Saturday, December 28, 2013

"SIAMINI KUHUSU MUNGU" KATY PERRY


Nyota wa muziki wa Pop mwenye umri wa miaka 29 ambaye alizaliwa na kukulia katika mazingira ya Kikristo Katty Perry, alipokuwa akifanyiwa mahojiano na jarida la U.S la Marie Claire alisema kwa sasa haamini tena juu ya imani yoyote ya Kidini.

Katy Said: “Siamini cha Mbinguni wala Motoni, au kwa Mzee aliyeketi kwenye kiti cha ufalme. Naamini kwenye nguvu kubwa na za juu zaidi yangu sababu hiyo inanifanya nitambulike,” alilieleza jarida hilo.

“Uwajibikaji ni ngumu kuupata, hasa kwa watu kama mimi, sababu hakuna atakayetaka kuniambia kitu ambacho sitaki kukisikia.”  Perry akaongeza: “Mimi sio Mbuddhist, sio Mhindu, sio Mkristo, ila bado naamini kwamba nna muungano wa karibu na Mungu.

Nasali na kuomba kila wakati kwa ajili yangu kwa utu. Kuna ukweli ndani yake japo kwa kusema 'asante' wakati mwengine ni vizuri kuliko kuomba vitu.”

No comments:

Post a Comment

Blogger Widgets