Saturday, February 1, 2014

BABA AMUAUA MWANAE WA MIEZI 6 KWA KUMPIGA NA CHUPA YA BIA KICHWANI.

Masikini wa Mungu! Baba aliyetajwa jina moja la Shaban (25), mkazi wa Kimara-Suka, Dar anadaiwa kuhusika katika mauaji ya mtoto wake asiye na hatia, Salma Shaban (miezi sita) kwa kumpiga na chupa ya bia kichwani na kusababisha mshipa mkubwa wa damu kukatika kichwani.
Mtoto aliyeuwawa na Baba yake, Shaban.
Akilisimulia Risasi Jumamosi mkasa huo wa kuumiza moyo, mama mzazi wa mtoto huyo, Matlida Amon alieleza kuwa tukio hilo lilijiri maeneo hayo hivi karibuni majira ya 5:00 asubuhi.
Mama huyo alimtaja kwa machungu mzazi mwenzake huyo kuhusika na tukio hilo.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Matlida Amon.
Alisema kuwa mumewe huyo wa ndoa alimuomba aende kumchajia simu barabarani ambapo alimuacha mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka 13 na mtoto akiwa anacheza kitandani.
Alisimulia kuwa aliporudi nyumbani alishangaa kumkuta mdogo wake akilia nje ya nyumba yao.
Matlida alisema kuwa alipomuuliza mdogo wake kwa nini alikuwa akiangua kilio, akamwambia kwamba shemeji yake alikuwa akimwambia kuwa anataka kufanya naye mapenzi.
Baba wa mtoto Shaban (25), mkazi wa Kimara-Suka.
Alisema mdogo wake alimwambia kuwa alimsukumiza kitandani akitaka kumbaka ndipo akapiga kelele na kufanikiwa kumchomoka na kukimbilia nje.
Mama wa mtoto huyo aliendelea kusimulia kwamba alipoingia ndani alianza kumlaani mumewe huyo kwa kitendo alichotaka kukifanya kwa mdogo wake ambapo aliishia kuomba msamaha lakini alimwambia ni bora amuombe mdogo wake (shemeji) na siyo yeye.
Matilda alisema kuwa baada ya kumwambia hivyo, yeye alianza kukusanya nguo za mdogo wake ampe ili aende nyumbani kwao ndipo mumewe huyo alipochukua kisu alichokiweka pembeni ya godoro na kutaka kumchoma nacho yeye.
Hata hivyo, Mungu mkubwa kwani Matilda alisema kuwa alifanikiwa kukidaka na kwa vile kilikuwa kibovu mwanaume alibaki na mpini yeye akabaki na kisu bila mpini.
Alisema alikitupa kisu hicho kupitia dirishani ambapo alipogeuka mumewe, alimzibua kibao kikali usoni kisha akachukua chupa ya bia iliyokuwa tupu ndani na kwenda moja kwa moja kwa mtoto aliyekuwa akicheza kitandani na kumpiga nayo kichwani huku akisema: “Bora tukose wote.”
Matilda aliendelea kusimulia huku akilia kuwa baada ya kufanya kitendo hicho baba huyo alikimbia huku yeye akimkimbilia mtoto aliyekuwa akitapatapa kitandani.
Dakika chache baadaye mtoto alizimia hivyo baadhi ya majirani walimkimbiza katika Hospitali ya Boch iliyopo Kimara-Suka, Dar ambapo alipatiwa huduma ya kwanza kisha wakampiga X-Ray na kugundua kuna mshipa mkubwa wa fahamu kichwani ulikuwa umekatika.
Baada ya hapo alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar. Alipofikishwa aliingizwa kwenye chumba cha upasuaji ili kuokoa maisha yake lakini ilishindikana kwani alifariki dunia.



Baada ya kupata taarifa hizo, ndugu pamoja na mama wa mtoto huyo walikwenda katika Kituo cha Polisi cha Mbezi Kwayusuf na kuandikisha taarifa kisha wakapatiwa jalada la kesi namba KMR/RB/1017/2014 na KMR /735/2014- MAUAJI ambapo mtuhumiwa anasakwa na polisi ili kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
GPL.

Friday, January 31, 2014

tufanye kazi kwa maendeleo ya taifa letu

BABU MPENDA TOTOZ, AFUMWA UCH** WA MNYAMA NA KADENTI CHA SHULE, GUEST HOUSE.


YELEUUUWI! Ile tabia ya wazee ya kupenda dogodogo imemtokea puani mzee aliyetajwa kwa jina moja la mzee Omari, ni Ijumaa pekee lenye ubavu wa kuripoti sinema hiyo ya bure.
AIBU YA MWAKA: Babu akifunika uso wake baada ya kunaswa na denti gesti.
Mzee huyo alinaswa laivu akiwa gesti na denti wa shule moja ya sekondari jijini Dar (jina la denti na shule vinahifadhiwa kimaadili).
Tukio hilo la aibu lilijiri juzikati kwenye gesti moja iliyopo maeneo ya Kawe, Dar na kusababisha timbwili zito.
TAARIFA MEZANI KWA OFM
Hivi karibuni, kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, kilipokea lalamiko kutoka kwa mzazi wa denti huyo ambaye alieleza juu ya mabadiliko ya mwanaye kitabia na kushuka kitaaluma kutokana na kusumbuliwa na ‘mbaba’ huyo.
Mzazi huyo aliiambia OFM kuwa amekuwa akifuma mawasiliano ya kwenye simu ya mkononi ya mwanaye na mwanaume huyo ambaye alikuwa hamfahamu.
FUNDISHO KWA WAZEE: Babu akijiandaa kuvaa nguo yake ya ndani baada ya kunaswa gesti.
CHANZO
Mama huyo alisema kuwa kutokana na maendeleo ya mwanaye kuzidi kudorora shuleni, aliamua kumfuatilia kwa karibu kwa kuwa hakutaka apotee.
Mama huyo alitiririka kuwa, siku ya tukio, alimsikia mwanaye huyo akiwekeana miadi kwenye simu na mwanaume huyo ndipo akaamua kumuwekea mtego.
Alisema wakati mwanaye huyo akilonga kwenye simu, yeye alibana sehemu na kuyasikia yote ambayo alikuwa akiyaongea na kwamba walipanga kukutana baa.
“Nilichokifanya nilimpigia simu mjomba wake na kumweleza kila kitu, nikamwelekeza namna ya kumfuatilia. Alichukua bodaboda na kuanza kumfuatilia. Mimi na timu yangu tulifuata nyuma,” alisema mama huyo kwa uchungu.
CHINI YA ULINZI: Babu akiwa mikononi mwa wanausalama.
Alisema mzee huyo alikubaliana na mwanaye wakutane kwenye baa hiyo ambapo ndani yake kuna nyumba ya kulala wageni a.k.a gesti.
OFM YAITWA
Baada ya mpango wa mtego kukamilika ndipo mama huyo akawaita OFM ambao huwa hawalazi damu hivyo walifika mara moja.
TAARIFA POLISI
Kabla ya kuchukua hatua yoyote, walishauriana kutoa taarifa kituo cha polisi, jambo ambalo lilifanyika na kupatiwa msaada wa kiusalama.
NI SAWA NA BABU YAKE
Walipofika kwenye baa hiyo mama mtu alipigwa na butwaa kumuona mtu aliyekuwa akiwasiliana na mwanaye ni mzee sawa na babu yake.
“Yaani jamani kweli dunia imekwisha, mwanangu ni sawa na mjukuu wa huyu mzee, ama kweli tamaa mbaya sana,” alisema mama huyo kwa uchungu.
Huku wakifuatiliwa kwa karibu, mzee huyo na denti walipiga madikodiko na vinywaji ndipo wakatimba kwenye gesti hiyo.
Kilichofanyika ni kwamba polisi na mama wa denti walizama gesti hiyo na kuomba kumsaka mwanafunzi huyo, jambo ambalo halikupingwa.
FUMANIZI LAIVU
Baada ya kuzama ndani ndipo mtego ukafyatuka ambapo mzee Omari alibambwa katika moja ya vyumba vya gesti hiyo huku akiwa amejifunga taulo tu.
Mzee huyo alipatwa na taharuki kubwa asijue la kufanya kufuatia timbwili zito alilozua mama wa denti huyo.
“Kha! Kazi kuharibu watoto wa wenzenu, hivi angekuwa wa kwako ukakuta akifanyiwa hivi ungejisikiaje? Nasomesha kwa gharama kubwa wewe unataka kuniharibia. Hivi hujui mtoto anauma?” alihoji mama huyo kwa hasira huku akimtandika mwanaye vibao.
OMBI
Mara baada ya mzee huyo kunaswa, aliomba chondechonde kukaa na familia ya mwanafunzi huyo ili kuyamaliza yasifike mbali.
Hata hivyo, baada ya maombi ya muda mrefu walikubaliana kuandikishiana ambapo mzee huyo alitakiwa kulipa faini.
“Sisi hatuna maneno mengi, hatutaki kesi ila atulipe fidia ya kumsababishia mtoto wetu asiwe na mahudhurio mazuri shuleni kutokana na ulaghai wake,” alisema mzazi huyo.
MZEE AINGIA MITINI
Habari zilieleza kuwa mzee huyo alishindwa kulipa mara moja badala yake aliingia mitini kwa kigezo kuwa anakwenda kutafuta faini hiyo.
Hadi OFM inaondoka eneo la tukio mzee huyo alikuwa hajawasilisha faini waliyokubaliana hivyo tunafuatilia na tutakachobaini tutaandika katika matoleo yajayo.
FUNDISHO
Hivi sasa kumeshamiri tabia ya wazee kupenda kuharibu mabinti wadogo hivyo kunaswa kwa mzee huyo litakuwa fundisho kwa wengine kwani OFM ambao huwa haikosei, imeamua kulivalia njuga suala hilo. Subirini muone!

GPL.

KANYE WEST ALIPA ZAIDI YA MILIONI 350 ZA KITANZANIA KWA YULE DOGO ALIYEMWANGUSHIA KICHAPO BAADA YA KUMSEMEA MBOVU KIM K.


Wiki chache zilizopita, ililipotiwa kuwa Kanye West alimshambulia mvulana wa miaka 18 kwenye sehemu ya mapokezi ya ofisi za chiropractor.

Na sasa kwa mujibu wa TMZ, Kanye amefikia makubaliano nje ya mahakama ili kumalizana na kijana huyo kwa kumlipa fidia ya $250. Familia ya kijana huyo mdogo imesema kwamba hiyo ilistahili kulipwa kwa kitendo alichofanyiwa kijana huyo na Kanye.

DC Blog.

A-Z, KUJINYONGA KWA MSANII WA BONGO MOVIES HII HAPA


SAKATA la kujinyonga kwa msanii wa filamu Bongo, Victor Peter limegubikwa na matukio tofauti ya kustaajabisha ambayo marehemu aliyafanya siku kadhaa kabla hajapatwa na umauti, Ijumaa limefukunyua kila kitu.
Mwili wa marehemu Victor Peter ukipelekwa mochwari.
Kwa mujibu wa rafiki wa marehemu, Hamisi Koba, msanii huyo alijinyonga usiku wa Februari 27, mwaka huu mkoani Tanga ambapo marehemu alifika jijini humo kuigiza filamu yake iitwayo Our Family.
Hamisi alisema Victor aliwasili jijini humo akiwa na timu ya wasanii sita na kufikia kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Safari Junior iliyopo maeneo ya Kisosora ambapo punde walianza kushuti filamu hiyo ambayo yeye na Mzee Jengua ndiyo walikuwa wahusika wakuu.
Marehemu Victor Peter enzi za uhai wake.
“Mimi ndiye nilikuwa kama mwenyeji wake mkubwa hapa Tanga, alikuwa ni mpole na siku zote tulipokuwa kazini kwa ajili ya kushuti filamu hiyo aliniambia mambo mengi kuonesha amejipanga kuhakikisha anaifikisha mbali.
“Victor alitokea Mwanza, akaenda Dar ambapo alifika na kuandaa filamu yake ya kwanza aliyoiita Chozi ambayo tayari ilikuwa imekamilika na kuiuza kwenye Kampuni ya Kapiko ya jijini humo,” alisema Koba na kuongeza:
“Filamu hiyo ilikuwa bado haijatoka, akaamua kuja Tanga kuandaa filamu hiyo ya pili ambayo nayo ilikamilika juzi. Naumia sana ninapokumbuka mipango yake maana alikuwa ana ndoto za kufanya makubwa.
Wasanii wenzake na marehemu wakilia kwa simanzi.
“Siku ya Januari 27 tulipokuwa tunakamilisha filamu, kuna muda alikuwa anaonekana kama ana wenge hivi... alipomaliza kushuti sehemu yake tulienda benki, akachukua fedha na kuwalipa wasanii wote.”
Akiendelea kutiririka juu ya tukio hilo, Koba alisema marehemu alionesha kama alikiona kifo chake kabla kwani aliuliza mara mbilimbili kama kuna mtu anamdai ili amlipe.
“Wakati anatupatia fedha kila mara alikuwa anauliza kama kuna mtu anamdai hadi tuliingiwa wasiwasi na ingawa wengine walisema atakuwa amefurahia labda kumaliza muvi yake,” alisema.
Koba alizidi kueleza kuwa, marehemu akiwa na furaha ya kumaliza muvi hiyo, alikwenda chumbani kwake na kujifungia lakini alfajiri (Januari 28) walipomgongea mlango waligundua amejinyonga.
Baadhi ya mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
“Tulichungulia kupitia tundu la funguo tukaona kama ananing’inia ndipo tukaenda kwenye kituo cha Polisi cha Chumbageni na kuchukua askari ambao walishirikiana na mwenye gesti hiyo kuvunja
mlango na kumkuta kajinyonga, tukachukua mwili na kuupeleka kwenye Hospitali ya Bombo, mipango ya kuusafi risha mwili kwenda Kahama nyumbani kwao imeanza,” alisema Koba na kuongeza:
“Kwenye hiyo filamu yake, stori ilikuwa mzee Jengua kama baba wa Victor ambapo Mzee Jengua alikufa na baadaye Victor anakufa kiajabu, kifo kimempata kweli.”
Kuhusiana na kifo hicho, Koba alisema kilimuuma kwani alikilinganisha na kile kilichomtokea marehemu Steven Kanumba ambaye pia aliigiza filamu ya Power of Love ikionesha anakufa, akafa kikwelikweli.
Mwili wa marehemu uliokuwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Bombo ulitarajiwa kusafi rishwa juzi kwenda nyumbani kwao Kahama kuzikwa.

GPL

GURUMO AFAGILIA DIAMOND PLATINUMZ KWA KUWAKAMUA WATOTO WA KIKE TOFAUTI TOFAUTI, ADAI WANAJIPELEKA WENYEWE.


MSANII mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Muhidini Gurumo ambaye kwa sasa amestaafu, amefungukia skendo ya kuwa na mademu wengi inayomuandama Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni maeneo ya Ilala jijini Dar, Mzee Gurumo alisema: “Diamond ana nidhamu sana ila vile anavyotamba jukwaani na kudatisha mashabiki hapo ndipo balaa linapokuja, watoto wa kike wenyewe wanaanza kujisogeza kwake.
Mzee Muhidini Gurumo.
“Pamoja na skendo za mademu zinazomuandama, siwezi kumshusha thamani, ana haki ya kujiopolea mwanamke yeyote anayempenda, yeye kama mwanaume rijali wakati mwingine ni vigumu kujizuia na vishawishi hivyo.”
GPL.

WOLPER APAGAWA NA PENZ* LA JAMAA WAKE MPYA, AWACHANA WATU WASIMSHOBOKEE!!


THE Ijumaa Sexiest Girl 2012, Jacqueline Wolper amesema kuwa, ana imani kubwa na mpenzi wake wa sasa aliyemtambulisha kwa jina la G Modo akiamini atampoza machungu aliyoyapata kutoka kwa mpenzi wake wa zamani, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ huku akiwatahadharisha mashosti zake kutoleta shobo (kuwa mbali naye).
Jacqueline Wolper.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Wolper alisema anafikia hatua ya kusema hayo kwa kuwa muda mfupi aliokuwa naye amegundua ni mwanaume anayejitambua na anayeheshimu mapenzi ila akawataka mashosti zake kutomsogelea.
“Tangu niwe na huyu kijana nimekuwa ni mwenye furaha kubwa, nasahau hata yale machungu niliyopata kwa mpenzi wangu wa zamani. Lakini najua wapo wanaomtolea macho, tusitafutane ubaya, kila mtu na maisha yake,” alisema Wolper.
GPL.
Blogger Widgets