Monday, February 3, 2014

WEMA NAE KAVURUGWA, ETI AKIFA AAGWE UWANJA WA TAIFA MAANA LEADERS HAPATA TOSHA.


Kazi ipo! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ambaye huwa haishiwi habari, ameibuka na jipya akidai kuwa akifa leo au kesho basi aagwe Uwanja wa Taifa jijini Dar, Ijumaa Wikienda limemtegea sikio.
Wema Isaac Sepetu.
Miss Tanzania huyo wa 2006/07 ambaye anakimbiza kwenye sinema za Kibongo alifunguka hayo wikiendi iliyopita wakati akiwa safarini kuelekea jijini Arusha ambapo msanii anayemilikiwa na kampuni ya Wema ya Endless Fame Production aliyetajwa kwa jina moja la Mirrow alikwenda kuangusha shoo pande hizo.
Wema aliyasema hayo alipokuwa akichangia mada ya utabiri wa mtoto wa aliyekuwa mtabiri bingwa, marehemu Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan Hussein aliyetabiri kwamba wasanii wengi wenye majina makubwa watakufa mwaka 2014.
Mwanadada huyo alisema mastaa wengi wameaga dunia na kuagwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni lakini yeye itakuwa Uwanja wa Taifa.
Alitolea mifano ya waliokuwa mastaa kama Steven Kanumba, Albert Mangweha ‘Ngwea’, Julius Nyaisangah ‘Anko J’ na wengine kuwa waliagwa Leaders lakini kwa namna ambavyo jina lake ni kubwa ndani na nje ya Bongo viwanja hivyo havitatosha.
“Mimi nakwambia kabisa, pale Leaders hapatatosha. Kama nikifa leo au kesho, niagwe Uwanja wa Taifa ili kila mtu apate nafasi. Naamini watu watakuwa wengi sana so Leaders hapatatosha,” alisema staa huyo mkubwa anayeminya kilamalavidavi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Ijumaa Wikienda lilipododosa kwa marafiki zake wa karibu lilitonywa kwamba tayari jambo hilo alishawaeleza na kwamba aliomba iwe hivyo.
Mbali na wasanii, Maalim Hassan alitabiri pia kuwa mwaka huu kuna mwanasiasa mkubwa atakufa na utakuwa msiba wa kitaifa, vifo vya wanahabari na malumbano makubwa juu ya serikali tatu.
Wiki iliyopita ilijaa simanzi baada ya kufariki dunia kwa watu maarufu kama mchekeshaji wa Futuhi ya Star TV, Omary Majuto ‘Mzee Dude’, mpiga ngoma wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Soud Mohamed ‘MCD’, mwigizaji wa Bongo Movies, Victor Peter na mtangazaji wa East Africa Radio, Kenneth Kidago Lyanga.

GPL.

CCM YAWATEKA WASANII WA BONGO MOVIES, MAMIA WAJIUNGA RASMI.


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kupata wanachama wapya ambao ni wasanii wa tasnia mbalimbali, miongoni mwao ni Uwoya, Johari, Banana, JB na Mrisho Mpoto.

Chanzo: Jamii FORUMS

SNURA ALIA NA WABAYA WAKE, WANAOTAMANI AANGUKE.


STAA aliyeliteka soko la mduara kwa kibao chake cha Majanga, Snura Mushi amesema watu wenye chuki na yeye wamepanga njama za kumshusha kwenye chati kutokana na maendeleo yake.
Snura Mushi.
Akipiga stori na paparazi wetu juzi, Snura alisema: “Nashangaa sana ninapofanya jambo zuri halafu watu wanaligeuza kuwa baya ili nichafuke jina na kunipunguzia mvuto kwa mashabiki wangu.”
Chanzo cha yote ni baada ya mwanadada huyo kupiga shoo kwenye Ukumbi wa Buliyaga, Temeke, Dar siku chache zilizopita, kundi la watu wasiojulikana walianza kueneza taarifa kuwa alifanya vibaya na mashabiki wakamtaka ashuke jukwaani jambo ambalo alisema halikuwa na ukweli wowote.

"NINGEMKOSA H BABA MAISHANI MWANGU NINGEYUMBA" FLORA


UA la Bongo Movies, Flora Mvungi amefunguka kuwa anashukuru Mungu kumpata mume mwema, Hamisi Baba ‘H.Baba’ kwani vinginevyo angeyumba kimaisha.
Flora Mvungi na mumewe H. Baba.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Flora alisema H. Baba ni mwanaume anayestahili sifa zote hivyo endapo angekutana na mwanaume mwingine basi angeyaona mapenzi machungu.
“Mungu hakukosea kuniletea H. Baba, nampenda sana kwani ni mtu anayenijali mimi na mtoto wetu Tanzanite yaani sijui kitu gani ambacho nakikosa kwake, bila huyu maisha yangeyumba,” alisema Flora.

RAYUU BADO ANATAMANI KUTEMBEA NA MUME WA MTU, ASEMA HAWEZI KUJIZUIA.


MSANII kinda kwenye tasnia ya filamu Bongo, Rahma Bagenzi ‘Rayuu’ amesema kuwa, kamwe hatokoma kutembea na waume za watu kwa kuwa sheria ya dini yake ya Kiislamu inamruhusu kuolewa na mume wa mtu.
Rahma Bagenzi ‘Rayuu’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Rayuu alisema kipindi cha nyuma aliwahi kutoka kimapenzi na mume wa mtu (hakumtaja jina) na kufikia hatua ya kufikishwa polisi na mwenye mke lakini haimaanishi kuwa hatatembea tena na mume wa mtu.
“Nikila kiapo cha kutotembea na waume za watu nitakuwa naongopa, kwanza dini yetu imeruhusu ndoa za uke wenza huenda  Mungu kaniandikia niolewe ndoa ya aina hiyo sina uwezo wa kupingana naye,” alisema Rayuu.

GPL.

DR CHENI APANIA KUIRUDISHA KAOLE SANAA GROUP.


MWENYEKITI Msaidizi wa Bongo Movie Unity, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amesema amekumbuka na kutamani kurudisha Kundi la Sanaa ya Maigizo la Kaole ‘Kaole Sanaa Group’ liwe na nguvu kama zamani.
Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’.
Dk. Cheni alisema japo kundi hilo limeonekana kupoteza mvuto wake wa awali, lakini anaamini wasanii wengi wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya filamu kwa sasa wametoka katika kundi hilo maarufu.
Hata hivyo, pamoja na kupotea kwa kundi hilo, Dk. Cheni anatamani sana kulirejesha kwenye ulingo wa sanaa na kwamba kuna mikakati anayoiandaa ili kukamilisha azimia hiyo.
“Naitamani Kaole ya zamani, nahisi kama kuna vionjo vinakosekana siku hizi. Wasanii wengi wenye majina makubwa kwa sasa wametoka kwenye kundi hilo, lakini nitajitahidi kulirudisha, naamini nitafanikiwa,” alisema Dk. Cheni.

BAADA YA KUJIINGIZA KIAINA NA SIASA, WANA BONGO MOVIES WAMTAKA STEVE NYERERE AJIUZULU.


Hali si shwari katika klabu ya wasanii wa filamu za Kibongo, Bongo Movie Unity ikidaiwa kuwa baadhi ya ‘memba’ wake wanashinikiza mwenyekiti wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ajiuzulu.
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Habari zilizoifikia Stori Extra wikiendi iliyopita zilidai kuwa, baadhi ya wasanii wa klabu hiyo akiwemo mwenyekiti huyo walilamba mshiko kutoka kwa mwanasiasa mmoja wa CCM mkoani Mbeya ili wamfanyie kampeni katika uchaguzi ujao jambo ambalo wenzao walilipinga vikali kwa kuwa wao hawajihusishi na siasa bali wasanii na jamii.
Alipotafutwa Steve kujibu tuhuma hizo hakupatikana lakini katibu wake, William Mtitu alikiri kuwepo kwa ishu hiyo.
GPL.
Blogger Widgets