Wasifu wa Edward
Lowassa.
Je unamfahamu Edward Lowassa ni
nani katika siasa za Tanzania ?
Umoja usio rasmi wa
vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania unajulikana kwa jina la Katiba ya
Wananchi (UKAWA), baada ya kusubiri kwa muda hatimaye umemtangaza Waziri Mkuu
wa zamani Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais.
Lowassa anagombea
kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku vyama vingine vitatu
vikimuunga mkono. Hii inatokana na sheria za Tanzania ambayo haitambui umoja wa
vyama.
Kabla ya kujiengua
chama Tawala chama cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa amekuwa mwanachama wa CCM
kwa muda wa miaka 38, ambapo alijiunga na chama hicho mara tu baada ya kumaliza
elimu yake ya chuo kikuu mwaka 1977.
Hatua ya mwanasiasa
huyo mashuhuri nchini Tanzania kuamua kujiunga na chama cha upinzani Chadema,
ikiwa imebaki miezi mitatu tu kuelekea uchaguzi mkuu, kumebadilisha kabisa
upepo wa kisiasa nchini Tanzania, na hasa uchaguzi mkuu ujao.
Wasifu wa Lowassa
Lowassa alikuwa Maziri
Mkuu kati ya mwaka 2005 na 2008 kabla ya kujiuzuLu wadhifa huo kufuatia sakata
la kashfa ya rushwa iliyohusisha kampuni ya kuzalisha umeme ya ki-Marekani
Richmond Development Company LLC ya Houston Texas.
Hata hivyo wakati
anatangaza kuhamia kwake Chadema, Lowassa alikanusha katu katu kuhusika kwa
namna yoyote na kashfa hiyo na kudai kuwa yeye alifuata tu amri kutoka kwa
‘wakubwa’ walio juu yake.
“Kama kuna mtu yeyote
mwenye ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze” alisema Lowassa
“Kama kuna mtu yeyote mwenye
ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze” alisema Lowassa
Kuhama kwake
kunamfanya Lowassa kuwa ndie kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kabisa wa CCM
kukihama chama hicho tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania
mnamo mwaka 1992.
Mwanajeshi wa zamani
na aliyewahi kupigana wa vita kati ya Uganda na Tanzania mwaka 1978/79, Lowassa
aliiambia hadhara kwamba akiwa kama mtu mwenye uchungu na nchi yake isingekuwa
rahisi kubaki ndani ya CCM huku akiona chama hicho kimepoteza mwelekeo na sifa
ya kuongoza nchi.
Lowassa amekimbilia
upinzani baada jina lake kukatwa wakati alipoomba kuwa mgombea urais kupitia
chama tawala CCM katika uchaguzi mkuu ujao utakafanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Wakati mchakato wa CCM
wa kumtafuta mgombea wao wa urais ulipoanza, Lowassa ndiye aliyekuwa kinara wa
wagombea wote 42. Kila kona aliyozunguka, mikutano yake ya hadhara ilivutia
maelfu ya watu waliomuunga mkono.
Wakati chama cha CCM
kilimtaka kila mgombea apate sahihi za wadhamini 450 lakini Lowassa alipata
sahihi za wadhamini zaidi ya 700,000.
Wasifu wa Edward Lowassa
Hata hivyo mchujo wa
chama ulipofanyika jina lake lilikatwa mapema kabla hata ya kupelekwa kwenye
vikao vya vya juu vya chama hicho. Ambapo baadae Waziri wa Ujenzi John Pombe
Magufuli ndiye aliyeibuka kidedea na kuwa mgombea kupitia chama tawala CCM.
Lowassa ameushutumu
mchakato CCM wa kutafuta mgombea urais akiuita kuwa ulijaa chuki na mizengwe
dhidi yake, hali ambayo aliifananisha na ‘ubakaji wa demokrasia’
“Nitakuwa mnafki
nikisema bado nina imani na CCM. CCM niliyoiona Dodoma si CCM niliyokulia”,
alisema, na kuongeza “kama Watanzania hawapati maendeleo kupitia CCM basi
wakayatafute nje ya CCM”
Wakati sakala la
Richmond lilipoibuka miaka michache tu iliyopita, Chadema ilimfanya limsakama
Lowassa kuwa ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini. Lakini wakati chama hicho
kinamkaribisha kuwa mwanachama wao, kiligeuka na kusema hakuna mtu msafi nchini
na kwamba hawawezi kuacha kumpokea mwanasiasa mwenye mtaji mkubwa wa wafuasi
kama Lowassa.
Wakati akiwa Waziri
Mkuu, Lowassa alisifika kama mchapakazi hodari na msimamiaji wa moja kwa moja
wa shughuli za serikali. Bado anaendelea kufahamika kwa jina la utani la ‘mzee
wa maamuzi magumu’.
Je unamfahamu Edward Lowassa ni
nani katika siasa za Tanzania ?
Moja ya mafanikio
makubwa ya uwaziri mkuu wake ni jitihada kubwa na mafanikio ya upatikanaji wa
fedha za kujenga chuo kikuu cha Dodoma. Chuo hiki kikuu cha umma kilichopo
katikati ya Tanzania kilianzishwa mwaka 2007.
Lowassa ni mashuhuri
pia kwa kusimamia mpango wa serikali uliofanikiwa wa ujenzi wa shule za kata
ambazo uliiletea Tanzania sifa kubwa kwa kutoa fursa ya watoto wengi kupata
nafasi shuleni.
Mtoto wa Mzee Ngoyai
Lowassa, ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa serikali ya kikoloni, Lowassa ameanza
harakati zake za kuwania urais tangu mwaka 1995 lakini inaarifiwa kwamba rais
wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Nyerere alimkatalia kushika nafasi hiyo.
Wafuasi wa Lowassa wamekuwa wakiyatupilia mbali madai hayo
Ulipofika uchaguzi wa
mwaka 2005, Lowassa hakutaka kuwania urais, lakini badala yake alimnadi rafiki
yake wa siku nyingi Rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye alipata ushindi wa
kishindo wa zaidi ya asilimia 80.
No comments:
Post a Comment