Wednesday, January 29, 2014

WATOTO 6 KWA MAMA TOFAUTI WAMFILISI DUDE, AKOSA PESA YA KUREKODI TAMTHILIYA YAKE.

HALI ya uchumi ya mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’ imemkwamisha mwigizaji huyo ashindwe kurekodi tamthiliya yake.
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akizungumza na paparazi wetu, Dude alikiri kuwa uchumi umemkalia vibaya ambapo aliruhusiwa kupewa muda wa hewani katika Runinga ya East Africa lakini akashindwa kushuti kutokana na majukumu ya kifamilia kumuandama.



“Daa we acha tu, mwezi wa kwanza huu majanga matupu. Nimeshindwa, kama unavyojua nina watoto wengi mambo ya ada yamenibana kwelikweli,” alisema Dude ambaye ana jumla ya watoto sita kwa mama tofauti.

FARAJA KOTA, AFUNGUKA YA MOYONI KUHUSIANANA MUMEWE, WAZIRI NYALANDU.

MISS Tanzania 2004, Faraja Kota amefunguka kuwa kamwe hawezi kuingilia kazi za mumewe ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwani anaamini mumewe ana akili nyingi kuliko yeye.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Akizungumza na paparazi wetu, Faraja alisema siyo rahisi kuingilia kazi za mume wake zaidi ya kuzungumza naye kidogo sana kama kuna kitu amekiona anaweza kumshauri kwa sehemu fulani lakini siyo kwa kiasi kikubwa sana.
Faraja Kota.



“Unajua mume wangu ana akili zaidi kuliko hata mimi, naweza kumshauri kidogo tu kama nitakiona kitu fulani na siyo vyote kwa sababu ninaporudi nyumbani anakuwa ni baba zaidi na siyo kama waziri,” alisema Faraja.

MIMBA ILIVYOMNYIMA "DILI" ZA HELA DAVINA WA BONGO MOVIES

STAA wa Bongo Movie, Halima Yahaya ‘Davina’ amefunguka kuwa mwaka 2013 aliutumia zaidi kwa kulea mimba hadi kujifungua hivyo kukosa madili ya kazi za uigizaji.
Halima Yahaya ‘Davina’.
Akizungumza na paparazi wetu, Davina alisema mwaka huu amejipanga kurejea upya katika sanaa kwani amegundua kuwa mashabiki wake walikuwa wamemmisi hivyo lazima apambane kutetea taito yake katika sanaa.



“Nimejipanga zaidi mwaka huu, nimedhamiria kufanya mapinduzi makubwa katika sanaa tofauti na kipindi cha nyuma, kulea siyo mchezo ilibidi sanaa ikae pembeni kidogo,” alisema Davina ambaye sasa ni mama wa mtoto mmoja, Fazal.

AMBER ROSE, JIKO LA WIZZY KHALIFA, ATUPIA ZA KIMETEGO MTANDAONI, NI SHIDAAA!!!!


Hakika ni kama anajaribu kuwatega watu kwa umbile lake matata, kwani hivi karibuni mrembo huyu aitwaye Amber Rose aliamua kuzitupia picha zake kwenye mitandao ya kijamii katika hali tu ya kushea picha hizo na watu wake! Hakika ni mkali...

Mcheki hapo chini kwa picha zaidi...


DC.

MFANYA BIASHARA APIGWA RISASI 3 NA KUFA PAPO HAPO NDANI YA GARI LAKE.

Mwili wa marehemu Ahmed Bakhshuwein baada ya kupigwa risasi.
Mfanyabiashara, Ahmed Bakhshuwein ameuawa kwa kupigwa risasi tatu kichwani akiwa kwenye gari eneo la Malindi, Mombasa karibu na Al-R azaak Stores nchini Kenya.
CREDIT: Michuzi Issa.




HALI ILIVYOKUWA WAKATI JENGO LA JMC LILIVYOPAMBA MOTO LEO MCHANA





JENGO la JMC lenye ghorofa saba lililopo eneo la Kamata mtaa wa Kasanga Kariakoo jijini Dar linaungua moto muda huu! Vyombo mbalimbali vya usalama vipo eneo la tukio vikijaribu kupambana na moto huo ambao bado unaendelea kuteketeza mali zilizomo ndani ya jengo hi

BILIONEA WA KIKE "OPRAH WINFREY" ATIMIZA MIAKA 60 LEO.


MWIGIZAJI, mmiliki wa vyombo vya habari, mtangazaji, prodyuza kutoka nchini Marekani, Oprah Gail Winfrey leo ametimiza umri wa miaka 60. Oprah ambaye amejishindia tuzo mbalimbali kupitia kipindi chake cha 'The Oprah Winfrey Show' alizaliwa Januari 29, 1954 Mississipi nchini Marekani. Oprah ni bilionea namba moja ambaye ni Mmarekani mweusi wa karne ya 20.
Blogger Widgets