waoana Siku Moja.


Tukio hilo la kuvutia limetokea huko pande za Delta State ambapo Mapacha wa Kiume, Chinonso A. Okueza na Chuzor A. Okueze walifunga ndoa na wasichana mapacha, Folaweni Taiwo Okuninyi na Febisola Okuninyi mnamo tarehe 30 November 2013. Kila la a kheri kwao, angalia picha zaidi hapa chini.

 
Blogger Widgets