Mwaka 2013, vuguvugu la Anaconda lilimsaidia Lady Jaydee si tu kukusanya mashabiki wengi zaidi, bali pia limempa fedha nyingi mno. Hadi sasa muimbaji huyo ana zaidi ya likes laki mbili kwenye Facebook na followers zaidi ya 60,000 kwenye Twitter.
Zaidi ya tiketi 3,500 zilinunuliwa kwenye show yake ya mwezi June ya Miaka 13 ya Muziki na kuingiza takribani shilingi milioni 100. Haikuishia hapo, album yake Nothing But The Truth ilifanya vizuri na kumfanya kuwa msanii pekee wa Bongo Flava anayeendelea kufurahia mauzo ya album zake.
Hits zake mbili, Joto Hasira na Yahaya kutoka kwenye santurui take hiyo, zimebadilisha maisha yake na kumfanya kuwa mwanamuziki aliyekuwa na show nyingi zaidi mwaka jana. Lady Jaydee alitumbuiza kwenye karibu show zote za Kili Music Tour ambako aliiingiza si chini ya shilingi milioni 25.
Mwaka jana pia Lady Jaydee amefanya show nyingi kubwa ikiwemo ile ya uzinduzi wa filamu ya Lulu, Foolish Age, show yake kwenye Miss Tanzania 2013, Family Day Show ya Arusha iliyofanyika Eid Pili, Anaconda Show iliyofanyika Triple A na nyingine iliyofanyika Snow View Hotel. Akiwa Arusha pia, Lady Jaydee aliuza kopi za album yake kama njugu pamoja na t-shirt za Anaconda zilizouzwa kwa shilingi 15,000 kila moja.
June mwaka jana, Lady Jaydee alitumbuiza kwenye semina ya kuwezesha wanawake kuondokana na njaa na umaskini, iliyofanyika chini ya mfuko wa fursa sawa kwa wote chini ya mama Anna Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani Lounge, imeendelea kufanya vizuri pia kwa kupata wateja wengi wanaoenda kupata chakula, vinywaji na burudani kutoka kwa bendi yake ya Machozi.
Bado anaingiza fedha kupitia udhamini wa Airtel kwenye show yake ya TV ya Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo ambaye jina lake ni Judith Wambura pia miongoni mwa wasanii 24 wa bara la Afrika waliochukuliwa kwenye mradi wa Coke Studio Africa wa kampuni ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi Kenya. Na sasa Lady Jaydee amekuwa msanii wa Tanzania anayemiliki gari aghali zaidi, Range Rover Evoque.
“Hakupenda kudisclose mambo ya bei wala wapi alikoinunua,” mume na meneja wa Lady Jaydee, Gadner G Habash ameiambia Bongo5.
“Lakini tunashukuru Mungu kwa baraka zake na nguvu ya mashabiki wake amefikia hapo. Hiyo ni gari aina ya Range Rover Evoque. Gari hizi mara nyingi hapa Tanzania kuna wakala wake kampuni inaitwa CMC Moters, ni moja kati ya magari latest sana,” amesema Gadner.
Gadner amezitaja sababu za mafanikio ya Jaydee ni pamoja na ‘karama na fadhila ya mwenyezi Mungu, nguvu anayoipata kutoka kw mashabiki wa muziki nchini.
“Wamekuwa wakimwamini, wamekuwa wakimsupport na kwa jinsi hiyo ndio maana amekuwa anapata mafanikio. Sababu ya tatu ni ile commitment yak wake yeye mwenye kama msanii. Jaydee ni mtu ambaye ana bidii sana kwenye kazi yake na anapenda sana muziki. Jambo hili linafanya siku zote awe makini na umakini ule unampelekea awe na mafanikio kusema ukweli. Kitu kingine ni kwamba ni mtu ambaye anathamini kesho yaani kama leo tumefanya vizuri, je kesho itakuaje! Huwa anafikiria sana kutowaangusha mashabiki wa muziki wanaomsupport.”
Gadner amesema pamoja na kuwa na biashara yake ya Nyumbani Lounge, Lady Jaydee anatarajia kuongeza zaidi miradi mingine. “Huyu bado ni mjasiriamali mchanga anayejifunza zaidi na angependa kufanya biashara nyingi lakini muda ni mdogo. Isipokuwa kwa mwaka huu alitarajia kufanya kitu kingine kuongeza kama biashara. Hajawa tayari kusema ni kitu gani lakini mwenyezi Mungu akijaalia heri na afya mwaka huu kuna biashara nyingine Jaydee ataitambulisha, ukiacha Nyumbani Lounge na muziki,” Gadner amefafanua.
Akiongelea ushiriki wa Jaydee kwenye kipindi cha Coke Studio Africa, Gadner amesema Jide amejiongezea connection kubwa na amejifunza mengi.
“Pamoja na kuestablish mawasiliano lakini kumekuwa na kujifunza kwa malegend kama Salif Keita na zaidi ya hapo kumekuwa na kama aina flani ya miradi ya kufanya kazi pamoja na wasanii waliofika pale. Mzee Salif Keita amemkubalia Jaydee wakati wowote atakapokuwa tayari aende Mali wakafanye wimbo pamoja. Hali kadhalika Octopizzo kutoka Kenya tayari wameweka kwenye line wimbo wa kufanya pamoja na Jaydee na wasanii wengine wa Nigeria akiwemo Waje.
Gadner amesema kwakuwa kufanya kazi na wasanii wa nje kunahitaji maandalizi ya kutosha, muda muafaka ukifika Jaydee ataanza kuifutilia miradi hiyo.
Gadner ambaye ni mtangazaji wa Times FM, ameongeza kuwa kwa mwaka 2014 Lady Jaydee atasikika kwenye kazi alizoshirikishwa ukiwemo wimbo wa Juma Nature, One, Songa na Nikki Mbishi, huku pia yeye akiachia wimbo mpya uliotayarishwa na Bob Junior na kwamba Historia unaopatikana kwenye Nothing But The Truth ni wimbo wa mwisho kutoka kwenye album hiyo.
Amesema video ya Historia imefanywa na kampuni ya Ogopa na kwa sasa ipo kwenye hatua ya editing.
Kuhusu wimbo mpya, Gadner amesema video yake itaongozwa na muongozaji Mtanzania aishiye Marekani, Hefemi.
“Nafikiri Jaydee alikuwa anataka afanye kitu cha tofauti na ndio maana akaamua amchukue director ambaye yuko nje ya Tanzania ili atupe picha na idea tofauti.”
“Nafikiri Jaydee alikuwa anataka afanye kitu cha tofauti na ndio maana akaamua amchukue director ambaye yuko nje ya Tanzania ili atupe picha na idea tofauti.”
No comments:
Post a Comment