Kwa mujibu wa Abiria waliohojiwa wanasema Boti ya Kilimanjaro II ikitokea Pemba kuelekea Unguja imepigwa na dhoruba leo Jan 5 2014 kwenye saa nne asubuhi na kuponea kuzama ilipokua kwenye eneo hatari la Nungwi ambapo ilizama kidogo mbele na kunyanyuka hivyo watu wa mbele wote wakaachwa lakini pamoja na kuwatupa hao watu kwenye maji Nahodha akafanya uamuzi mwingine mgumu.
Hali ilivyo ndani ya boti ambayo imeendelea na safari ni watu kujawa na huzuni na wengine wamebaki wanalia tu.
KAULI YA POLISI KUHUSU TAARIFA YA ABIRIA 10 WALIOTUPWA MAJINI
Kuhusu taarifa za watu 10 kurushwa baharini wakati upepo mkali ulipotokea, Polisi wanasema ‘hakuna mtu yeyote aliedondoka baharini na hizi taarifa ni kwa mujibu wa Captain wa boti hii N. Abubakar’
No comments:
Post a Comment