Friday, August 2, 2013

Kipanya na Uhaba wa Fedha


-->

Yawezaekana Hili Likaja Tokea, Wenye Pesa Zao Wakae Chonjo.

Thursday, August 1, 2013

Wanaume wenye KORODANI( "MAPUMBU") Makubwa wapo hatarini kupata Magonjwa ya Moyo



Daah, sasa kwa wale wenzangu na mimi ambao tuna mizigo mikubwa naomba tukae vizuri na tuelewane ya kwamba Silaha Pesa, Kisu Mzigo.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Florance Huku Uingereza umebaini ya kwamba Wnaume wenye Korodani "Mapumbu" Kubwa wapo hatarini Kupata Shinikizo na Damu na wengi wao hupendelea kunywa Pombe kupindukia.

Pamoja na hayo hawakusema ni kipi hasa kinapelekea Baadhi ya Wanaume kuwa na Korodani Kubwa. Wanasayansi hao waliweza kuwapima Wanaume 2,809 ambao walikuwa wanahudhuria Clinic za Afya ya Uzazi ambapo walikuwa wakiwapima saizi ya Korodani hizo na kiwango cha Hormone na kuwa wanawafatilia kwa uangalizi wa kipindi cha miaka Saba.

Kwa kipindi hiki waligundua ya kwamba wanaume wenye Korodani Kubwa ndio waliokuwa na matatizo ya Moyo sana, Pia waligundua wanaume hao wenye Korodani Kubwa walikuwa na Luteinising Hormone ambayo huathiri saizi ya Korodani hizo.




Men with large testicles are also more likely to be hospitalised with heart problems and tend to be heavier, drink more alcohol, and to have higher blood pressure


Hormone Hiyo huwa na Athari katika Moyo, Ingawa Tafiti zilizopita zilibainisha Ufanisi katika suala zima la Uzazi katika Wanaume wenye Korodani Kubwa, Tafiti hii inapingana na hiyo ya kuzikombatia zilizopita.

Ex-Lover wa Pokello, Mshiriki wa BBA Amjibu kwa Nyimbo.


Mwanamuziki, Rapper Stunner ameachia Single yake mpya inayokwenda kwa jina la "Bye Bye" ambayo kiundani inamjibu Aliyekuwa Mpenzi wake, Mwakilishi katika jumba la BBA The Chase, Pokello ambaye uhusiano wao ulivunjika baada ya mwanamke huyo kuanzisha mahusiano na Mshiriki Mwenzie Elikem wa Mjengoni hapo

Pokello alimkacha Stunner live katika mahojiano na kiyuo kimoja cha Television cha nchi hiyo, wengi wamesema mbinu ya mwanadada huyo kujiweka karibu na Stunner ilikuwa ni kujijengea Umaarufu tu.

Akimbiwa na Mumewe Baada ya Kujifungua Mapacha 3,


Pichani ni Mke wa Mkulimu kutoka Jimbo la Ogun, Bi Bosede Akapo, 30, Ambaye analalamikia kukimbiwa na mumuwe baada ya kujifungua watoto watatu mapacha siku ya tarehe 24/07/2013.

Imeelezwa kuwa Bw. Biodun mume wa mwanamke huyo alikimbia siku ambayo Bosede alianza kuumwa Uchungu wa Uzazi. Kabla ya ujio wa malaika hao watatu, tayari familia hiyo tayari ilikuwa ana watoto wawili hivyo kuifanya idadi ya watoto kuwa watano ambao wamempelekea Mkulima huyo kuingia mitini.

Mwanamke alipata msaada wa kuzalishwa na wazee wa kijijini kwake ambao walimsaidi kumpandisha Pikipiki na kumpeleka katika kituo cha afya na huko ndipo mambo yalipojulikana. Amesema hakuwahi kufanya Kipimo cha " Ultra Sound" kufahamu Watoto na Jinsia kwani hakuwa na uwezo huo.

Anamsihi mwanaume huyo kurudi nyumbani wailee familia hiyo kubwa ambayo peke yake haitaiweza.

Chupa za Kunyonyeshea Watoto Zinawasababishia Watoto Saratani.


Dar es Salaam. Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), imesema matumizi ya chupa za plastiki za kunyonyeshea watoto maziwa, zinaweza kuwasababishia ugonjwa wa saratani.
Mratibu wa watoto wachanga na wadogo wa TFNC, Neema Joshua, alisema juzi kuwa taasisi hiyo inawataka wanawake kutumia vikombe badala ya chupa.
Joshua alisema chupa hizo zikioshwa kwa maji ya moto hutoa chembechembe, ambazo watoto wakizinywa zinaweza kuwasababishia ugonjwa huo, kwa maisha ya baadaye.
Alisema ingawa hakuna utafiti uliofanywa kuthibitisha hilo, lakini chembechembe za plastiki zinapotumiwa na binadamu huweza kusababisha saratani.
“Tunaomba wanawake wasitumie chupa hizo licha ya kuwa zipo nyingi dukani, watumie vikombe kuwanywesha watoto wao,” alisema.
Pia, Joshua alisema chupa hizo hazifai kwa sababu ni vigumu kuziosha kwa ufanisi, kutokana na muundo wake hali inayoweza kuwasababishia watoto magonjwa mbalimbali.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe, Dk Joyceline Kaganda, alisema ukosefu wa lishe bora unaweza kusababisha kudumaa kwa mwili hata akili.
“Tunaweza kulaumu Serikali kwa matokeo mabaya ya mitihani, lakini kumbe matokeo hayo yanaweza kusababishwa na ukosefu wa lishe kwa wanafunzi,” alisema. Dk Kaganda alitaka wanawake kuwanyonyesha watoto maziwa tangu wanapozaliwa hadi wanapofikisha umri wa miezi sita, bila kuongezewa chakula chochote.
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Donald Mmbando, alisema ni asilimia 49 ya wanawake wanaojifungua ndiyo wanaowanyonyesha watoto kwa muda sahihi.
Chanzo:- Mwananchi

Kajala Atimkia South Africa, Wadau Wamohofia na Madawa, Mwenyewe Asema ni kupunguza Stress Tu!!!


Imelda Mtema
MWIGIZAJI Bongo, Kajala Masanja ambaye miezi michache iliyopita alichomoka nyuma ya nondo za Segerea kwa dhamana, ametimkia nchini Afrika Kusini kupunguza mawazo.
Kajala Masanja.
Mapema wiki hii, Kajala alitupia picha zake mbalimbali katika mtandao wa Instagram zikimuonyesha akiwa nchini humo na kusindikiza na ujumbe wa maandishi uliosomeka kuwa amekwenda kwa ajili ya kubadilisha hali ya hewa kwani toka akumbwe na matatizo, hajapata mtoko wa kupumzisha akili.
“Nimekuja kubadilisha hali ya hewa  maana nimetoka kwenye matatizo, sijapata kabisa muda mzuri wa kuipumzisha akili yangu hivyo nimeona bora nije huku kupumzika kidogo kisha nitarejea nyumbani,” alisema Kajala.

Source: GPL

Waziri Mkuu Afunguliwa Kesi Rasmi Mahakamani, Ni kutokana na kauli yake ya Kuruhusu Raia Kupigwa na Vyombo vya Dola.


Dar/Dodoma. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemfungulia mashtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokana na kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kwamba wanaokaidi maagizo ya dola wapigwe.
Hatua hiyo ya LHRC imepingwa vikali na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Dk Elieza Feleshi akisema hakuna uhalali wa mashtaka yoyote dhidi ya kiongozi huyo sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.

Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo Bisimba alifungua mashtaka hayo katika Mahakama Kuu jana akisema kuwa wanamshtaki Waziri Mkuu kwa maelezo kuwa amekiuka kifungu cha Katiba Ibara 13 (1). Pinda ametajwa kuwa ni mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 24.
Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia alisema jana kwamba, mwingine aliyeunganishwa katika kesi hiyo ya kikatiba iliyofunguliwa na LHRC na Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Alisema katika kesi hiyo, kuna jopo la mawakili wasiopungua 20 na kwamba wamepata saini za wananchi 2,029 wanaopinga kauli hiyo ya Pinda na kuunga mkono kufunguliwa kwa kesi hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya LHRC, Wakili Dk Ringo Tenga alisema katika kesi hiyo wameangalia zaidi sheria na hasa haki za msingi za binadamu na kwamba kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda inahatarisha haki hizo.
Kauli yenyewe
Wakati wa Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu bungeni, Juni 19, mwaka huu, Waziri Mkuu akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyeuliza: “Serikali ipo tayari kiasi gani kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”
Waziri Mkuu alijibu: “Ni lilelile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka.” Kesi hiyo itakayosikilizwa na majaji watatu, haina uhusiano na kesi nyingine ambazo wajibu maombi hupewa siku 90 kujibu hoja zilizowasilishwa. Kesi hiyo imefunguliwa kwa mujibu wa Katiba Sura ya Tatu.
 Inaendelea katika Chanzo - Mwananchi
Blogger Widgets