Thursday, December 20, 2012

James Alivyooa "Shoga'!

   Kisa kinamuhusu kijana James ambaye amebarikiwa hela na utajiri wa kiasi chake aliopewa na wazazi wake. Kijana huyu alikuwa na maisha ya kawaida ya ndoa na Mkewe kabla ya Mungu kuchukua mkewe na wakafanya maziko kijijini kwao. Alipokuwa msibani wanandugu pamoja na wazee walimuuliza kuhusu uamuzi wa kuoa tena na kwamba angefanya jambo la busara iwapo angeoa msichana kutoka kijijini hapo, lakini alikataa na kusema anahitaji muda wa kutulia kidogo.
     Aliporudi mjini alikutana na rafiki yake mmoja ambaye mbali na mengi waliyoongea alimshauri usiku mmoja waende katika Club Moja Kwani kuna Party ya "Mashoga" jamaa akakubali na kwenda nae.Hapo ndipo maisha ya kijana James yalipobadilika kiasi cha kufikia kujitangaza yeye na mpenzi wake huyo mpya(shoga) aliyempata katika club hiyo ya usiku! Kitendo ambacho kilisababisha mtafaruku na ugomvi na familia yake lakini jamaa kabakia na msimamo wake.

No comments:

Post a Comment

Blogger Widgets