Friday, December 27, 2013

MREMBO WA TANZANIA ALIENASWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO CHINA



Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao.

Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.

Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013.

Taarifa zisizo rasmi zinasema dada huyu anaitwa  Jackie Cliff, aliyeonekana kwenye wimbo wa Diamond uitwao 'Nataka Kulewa' ambaye pia inasemekana aliwahi kuwa mshiriki wa Miss Tanzania miaka ya nyuma. 



No comments:

Post a Comment

Blogger Widgets