Kanisa hilo ambalo linajulikana kwa jina la The Pool of Siloam lililoko Mbezi- Makonde, Kinondoni, Dar es Salaam linafanya ibada zake Jumanne badala ya Jumapili wakiamini ndivyo Neno la Mungu linavyotaka.
Jambo lingine ambalo linachagiza u-ajabu wa kanisa hio ni kupinga jina la Biblia Takatifu. Muumini mgeni anayefika kwenye kanisa hilo hulazimika kukabidhi Biblia yake kwa uongozi ambapo wao hutoa ‘kava’ ya nje yenye jina la Biblia na kuweka kava nyeupe yenye maandishi ya Kitabu Cha Bwana.
Kama vile hayo hayatoshi, kanisa hilo linaamini siku za mwezi ni 28 na si 29, 30 au 31. Wanasema Mungu alipanga hivyo na ndiyo maana aliwapa hata wanawake mzunguko wa siku 28 kuingia katika hedhi.
“Kinachotuingiza kwenye majira halisi ya Mungu ni kufuta tarehe 29, 30 na 31 za Julius Kaisari katika kila mwezi wa kalenda ya Gregori kwa mamlaka ya Mungu wa Majeshi ili kuondoa uovu ulioambatana na tarehe hizo za ziada kwenye miezi 12 ya mwaka,” alisema muumini mmoja kanisani hapo.
Uchunguzi unaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2008 kanisa hilo lilichapisha kitabu ambacho kinaonesha kuwa mwanzo wa mwaka si Januari bali ni Machi (wao huita Abib au Aviv). Na mwisho wa mwaka si Desemba, bali ni Februari (wao huita Adari).
Source: GPL.
No comments:
Post a Comment